Nikupe tu ushuhuda, miaka 12 iliyopita nilimtuma mke wangu kwenda mkoa x kununua shamba, huku akiwa na kiasi cha cash mkononi.
Alipofika kule alichukua lodge, akalipia na baadaye akaenda kukagua shamba na akanipa taarifa za kimuonekano.
Ile anarudi lodge akakutana na mkongo ambaye alijitambulisha ni mganga na yeye amefikia kwenye hiyo lodge, na yupo kule kwa ajili ya kuuguza watu
mbaya zaidi, yule mkongo akawa anamwambia mke wangu abc za maisha yetu na ndugu, na ni kweli alikuwa anasema ukweli.
Akamshawihi kuwa atampa dawa ili changamoto zilizopo ziishe.
Baada ya wife kunijulisha kwa njia ya simu,nilipata mashaka na kuwasiliana na ndugu zangu pamoja na wakwe zangu
Baada ya dakika 20 nilipata majibu,kuwa yule mtu si mzuri ameshamtamani mke wangu, na anataka aende naye nairobi, na hapo alipo kiimani ameshabadilishwa bila yeye kujijua
Niliambiwa anatakiwa aondoke huko aliko bila kuchelewesha muda
Kilichofanyika, muda huo huo ilibidi nimuambie aanze safari iwe kwa kukodi teksi mradi afike eneo fulani; kwa hiyo ile hela ya shamba ilitumika kwa nauli.
Baada ya kufika kwa ndugu zake na kupelekwa kwa wazee, kuna dawa alifukiziwa na alizimia kama nusu saa, ikiwa na maana ule uchafu aliopewa unatakiwa urudi ulikotoka.
Baada ya kuzinduka, mkongo alimpigia simu na kumuuliza umenifanyia nini.
Wazee wakasema block hiyo namba na iwe fundisho kwake.
Nachotaka kusema, usipokee kitu, ikiwezekana fanya maombezi utoe huo uchafu aliokutumia.