Huyu mtumishi wa Serikali anatoa wapi pesa za kutoa misaada kwa jamii?

Huyu mtumishi wa Serikali anatoa wapi pesa za kutoa misaada kwa jamii?

kumbuka huyu siyo mfugaji wa ng'ombe, ulaji wake unategemea kodi yako
Mfugaji kumkatia mwanae wa miaka 15 ng'ombe elfu mbili ni kitu kidogo sana wala hakuna mjadala kwao, sasa sijui kama unaujua mgao aliopewa na baba yake.
 
Dogo anapofanikisha upatikanaji wa pesa za kuwapeleka watoto nje kwenda kutibiwa, huyu mleta mada haleti uzi jukwaani, ila masuala ya Kaseja ndio yanapewa umuhimu. Roho ile ile ya kwanini.

Phillipo hapo hela ni imetumika kufanya nini ni inatoka wapi?
 
Phillipo hapo hela ni imetumika kufanya nini ni inatoka wapi?
Mleta mada anahoji pesa aliyopewa Kaseja shilingi milioni kumi baada ya kuokoa penati.

Atajua mwenyewe anazitoa wapi, lakini anapofanya mema ni kama hayaonwi na kuanzishwa uzi humu JF, ni aina fulani ya roho zetu za kiafrika, unachagua cha kuhoji.
 
Mfugaji kumkatia mwanae wa miaka 15 ng'ombe elfu mbili ni kitu kidogo sana wala hakuna mjadala kwao, sasa sijui kama unaujua mgao aliopewa na baba yake.
hapo nimekusoma kwa mbaaaali mkuu, ni kweli huo mfano upo hai kwa jinsi mambo yanavyoenda
 
kwa hiyo hii yeye huwa anapewa na wafanya biashaea kama zawadi au kama hela yake ya kujikimu, make mfanyabiashara yyte lazima alipie kodi iweje wampe mkuu wa mkoa?
kama anazifuataga kwa adabu uku kainama kuna tatizo tena anaenda kinyume nyume.
 
Mkuu hizi ni pesa zetu walipa kodi zinazochotwa kinyemela na kubwa la majizi AKA kichaa jiwe pale hazina kupitia VOTE 20 na VOTE 30. Ndiyo sababu huyo bashite hawezi kuguswa maana anazijua siri nyingi zilizojaa maovu ya kutisha yanayofanywa na Bugiri. Na Bashite ndiyo mbeba mazabe yote ya Bugiri.

Nadhani watumishi wote wa serikali mshahara wao unajulikana, lakini inapokuja mtu mmoja anatoa misaada ambayo ipo nje ya mshara wake, inaleta uwalakini. Mtu huyu amekuwa akifanya kazi nzuri sipingani na hilo, ni mtumishi ambaye kiwango chake kinajulikana kwa mwezi kama wakuu wa m*** wengine. cha kushangaza ukimuangalia bado ni kijana mdogo ambaye ni majuzi juzi tu ameingia serikalini ingawa ana kinga na namba one.
Hana biashara kama akina Mo ya kusema kuwa hela zake anazivuna kutoka huko.

Sitamtaja jina ila ametangaza tena baada ya Taifa Stars kushinda jana atampa golikipa milioni kumi, sina chuki na hilo la kuhamasisha, ni vizuri sana kufanya hivyo lakini katika fungu gani hizi hela unazogawa gawa unazitoa? Asante kwa kujitolea kuwatibu wagonjwa tofauti, kuwatolea michango kwenda kutibiwa ndani na nje ya nchi, kuhamasisha katika michezo, tena nia yako ni ya kuigiwa ila mkuu pato lako ni lipi?

Mbona wenzako ambao ni wakuu wa *****kama wewe huko mi*** kwao hawatowi misaada kama hiyo, na tunajua mishahara yenu ni sawa sawa. Wabunge, Mawaziri, Wafanyabiashara wote hawana kapu la hizi hela la kutoa misaada kama hii. Nisiwachoshe la msingi huyo mheshimiwa, na mtumishi mkuu, anatoa pesa wapi za kutoa misaada ni kodi zetu au...?

CC: BAK, Mshana jr, Tindo.
 
Mleta mada anahoji pesa aliyopewa Kaseja shilingi milioni kumi baada ya kuokoa penati.

Atajua mwenyewe anazitoa wapi, lakini anapofanya mema ni kama hayaonwi na kuanzishwa uzi humu JF, ni aina fulani ya roho zetu za kiafrika, unachagua cha kuhoji.

Mkuu yeye ameamua kuhoji hizo za Kaseja, ww ulitakiwa ulete hizo habari za mema. Ila hata kama ni mema inapaswa chanzo kieleweke isije ikawa mtu akauza unga akatoa ili kutakatisha pesa chafu.
 
Hili ni jukwaa la siasa ndio maana huu uzi uko huku, asingehoji kisiasa ungekuwa kwenye jukwaa la mapenzi au lingine husika.
Unafiki tu, ina maana kazi ya Juma Kaseja jana unaweza kulinganisha na shilingi milioni kumi za RC wa Dar?.

Mleta mada anaelewa maana ya ushindi wa timu ya taifa na kuingia hatua ya makundi ya kuelekea Qatar 2022?.
 
Duuu, kwa hiyo ukifanya kazi kubwa unaweza pewa pesa isiyofahamika inatoka wapi?
 
Duuu, kwa hiyo ukifanya kazi kubwa unaweza pewa pesa isiyofahamika inatoka wapi?
Mleta mada aende pale ilala boma ofisini kwa Makonda atapewa taarifa ya zilipotoka pesa, kuandika uzi uliokaa kimajungu hakuwezi kutusaidia sisi wasomaji na watoa maoni.
 
Back
Top Bottom