Huyu huenda kweli akawa ni mwana wa Mungu aliye hai angalia Mayele, Dkt Biteko, Chalamila, Dkt Mwigulu, Dkt Samia, Dkt Tulia hata Paul Makonda

Huyu huenda kweli akawa ni mwana wa Mungu aliye hai angalia Mayele, Dkt Biteko, Chalamila, Dkt Mwigulu, Dkt Samia, Dkt Tulia hata Paul Makonda

Mimi nililogwa sana kwa zaidi ya miaka 15,nilitembea sana kwa waganga ila nilipofika Kawe namshukuru Mungu walau kwa Sasa hata naonekana mtu, Mwamposa ni mtumishi wa Mungu

Kuamini umelogwa ni ugonjwa wa akili let alone kwenda kwa Mwamposa.
 
View attachment 2849652View attachment 2849653View attachment 2849654
View attachment 2849655

Habari Tanzania,

Kwa muda sasa kumekuweko mijadala mbalimbali kuhusu Ndugu yetu Apostle Bonface Mwamposa almaarufu kama Bulldozer.

Apostle Bonface Mwamposa anahudumu katika madhabahu ya Arise & Shine au kwakimombo " INUKA UANGAZE" ( Isaya 60:1 ) yaliyoko Kawe jijini Dar es Salaam Tanzania.

Apostle Bonface Mwamposa amekuwa na wafuasi wengi wanao ongezeka siku kwa siku mwezi kwa mwezi au mwaka kwa mwaka yaani ni mamilioni kwa mamilioni ya waamini toka nje na ndani ya bara la Africa,

Apostle Bonface Mwamposa, ibada zake zote hazina Misingi ya dini au dhehebu lolote ila " IMANI KWA YESU KRISTU NA MUNGU ALIYEMTUMA "


Apostle Bonface Mwamposa, anahudumia wakristo kwa Waisilamu hata wale wote wasio na dini kabisa kama akina Yeriko Nyerere nao pia wakiamini wanapokea uponyaji wa mwili na roho pamoja na haja zao kutimilizwa na Mungu wa Boniface,

Apostle Bonface Mwamposa, ndiye aliyemwambia Dkt Willium Ruto kwamba "Nenda Utashinda Uchaguzi" na mishowe Ruto akashinda Urais,

Bila Mungu ilikuwa ni ngumu sana mtu kama Mhe Willium Samoi Ruto kuwashinda Mhe Raila Omolo Odinga na Kenyatta Uhuru ila Mungu wa Boniface akafanya jambo pale Kenya na Dunia ikashangaa,

Apostle Bonface Mwamposa, Ndiye aliyemwombea Dkt Tulia na akashinda kuwa Spika wa mabunge yote Duniani ( IPU ) hata Leo,

Apostle Bonface Mwamposa, ndiye aliyemwombea kaka yetu Fiston Kalala Mayele na akawa mchezaji bora wa wakati wote Nje na ndani ya Tanzania nadhani sote tunakumbuka huyu kijana anayechezea Pyramids hivi Sasa,

Orodha ya waliosaidiwa na Mungu kupitia kwenye kinywa Cha Apostle Bonface Mwamposa ni wengi wengine wanakwenda kwa Siri na hawashuki kwenye magari yao ila wanatendewa japo ni ujinga kujificha au kuficha matendo ya Mungu wakati kwa waganga mnakwenda tena waziwazi.

Hoja yangu hapa ni , Je? Mwamposa kwa kuzingatia mafundisho yake na upako alionao huenda ni kweli huyu bwana akawa ni mwana wa Mungu ila sisi imani zetu zimekamatwa na shetani na hivyo tunashindwa kutofautisha kati ya kazi za shetani na kazi za Mungu?
====

Kama hujawahi kwenda au kumsikiliza Apostle Bonface Mwamposa jipe muda wa kumfuatilia kabla hujamsema vibaya,


MFuatilie: Azam channel No 469
Startimes No 117

You tube: Mwamposa Live
: Arise & shine Tanzania

Instagram: Arise & shine Tanzania
Anaweza kuwa mtumishi wa Mungu anayehitaji Roho Mtakatifu kumwongoza kutibu Roho za watu kwanza.Mungu anajali sana mioyo ya wanadamu kumrudia yeye kutoka utumwa mwa dhambi zetu.Mungu anasema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu ndipo na hayo mengine mtapewa.Hata hivyo Mwamposa si kama wengine
 
Hapana wewe ni muongo kama hujui Kaa kimya tena kuwa kimya kabisa yatakupata mabaya sana
Naonngea kitu cha kweli, nenda pale nje kawaulize wale wapika chakula watakuambia, tena mwamposa aliwapa ela kufidia vitu vyao vilivyovunjwa na yule kichaa
 
Back
Top Bottom