Huyu mhalifu wa Selander alipaswa kukamatwa, siyo kuuawa
Acha wawe hivyo hivyo. Ni mpango wa Mungu. Vinginevyo wataanza kuwalenga akina Lissu, Heche, Mbowe... Hao wanaonekana kuwa maadui wao wakubwa kuliko magaidi halisi. Yule wa jana eti wanamwita mhalifu halafu Mbowe eti gaidi!
Kuna haja ya jeshi letu kuunda kikosi cha marksman Mahiri na kuwamotisha!
 
Jamaa hana mafunzo makubwa. Askari wanaonekana kukosa weledi na woga kupita kiasi.

Jamaa alikuwa open wamepiga risasi zaidi ya 20 wakimkosa kihasara jamaa ambaye yupo open na polisi wapo zaidi ya 10. Wanakimbia kimbia tu.

Ni udhaifu yeye ambaye hana mafunzo makubwa kuwapora askari smg na kuendelea kuwatandika kuua wanne. Mtu mmoja wamejibishana naye kwa nusu saa nzima. Wangekuwa watatu na wenye uwezo mkubwa?

Kwa woga wa polisi walishindwa hata kum netraulize wampate akiwa hai kwa mahojiano. Wamempiga risasi kaangua badala ya kufanya utaratibu wa kumpata hai wanaendelea kumpiga risasi mtu ambaye tayari isnt a threat. Ni woga. Woga wa hali ya juu.

Inaonekana waliendelea hata kuimiminia risasi maiti huko mbele wakiwa hawaamini kama jamaa amefariki.

Huyu alipaswa akamatwe mzima. Angepigwa risasi miguuni au sehemu ambayo isingemlazimisha kufa. Then wange mchukua kumtibu na kuja mhoji awaeleze kisa na mkasa.

Polisi acheni kuwa mnaonea tu raia wasio na silaha. Huyu jamaa ndo alikuwa kipimo chenu tosha.
 
Huwezi kunyanyua mkono juu una silaha mkono mwingine. Alikuwa anataka wafariki askari wengi zaidi?

Kama alitaka yaishe angeweka silaha chini na kunyanyua mikoni yote juu na kutoka eneo iliyopo silaha hata mita kadhaa ambazo kweli kila mtu angeona jamaa hana nia tena na mapambano.
Watu wanasikitika sana Hamza kuondoka na askari wawili pekee
 
Watu wanasikitika sana Hamza kuondoka na askari wawili pekee
Kwavile waliofariki siyo ndugu zao au? Kuna siku tukio la hivi litatokea na kugusa mioyo yao ndipo watang'amua umuhimu wa hao askari wanaowaona ni wajinga.
 
Jamaa unataka kunitia HASIRA sasa.

Mtu kaua askari wawili na anapambana na wengine unataka apewe wito wa kuweka silaha chini au kulala kifudifudi?

Kama alitaka kujisalimisha angeweka silaha chini kusonga mbele akiwa kaweka mikono juu.

Serikali sisitizeni matumizi na kilimo cha mbogamboga wananchi wenu wanawehuka huku.
Kama hutumii akili hasira hazitokosekana.

Hata kama alishaua Kijiji chote unadhani kumuua ndio suluhisho?

Mtu akishanyoosha mikono juu ni juu yako wewe kumuamrisha unavyotaka, akikataa kutii amri ndio hatua nyingine zinaendelea.

Huenda wewe ni Askari na napoteza muda kubishana nawe...Ila nikwambie tu kuna manufaa mengi ya kutanguliza weledi dhidi ya mihemuko..
 
Sikulaumu hayo ni mawazo yako ila tambua bunduki km AK47 au SMG hawashiki askari wa kawaida angalia yule jamaa alishika silaha ya aina gani na kawaida maaskari hutumia silaha ya aina gani.

Halafu angalia Tanzania ni nchi ya aina gani. Hii nchi ilizoea amani na tulikaa muda mrefu hatuna bugudha leo hii mtu km yule atokee unadhani inakuaje?

Tulishazoea amani na utulivu.
 
Haya mambo mnayasema kwa sababu hamuijui Bunduki. Haiwezekani na haitatokea mtu kujua kwamba anaepambana nae ameishiwa Risasi. Lakini pia kumbuka asui yule alikuwa akiua askari haiwezeka umuamini kuwa ameishiwa risasi na amesalenda
Askari wana mafunzo, sasa kama nao wanwaza na kutena kama Watu baki basi hakuna haja ya kuwa na Jeshi la Polisi.

Wanatakiwa watangulize uwezo wa kumkamata kwanza bila kujali Muhusika anatisha kiasi gani...sasa kama unataka nao walielie kuwa eti huyu Mtu ni hatari basi hatuna Jeshi la Polisi tuna kundi tu la Watu.
 
Kama hutumii akili hasira hazitokosekana.

Hata kama alishaua Kijiji chote unadhani kumuua ndio suluhisho?

Mtu akishanyoosha mikono juu ni juu yako wewe kumuamrisha unavyotaka, akikataa kutii amri ndio hatu nyingine zinaendelea.

Huena wewe ni Askari na napoteza muda kubisha nawe...Ila nikwambie tu kuna manufaa mengi ya kutanguliza weledi dhidi ya mihemuko..
Kumuua halikuwa suluhisho bali askari walitakiwa wamuache na aendelee kuwauwa hadi waishe wote.

Askari hawakutumia weledi walitakiwa kuacha jamaa awapige risasi hadi ziishe kisha arudi nyumbani kwake kulala.

Weledi ni kumpa ruhusa afyatue risasi kwa askari hata mimi nasikitika kwanini hakupewa nafasi hiyo.

Umefurahi sasa?
 
Kwakweli vifo vya polisi jana na yule mlinzi wa kampuni binafsi ni jambo la kusikitisha sana.

Hawa watu wana familia zoa, wake na watoto huko nyumbani, inasikitisha kwamba baba kaenda kazini lakini hatorudi kamwe nyumbani akiwa hai.

Pamoja na hayo, polisi waliokwenda kukabiliana na Hamza walionesha madhaifu ambayo ni muhimu yafanyiwe kazi. Kuendelea kumpiga risasi mtu ambaye tayari yuko chini sio sawa kabisa.

Pia kama kuna uwezekano wa kumkamata mhalifu akiwa hai pasipo kuhatarisha maisha ya askari, lazima hicho kiwe kipaumbele badala ya kuua tu.
 
Kama ni movie basi jamaa ameshinda japo kafa

1.Kwanza katawala eneo la tukio kwa muda wa zaidi ya nusu saa( most secured place.. balozi..TISS office..bank..polisi

2.kapokonya silaha mbili na kuua Askari 3 na mlinzi mmoja..

3.Kajisalimisha wamuue na wakamuua kweli...nadhani ilikuwa ni motive yake baada ya tukio

Polisi wetu wajitathmini katika hili
 
Kuna Watu hata sijui kama mnaelewa kile mnachobishania.

Tunaongelea Weledi wa Askari na si Watu wa kawaida.

Askari wasio na Weledi na umahiri wa kazi si hatari tu kwa Wahalifu, bali ni hatari kwa Jamii yote.

Mnachangia tu kishabiki kama vijiweni lakini mkumbuke wanaoweka sheria kali kuwadhibiti Polisi ni kwa sababu wameshaona madhara ya Polisi kufanya kazi kiholela.

Hasira za kumuua Mtu kwa kuwa tu kamuua Ndugu yako ndio kunamrudisha huyo Ndugu?...na hapa tunazungumzia Askari mwenye kazi yake, sio raia tu....anapaswa kutanguliza akili sio kulipiza kisasi.
 
Sikulaumu hayo ni mawazo yako ila tambua bunduki km AK47 au SMG hawashiki askari wa kawaida angalia yule jamaa alishika silaha ya aina gani na kawaida maaskari hutumia silaha ya aina gani.
Halafu angalia Tz ni nchi ya aina gani.
Hii nchi ilizoea amani na tulikaa muda mrefu hatuna bugudha leo hii mtu km yule atokee unadhani inakuaje?
Tulishazoea amani na utulivu.
Kwani silaha alizotumia si ni SMG, ambazo aliwanyang'anya hao maaskari aliowaua?inshu sio kuwa Tz, ni nchi ya namna gani ndio kuhalalisha mapungufu yaliyopo kwenye vyombo vya ulinzi?siku zote hapa huwa tunalindwa zaidi na MUNGU, tu lakini kila sekta ni hoi tu mala ngapi majanga kila yanapotokea ndipo tunashituka?utaona kuanzia leo kutakuwa na mabadiriko makubwa kwenye vibanda vya kumpuzikia askari,ki utendaji lakini subili baada ya mwezi, kama kawaida!na ndio maana linapotokea tukio kama lile huwa ni kupagawa, , pale na kituo cha salenda bridge kuna umbali gani?lakini ulizia muda waliotumia kufika pale!?na bahati nzuri jamaa hakuwa na shida na raia wa kawaida, ingekuwa maafa.
 
Back
Top Bottom