Huyu mdada nlikutana nae kwenye sherehe ya harusi ya ndugu yangu, kuulizia ulizia, nkatambulishwa kuwa alikua ni family friend wa ndugu yangu tena anaishi jirani na mtaa anaoishi ndugu yangu, alinivutia, nikamwomba namba akakubali, tukawa tunachat, tena cku ingine anaanza yeye kunitext , ndani ya siku 4, siku ya 5, nika-set a date akaja, tukakutana kwenye mgahawa mzuri, mm nkaagiza sprite yeye akaagiza juisi, nkamweleza nia yangu, akaonesha kukubaliana na mm, baada ya hapo akanisindikiza..nkasepa
Sasa nkamwambia aje gheto kwangu apajue alisema atakuja baada ya wiki 1, kabla ya hio siku ya yeye kuja gheto kufika, akanitext akaniambia ana shida ya tsh elf 10 nimtumie, nkamwambia asijali, akija gheto ntampa zaidi ya hiyo tsh elf 10, akasema hapana anaihitaji kwa muda huo, nkamwambia akope sehemu ingine akija gheto hata tsh elf 40 ntampa na nauli ntamrudishia Mara mbili yake..kiuhalisia mm uwezo wa kumpa hata tsh elf 70 nlikuwa nao, Akasema haya..
Tangu siku hiyo alinichunia, SMS zangu hakujibu tena, simu zangu hapokei, na gheto hakuja tena sasa wazee mm kosa langu lilikuwa nn hapo, maana hata nlivomtongoza nlienda kawaida, sikujifanya Nina hela..