Teslarati
JF-Expert Member
- Nov 21, 2019
- 2,621
- 10,466
Wanawake jifunzeni basi, hata kama mme wako nakushirikisha mara chache kwenye deals zangu za biashara usijiweke uhusika ambao sijakupa. Kuna mwanamke nimezaa nae na anakaa kwenye nyumba yangu huko mkoani, mimi nipo zangu hapa Town nimeajiriwa ofisi fulani na nimepanga ila mara kwa mara huwa natuma watu wakachukue au wapeleke hela zinazotokana na business pale nyumbani.
Shida ilianza huyu mwanamke akataka kufungua saloon nikasema 'no' sababu najua madada wa saloon wanalika sana. Baadae kelele zikawa nyingi nikaamua kumfungulia ila kwa masharti kwamba asije akachanganya pesa kutoka kwenye biashara zangu nyingine akaweka huko saloon bila kuniambia.
Sasa hesabu za mwezi wa tatu hazikuwa sawa kwenye kibanda changu kimoja cha MPesa, dogo wa pale akawa haeleweki. Ikatokea nafasi nikarudi mkoani wiki kama mbili zimepita, kumbana yule dogo ndo akasema "Shemeji alichukua hela akasema nisikwambie atarudisha ndani ya wiki moja" lakini muda umepita hadi mie nilipokuwa narudi alikuwa hajarudisha hio hela,
Shida kubwa sio kuchukua hela, shida kubwa ni kutoniweka wazi na kuvunja makubaliano yetu kwamba asichanganye hela zangu na biashara zake.
Argument na huyu mwanamke ikawa kubwa ndipo nikamwambia "Mimi nataka mke wala sio business partner", Naona kanikasirikia, nikasema unakasirika eenh, nikafunga saloon yake hapa nilipo nishamkabidhi dalali auze kila kitu ili huyu mwanamke atulie nyumbani.
Jana ndo nimeanza safari ya kurudi Dar ila bado kanichunia, nimemwambia akiendelea hivyo atashangaa narudi na mzaramo mmoja aje ampe tuition kidogo.