Tatizo kubwa sana ninalolishuhudia kwa Watanzania wengi ni ujinga mbaya, tuelewane kuwa ujinga siyo tusi, ujinga ni sifa ya kutokuelewa. Sifa inaweza kuwa nzuri au mbaya, sifa ya ujinga mbaya ni ile ya kutokuelewa kuwa huelewi, sifa nzuri ya ujinga ni ile ya kutokuelewa lakini unafahamu kuwa huelewi.
Ukishaelewa kuutofautisha ujinga katika sifa nzuri na mbaya basi itakuwa wepesi sana kutokana na ujinga mbaya mwingi na kubaki na ujinga mzuri mchache wa yale mapya usiyoelewa. Na namna ya kuufuta ujinga mbaya ni kujifunza kile usichokielewa, ukishakielewa ina maan hu mjinga tena kwenye hicho unabaki kuwa mjinga katika kile tu ambacho hujajifunza.
Mfano mzuri tena ni mfano hai, ni huu wa sakata la bandari. Wengi tunajifanya tunaelewa kumbe hatuelewi chochpote, tunakuwa washitaki sisi, watowa hukumu sisi, waadhibuji sisi, wachimba makaburi sisi ya tuliowahukumu sisi. Siyo vibaya yote hayo, si ndiyo tunafanya kazi zote hizo kwa bidii, hatungoji kufanyiwa, au sivyo? Ni sifa kubwa hiyo.
Lakini ni sifa ya ujinga mbaya, sana tena sana. Kwa sababu huyo tunaemhukumu hatumjuwi. Tunamhukumu bila hata ya kumuona. Ujinga mbaya unazidi pale aliyekwenda kumuona, akmjuwa huyu ni nani, anafanya nini, tunamuona yeye ni mjinga. Nadiriki kusema tulionao ni zaidi ya ujinga mbaya, ni uhayawani kabisa.
Anaebisha atwambie, yeye kishafanya biashara ipi inayohusu bandari? Na kishafanya na nani? na kaifanya wapi?
Kama hana qualification hata kidogo za kuyajuwa hayo, na haujafanya hata utafiti japo kidogo wa kupata uelewa wa hayo, basi huna haki ya kunyanyua mdomo. Mao Tse Tung alisema "haujanya tafiti hauna haki ya kuongea". Nyerere alisema mmoja katika maadui zetu ni ujinga. Na mimi nakubaliana nae kwenye hilo 100%, nisichokubaliana nae ni zile sifa nyingine za maadui zetu. Nna sababu yangu moja tu ya kuzikataa hizo. Nayo ni kuuta ujinga, naamini tukifuta ujinga zile sababu zake mbili zingine hazitakuwepo tena.
Ambae hajafanya biashara za kimataifa au hata za kitaifa zinazohusiana bandari na ambae hajafanya japo utafiti wa anachokipinga katika sakata la bandari, hana haki ya kupinga na hana haki hata ya kufunguwa mdomo wake, yeye akubali tu, awawachie waliokwishafanya biashara hizo na au waliokwishafanta tafiti kwenye hilo.
Mimi napinga wajinga wote wanaopinga kijinga kwenye sakata hili. Haya, leta ujinga wako tuupime hapa ni ujinga mzuri au ujinga mbaya.