Ndugu zangu Watanzania,
Uchunguzi wa kina nimeufanyika na kuona kuwa muuza madafu aliyeonekana katika viwanja vya ikulu na Mwanajeshi kutoka kikosi maalumu cha Makomando waliofanya maonyesho siku ya leo ya kuazimisha miaka 60 ya Muungano ni watu wawili tofauti kabisa. Na hapa chini ndio vitu nilivyotizama kwa ukaribu na kuonesha siyo mtu mmoja.
Cha kwanza ni pua zao ukitizama kwa ukaribu na kwa umakini unaona kabisa pua zao zinatofautiana na wala hazifanani hata kidogo.angalia upana na urefu wa pua zao,angalia muonekano na muundo wa pua zao kutoka chini ya macho mpaka eneo zinapotanukia na ukaaji wa matundu yote mawili ya pua kwa kila mmoja.
Pili ni mdomo tizama midomo yao ilivyo kwa ukaribu, tizama ukaaji wa lipsi zao katika picha ambazo ziliwachukua wakiwa wamefumba midomo tizama mkao wa midomo yao kutoka eneo la chini kidogo ya pua kushuka chini.
Tatu ni muonekano wa sura kuanzia mashavu,paji la nyuso zao wote wawili, ukubwa wa macho yao na ukaaji wa macho ikiwa ni pamoja na muonekano wake katika kuingia ndani.na namna wanavyoonekana katika picha zilizowachukuwa wakiwa wamefumba midomo.
Haya kwa uchache tu ukiyaangalia unagundua kuwa watu hawa ni watu wawili tofauti kabisa.na siyo kweli kwamba ni mtu mmoja.
Picha nazileta muda siyo mrefu.
Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.
MAMA ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili kutokana na uchapa kazi wake uliotukuka.