mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,995
- 3,402
Ufafanuzi alikwisha utoa kitambo sana ,ni hivi yeye huwaomba wafanyabiashara na taasisi baadhi zenye ukwasi kumsaidia pesa anapotaka kufanya jambo la kusaidia jamii, taasisi , wafanyabiashara hata watu wakawaida tu, humpatia bila mashariti na wengine hawapendi kujitangaza ila huweka rekodi zao sawa,mfano marehemu Mengi.Nadhani watumishi wote wa serikali mshahara wao unajulikana, lakini inapokuja mtu mmoja anatoa misaada ambayo ipo nje ya mshara wake, inaleta uwalakini. Mtu huyu amekuwa akifanya kazi nzuri sipingani na hilo, ni mtumishi ambaye kiwango chake kinajulikana kwa mwezi kama wakuu wa m*** wengine. cha kushangaza ukimuangalia bado ni kijana mdogo ambaye ni majuzi juzi tu ameingia serikalini ingawa ana kinga na namba one.
Hana biashara kama akina Mo ya kusema kuwa hela zake anazivuna kutoka huko.
Sitamtaja jina ila ametangaza tena baada ya Taifa Stars kushinda jana atampa golikipa milioni kumi, sina chuki na hilo la kuhamasisha, ni vizuri sana kufanya hivyo lakini katika fungu gani hizi hela unazogawa gawa unazitoa? Asante kwa kujitolea kuwatibu wagonjwa tofauti, kuwatolea michango kwenda kutibiwa ndani na nje ya nchi, kuhamasisha katika michezo, tena nia yako ni ya kuigiwa ila mkuu pato lako ni lipi?
Mbona wenzako ambao ni wakuu wa *****kama wewe huko mi*** kwao hawatowi misaada kama hiyo, na tunajua mishahara yenu ni sawa sawa. Wabunge, Mawaziri, Wafanyabiashara wote hawana kapu la hizi hela la kutoa misaada kama hii. Nisiwachoshe la msingi huyo mheshimiwa, na mtumishi mkuu, anatoa pesa wapi za kutoa misaada ni kodi zetu au...?
CC: BAK, Mshana jr, Tindo.
Kama wewe huwezi toa na saidia wapo wakielezwa wako tayari kutoa kwa moyo mmoja .
Ulichokileta hapa ni kutaka kupika majungu,ndicho tulichobaki nacho watanzania kama mtaji wetu