Maswali mazuri hayo.
Tuanze na fasili kwanza.
Martial arts ni nini? Ni sanaa za mapigano.
Sanaa hizo ni masumbwi [boxing], mieleka [siyo ile ya WWE ya akina Bianca Belair😉], kickboxing, jiu-jitsu, judo, karate, aikido, n.k.
MMA [Mixed martial arts] ni nini? Ni mchanganyiko wa hizo sanaa za mapigano na kutengeneza mchezo au mashindano yanayohusisha hizo aina zote za mapigano.
Kwenye MMA unaruhusiwa kumpiga teke mshindani wako. Unaruhusiwa kumpiga kifuti. Unaruhusiwa kumpiga kipepsi. Unaruhusiwa kumpiga kabali. Unaruhusiwa armbar [sijui Kiswahili chake]. Unaruhusiwa heel hook [sijui Kiswahili chake]. Unaruhusiwa kurusha mangumi.
Kwa ufupi, kwenye MMA unaruhusiwa kutumia mbinu nyingi kumshinda mpinzani wako.
Askari wa special forces, wanafunzwa basics tu [mambo ya msingi] za kujihami, basi.
Hapigani kikweli kweli. Anapewa tu hiyo elimu ikitokea anaihitaji, ataitumia kujinasua kutoka kwenye mbananisho.
Professional MMA fighter, yeye ndo ajira yake hiyo. Kupigana na MMA fighters wengine kwenye mashindano.
Sasa, kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu kupewa mafunzo ya msingi ya kujihami na mtu ambaye ajira yake ni kupigana ili aweze kulipwa ujira.
Na ndo maana ni nadra sana kukuta mtu aliyepo au aliyewahi kuwa kwenye special forces kufanya vizuri kwenye mashindano ya MMA.