Huyu mtumishi wa Serikali anatoa wapi pesa za kutoa misaada kwa jamii?

Huyu mtumishi wa Serikali anatoa wapi pesa za kutoa misaada kwa jamii?

Kwenye msako wa vyeti fake walisema siyo mtumishi wa serikali ila ni kiongizi wa siasa hivyo wakakwepesha asikaguliwe vyeti vyake
 
Mkuu hizi ni pesa zetu walipa kodi zinazochotwa kinyemela na kubwa la majizi AKA kichaa jiwe pale hazina kupitia VOTE 20 na VOTE 30. Ndiyo sababu huyo bashite hawezi kuguswa maana anazijua siri nyingi zilizojaa maovu ya kutisha yanayofanywa na Bugiri. Na Bashite ndiyo mbeba mazabe yote ya Bugiri.
ndo maana amejaa minoti ambayo anamwaga nje na mshahara wake na hakuna wa kukohoa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu yeye ameamua kuhoji hizo za Kaseja, ww ulitakiwa ulete hizo habari za mema. Ila hata kama ni mema inapaswa chanzo kieleweke isije ikawa mtu akauza unga akatoa ili kutakatisha pesa chafu.
hiyo ndo pointi mkuu, ina maana anawaziba hata wauza unga wamletee gela kwa kisingizio kuwa atatoa msaada kwa jamii kumbe hela yenyewe ni chafu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hili ni jukwaa la siasa ndio maana huu uzi uko huku, asingehoji kisiasa ungekuwa kwenye jukwaa la mapenzi au lingine husika.
hahahahaaa, hilo jibu, asante kwa kunijibia mkuu, atakuwa ameelewa.
 
Kutoa misaada siyo lazima uwe na mamillioni...

Unaweza tafuta wafahdili na wahisani wakukupa hizo pesa nawe ukazitoa kama misaada...


Cc: mahondaw
 
huo ni wivu tu, nawewe ungekua na kipaji cha faida ungepongezwaaa....kiongozi anapatia wapi pesa hayakuhusu kwani kila mtu anajua anavyopambana kupata kipato chake
 
Ndugu kwani ukiwa mtumishi wa Umma hurusiwi kujiendeleza kiuchumi kupitia kilimo, ufugaji nk?
 
Nadhani watumishi wote wa serikali mshahara wao unajulikana, lakini inapokuja mtu mmoja anatoa misaada ambayo ipo nje ya mshara wake, inaleta uwalakini. Mtu huyu amekuwa akifanya kazi nzuri sipingani na hilo, ni mtumishi ambaye kiwango chake kinajulikana kwa mwezi kama wakuu wa m*** wengine. cha kushangaza ukimuangalia bado ni kijana mdogo ambaye ni majuzi juzi tu ameingia serikalini ingawa ana kinga na namba one.
Hana biashara kama akina Mo ya kusema kuwa hela zake anazivuna kutoka huko.

Sitamtaja jina ila ametangaza tena baada ya Taifa Stars kushinda jana atampa golikipa milioni kumi, sina chuki na hilo la kuhamasisha, ni vizuri sana kufanya hivyo lakini katika fungu gani hizi hela unazogawa gawa unazitoa? Asante kwa kujitolea kuwatibu wagonjwa tofauti, kuwatolea michango kwenda kutibiwa ndani na nje ya nchi, kuhamasisha katika michezo, tena nia yako ni ya kuigiwa ila mkuu pato lako ni lipi?

Mbona wenzako ambao ni wakuu wa *****kama wewe huko mi*** kwao hawatowi misaada kama hiyo, na tunajua mishahara yenu ni sawa sawa. Wabunge, Mawaziri, Wafanyabiashara wote hawana kapu la hizi hela la kutoa misaada kama hii. Nisiwachoshe la msingi huyo mheshimiwa, na mtumishi mkuu, anatoa pesa wapi za kutoa misaada ni kodi zetu au...?

CC: BAK, Mshana jr, Tindo.
Dah nimechelewa kuiona hii mada... Ngoja nitarejea
 
Mkoa huu una Watanzania wengi wenye asili ya Asia, huenda hujumuika nao kule Jamatini na ndipo humpa tafu la ngawira, ama pia anaweza kanisa lake "Kolomije Revival Church" na yeye ndiye mbeba maono na kapu la sadaka. Huwezi jua mazee.
 
Mkoa huu una Watanzania wengi wenye asili ya Asia, huenda hujumuika nao kule Jamatini na ndipo humpa tafu la ngawira, ama pia anaweza kanisa lake "Kolomije Revival Church" na yeye ndiye mbeba maono na kapu la sadaka. Huwezi jua mazee.
kwa hiyo ndiko anapata mlungula wa kutoa zawadi
 
Back
Top Bottom