Huyu mwanamke alikuwa anaonyesha u-wife material ila baada ya kumwambia sitafuti business partner nataka mke basi kaanza kutafuta njia ya kuondoka

Huyu mwanamke alikuwa anaonyesha u-wife material ila baada ya kumwambia sitafuti business partner nataka mke basi kaanza kutafuta njia ya kuondoka

Teslarati

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2019
Posts
2,621
Reaction score
10,466
Wanawake jifunzeni basi, hata kama mme wako nakushirikisha mara chache kwenye deals zangu za biashara usijiweke uhusika ambao sijakupa. Kuna mwanamke nimezaa nae na anakaa kwenye nyumba yangu huko mkoani, mimi nipo zangu hapa Town nimeajiriwa ofisi fulani na nimepanga ila mara kwa mara huwa natuma watu wakachukue au wapeleke hela zinazotokana na business pale nyumbani.

Shida ilianza huyu mwanamke akataka kufungua saloon nikasema 'no' sababu najua madada wa saloon wanalika sana. Baadae kelele zikawa nyingi nikaamua kumfungulia ila kwa masharti kwamba asije akachanganya pesa kutoka kwenye biashara zangu nyingine akaweka huko saloon bila kuniambia.

Sasa hesabu za mwezi wa tatu hazikuwa sawa kwenye kibanda changu kimoja cha MPesa, dogo wa pale akawa haeleweki. Ikatokea nafasi nikarudi mkoani wiki kama mbili zimepita, kumbana yule dogo ndo akasema "Shemeji alichukua hela akasema nisikwambie atarudisha ndani ya wiki moja" lakini muda umepita hadi mie nilipokuwa narudi alikuwa hajarudisha hio hela,

Shida kubwa sio kuchukua hela, shida kubwa ni kutoniweka wazi na kuvunja makubaliano yetu kwamba asichanganye hela zangu na biashara zake.

Argument na huyu mwanamke ikawa kubwa ndipo nikamwambia "Mimi nataka mke wala sio business partner", Naona kanikasirikia, nikasema unakasirika eenh, nikafunga saloon yake hapa nilipo nishamkabidhi dalali auze kila kitu ili huyu mwanamke atulie nyumbani.

Jana ndo nimeanza safari ya kurudi Dar ila bado kanichunia, nimemwambia akiendelea hivyo atashangaa narudi na mzaramo mmoja aje ampe tuition kidogo.
 
Niwe mkweli hapa wanawake wengi sana wanakuja na maslahi yao binafsi kwa mwanaume. Kama mwanaume hueleweki hakutaki na kama unaeleweka utaibiwa nae kusepa
Nina rafiki zangu watatu wamelizwa na wake zao na they never saw it coming sababu maisha walokua wanaishi ni upendo hadi unaona jamaa anakula pepo duniani, wote walifanya mistake moja ambayo ni kuwafanya wanawake zao kuwa kama business partner, hio ni mistake wanaume wenzangu.
 
Anakufyonza kama kupe 😂 aisee wanawake.....
Hawana adabu,

Mie nishajua ndo kilichomleta pale na kumtuliza ni anataka sana maslahi, nilipima watoto DNA sababu kuna mida nikawa nahofia hata watoto sio wangu sababu she's so calculative.

Baada ya kuona nmejua mchezo naona anatafuta gia tu nimtimue
 
Nina rafiki zangu watatu wamelizwa na wake zao na they never saw it coming sababu maisha walokua wanaishi ni upendo hadi unaona jamaa anakula pepo duniani, wote walifanya mistake moja ambayo ni kuwafanya wanawake zao kuwa kama business partner, hio ni mistake wanaume wenzangu.
Mwanamke ni kama sukari ana ladha tamu lakini matumizi yake yakizidi itakupa maradhi.
 
Back
Top Bottom