Huyu huenda kweli akawa ni mwana wa Mungu aliye hai angalia Mayele, Dkt Biteko, Chalamila, Dkt Mwigulu, Dkt Samia, Dkt Tulia hata Paul Makonda


Tupunguze porojo. Tatizo ni tozo na mfumuko wa Bei.
 
Mimi nililogwa sana kwa zaidi ya miaka 15,nilitembea sana kwa waganga ila nilipofika Kawe namshukuru Mungu walau kwa Sasa hata naonekana mtu, Mwamposa ni mtumishi wa Mungu
Vp ambao wameenda sana kwa Mwamposa na hadi sasa hawajakata tamaa ila matatizo yao yako palepale?
 
N
Watoto wangu walifeli sana ila baada ya kufika Kawe namshukuru Mungu wanafanya vizuri kwa sasa darasani
Nina ndugu yangu ameshampeleka sana mwanae kwa Mwamposa ili apate kazi ila wapi, wakati mwanae anasoma alimpeleka ili afaulu mitihani ila wapi. Pamoja na yote ila bado anaamini miujiza ya Mwamposa hadi sasa.
 
Wapumbavu huhamasishana waende kule mara huku kuna miujiza, ni umbumbumbu wa SGR levels.

Duniani kote Mungu hupatikana Kawe tu? nina wasiwasi na akili zetu Waafrika kiuumbwaji...
Tafsiri ya haraka hapo Mwamposa ndio hufanywa kuwa mungu mwenyewe.
 
Mke wangu alisumbuliwa na sukari kwa mwaka mzima ila Sasa iko 5.5,amepona kabisa
Mkuu watu wanapona hadi kansa kimiujiza ambayo haitumii uchawi wala kuhusishwa imani kwa Mungu.
 
Mimi sio Mkristu ila Jumapili asubuhi Insha'allah nitafika hapo Kawe asubuhi
Kwa waganga na masheikh kutibiwa ni ghari ndio maana watu wanaenda huko wanajua wanaweza wakapona matatizo yao bure tu.
 
Aiombee TANESCO isikate umeme. Akimaliza akaiombee Taifa Stars ibebe AFCON. Mleta uzi acha kuabudu binadamu mwenzako.
 
Nabii kuna huyu mama katoka katavi, anasema mume wake ajawahi ajawahi kumnunulia hata upande wa kanga, nini kimetokea? Baada ya kufika madhabahuni pako kukanyaga keki ya upako, mume wake amemtumia meseji Mke wangu nimekununulia vitenge

Makofi kwa bwana pwa pwa pwa pwa pwa.
Nani mtenda mijuza yesu.
 
Nchi Ina matatizo lukuki... Achague hata Moja mfano umeme... Kama nabii atoe unabii wake??
Yesu alienda kwa wenye shida akawaponya... Alienda bwawani na ajatenda kwa yule asiyejiweza!
Kwanini Mwamposa hafuati nyayo aende mlongazila kuponesha wagonjwa??
 
Mimi nililogwa sana kwa zaidi ya miaka 15,nilitembea sana kwa waganga ila nilipofika Kawe namshukuru Mungu walau kwa Sasa hata naonekana mtu, Mwamposa ni mtumishi wa Mungu
Wanawake walikua wakinikataa sana. Ilihitaji niimbishe sana ndio nipewe. Hata kwa kutumia hela ilikua ngumu sometimes.

Ila saa hivi uongo mbaya mi ndo nawakimbia.
 
Kwenye ukristo ukishashikia mtu anjiita "mtume" au "nabii" ujue huyo ni shetani mkubwa wa kuogopa kama ukoma.
 
Mimi nililogwa sana kwa zaidi ya miaka 15,nilitembea sana kwa waganga ila nilipofika Kawe namshukuru Mungu walau kwa Sasa hata naonekana mtu, Mwamposa ni mtumishi wa Mungu
Watu wenye Imani haba huhangaika kwa waganga na kwa mitume.
Jiulize swali na fanya utafiti kidogo;
Katika watu wanaoishi maisha ya kawaida, idadi inayoenda kwa waganga na mitume na ile isiyoenda huko, ipi ni kubwa?
Kitu Muhimu ni kumuamini Mungu wa kweli asiyekuhitaji uende kwa mganga au wanaoitwa mitume ili akubariki.
Baraka za Mungu zinakuja moja kwa moja kwako bila kupitia kwa waganga au hao manabii wa maji, chumvi, mafuta,,.....
 
Ndugu zangu wote walioenda kwa jamaa kupata uponyaji hawajasaidika.

Nimepoteza wengi kwa kudhani mwamposa angewaponya kwa maombezi
muache ujinga, imani inaanza na nyie, kama nyie hamna imani mnadhani mtumishi huyo atafanya nini?
 
Wewe Mfuatilie Mwamposa hutajuta na imani yako itapanda zaidi ya hiyo
Mkuu, usimuangalie mtumishi Mwamposya kama mtu binafsi, bali chunguza na angalia huduma yake kwa kina kama inashabihiana na ile waliyoihubiri mitume. Ni hilo tu.

WAGALATIA 1

7 Ukweli ni kwamba hakuna Injili nyingine, ila nafahamu kuwa wako watu wanaowavuruga, ambao wanataka kuipotosha Injili ya Kristo.

8 Lakini hata ikiwa ni sisi au ni malaika atokaye mbinguni, kama mtu akiwahubiria Injili ambayo ni tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi mtu huyo na alaaniwe.

9 Kama tulivyokwisha sema kabla, sasa nasema tena, kwamba mtu ye yote atakayewahubiria Injili tofauti na ile mliyokwishaipokea, basi mtu huyo na alaaniwe.
 
Sio lazima kila mtume apitie taabu au kifo ili kuhubiri injili kama wale wa kipindi kile.

Nyakati zimebadilika .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…