Huyu Mwanajeshi aliyekuwa akihutubia leo si ndiyo yule muuza madafu wa Ikulu, au?

Kapteni wa Jeshi anayeuza Madafu.
TPDF kuna idara ya upelelezi wa ndani na upelelezi wa nje, Kwa ufupi nje hupelekwa wafanyabiashara kama kawaida au bloggers, au madreva malori, ndani ndio hubakia bodaboda, malaya, walimu, manesi, makuli, mafundi ujenzi na kadhalika na askari hufanya kazi Kwa weledi haijalishi ana rank gani ya cheo, ( MI) , ulinzi wa nchi sio lelemama hadi wauza mkaa wapo, na kila jeshi kuanzia polisi, uhamiaji, magereza, zimamoto, na kadhalika wote hao wana vitengo vya intelijensia na hubadirishana taarifa inapobidi hadi kwenye mashirika ya umma kote hao wapo
 
Alikuwa anauza madafu lini..
Wakati wa mfungo wa ramadhan raisi Samia aliandaa iftar ikulu wakatafutwa wauza madafu vijana zaidi ya watatu wanaenda kywanjibgea madafu waalikwa.
Kisha zikatoea picha raisi kapita walipo kawasalimia na kuwakaribisha Ikulu.
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Ni yeye huyo huyo.
Lakini, Je, maigizo ya namna hii yana faida gani kwa uchumi wa nchi na Wananchi wake?
Kwa mtazamo wa haraka-haraka utaona kama hakuna faida yeyote ... lakini ukizingatia hoja ya nchi kuwa kwenye Usalama, Amani na Utengamano utagundua kwamba huyo jamaa alikuwepo hapo kwa kazi maalum na sio kuuza madafu. Kuuza madafu ilikuwa ni kuhalalisha uwepo wake hapo na kuwapoteza malengo wanoko endapo walikuwepo. Hilo lilikuwa ni Mkakati maalum. Si umeona watu mwanzoni walihoji na kukomenti eti kuuza madafu Ikulu ni kuidhalilisha nchi? Labda kwa sasa watakuwa wamepata mwanga.
 
Umenikumbusha maigizo ya mchoma mahindi alipomuuzia Magu hindi la kucoma kule Dumila, naye akalila hadharani huku walinzi wake wakimtazama tu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…