Huyu mwanamke kila akipata hela lazima anikumbuke hata kama ni hela ndogo, nahisi kumpenda sana

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
993
Reaction score
2,045
Kwema binaadamu wenzangu mliomo humu?

Jamani kuna huyu mwanamke naweza sema ni mchumba wangu tuna kama miaka miwili toka tumefahamiana.

Tumepitia stages tofauti tofauti, kugombana, kupotezeana, kuumizana, kuenjoy na kununiana kama ilivo kawaida mambo ya mahusiano.

Huyu mwanamke ni aina ya wanawake simple, siyo slay queen, ni mtu focused sana.

Ni mwanamke ambaye namchukulia kama rafiki yangu, ndugu yangu, hana ujinga ujinga wala ugai gai.
Huyu mchumba anaishi mjini dasalama mimi nipo mkoani.

Hana kazi ya kuajiriwa serikalini ila anaunga unga nayeye kitaa hapa na pale japo kwao siyo maisha mabovu kivile ila anapambana na mambo tofauti tofaut hapo dasalama.

Kikubwa ambacho kinanivutia sana Kwa huyu kimwana ni kwamba kila akipata kihela hata kama ni laki moja lazima aniambie na aniombe anipe kidogo hata kama ni buku teni au 15k inategemeana na anakuwa kapata shingap.

Sometimes huwa nahisi huruma sana kwasabab hana kazi ya kueleweka kabisa anabangaiza ila ananipa hicho hicho kidgo na siyo kwamba nalia njaa kwake no sina hizo njaa ndogo za kuomba mpka 10k kwake na sijawah kumuomba hela na naonaga aibu kumuomba mpenzi wangu hela siyo yeye tu ila mpenzi wangu yeyote hata huko nyuma yani naogopaga sana hata kama nina shida kiasi gani siwezi kumuomba mpenzi hela.

Ila Kwa huyu mchumba yani ni anabangaiza mtaani ila akipata ananipigia cm ananambia kapata kiasi flani anaomba anigawie kidogo namimi nahisigi kutoa machozi kabisa na nakubaligi kwasabab naona kumkatalia itakuwa vibaya.

Hivi hapa katoka kunipigia cm kuna hela kidogo kaipata anataka anitumie hela kidogo na nashindwa kumkatalia kwasabab nahisi ntamuumiza.

Ila nachofanyaga namimi nampaga vihela Kwa kustukiza akipotea online najua hana vocha natuma vocha, video call niliona kachakaa kichwani nampa hela ya saloon japo sometimes anasemaga yupo vizuri anaweza kuhandle mwenyewe.

She is such a lady ambaye najihisi kabisa naenda kuachana na hawa ma kumbahewa wa mjini nijikite kwake nimpe mapenzi yote yeye maana hakuna nachokosa kwake, anajua how to make love in the bed, she is so romantic akinimiss anakuja na haombi hata nauli ya kuja ila ni mm tu najiongezaga kumpa kwasabab naelewa majukumu ya mwanaume.

Mungu nakuomba umlinde huyu mwanamke, umpe maisha marefu, umpe kila hitaji la moyo wake, umpe ajira, umpe moyo wa upendo na umlinde na hila zote za shetani. Amen!

Kuna wanawake na huyu mwanamke wangu jamani she seems to be absolutely different from many other girls out there

I love you (**********)
 
Ngoja nikuamshe kidogo toka kwenye hilo lindi la mahaba.

Umesema anaishi Dar es Salaam na hana kazi maalum, anabangaiza tu lakini kila akipata kihela anakukumbuka.

Umeshajiuliza hayo mabangaizo yake yanatoka wapi? Maana Dar hii ya sasa, kupata laki moja ya hapa na pale bila ofisi inayoeleweka, unahitaji uwe na connection imara sana.

Sitaki kusema ana sponsor, hapana! Lakini fungua macho kidogo usije ukawa unakunywa supu ya jasho la mwanaume mwingine aliyetoka kumuhonga shemeji yetu.

But anyway, kama ni jasho lake halisi, basi huyo ni wife material aliyepitiliza kiwango.
 
Nachoamini mimi hakuja mwanamke au mwanaume wa mtu mmoja binafsi, mke wa mtu analiwa vizuri tu na mume wa mtu anachepuka sana tu. Kwahyo hoja siyo kupigwa mashine na kuhongwa na vibopa ishu ni kunikumbuka kwenye hata kidgo anachopata na siyo kwamba namuomba au nina shida na hizo hela zake ila nina express ni Kwa kiasi gani anahuruma na kujali wengine kwani kuna malaya wangapi wanalipwa mapesa mangap na hawawakumbuki wenza wao? Tuanze na huyo mpenzi wako anakukumbukaga hata kwenye hicho kipato chake ambacho pengie wewe unaona anakihangaikia kihalali?
 
Hela ya mwanamke hailiwi kizembe hata kidogo. Una kitu na unaandaliwa kutoa vitu.
Nishaishi naye muda sana na angekuwa kama wewe kumbahewa ningekuwa nishamjua na btw akiwa na shida ananambia mapema kabisa namuandalia vyake, na shida yake inakuwa inaeleweka siyo kama nyie hata 10k ya chips au bando mnaomba mabwana zenu. Kubali kataa wanawake mnatofautiana. Kwa anachonipa kitandani hata asingekuwa ananipa huto tu hela ingetosha kumhonga hata figo
 
mimi na kushauri kaza buti jifunze ustaarabu zaid ya huo ulio nao .. mtendee mema usimlipe ubaya utajiundia carma .. mjali zaid na jifunze ustaarabu zaid ya huo ulio nao nimekukibali uko vizur nachukiaga sana wanaume wanao waachaga kiholela wapenz wao. au wale wanaume ma casanova *** them wanasababisha masingo mother kila kona ujinga tu hata akili za kujitambua hayana.
 
Mbinu ya kisaikolojia inayoitwa reverse psychology unafahamu inavyofanya kazi?

Hapo hamna huruma wala nini , anachokifanya huyo mwanamke tunakiiita strategic positioning, anaelewa wanaume wengi tumezoea wanawake wa "nitumie na ya kutolea".

Kwa hiyo ameamua kucheza na saikolojia yako kwa kukutengenezea mazingira ya wewe kuwa unajihisi hatia, ndiyo maana unajikuta unamtumia hela bila yeye kuomba, na nina amini hela ambazo wewe unatoa lazima itakuwa ni kubwa kuzidi anazotoa yeye, kaweza kucheza na akili yako mpaka umeamua kumuanzishia mpaka uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…