Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

Bila kujua falsafa ya Kasanga & Kambona na wangineo waliompa.ushauri mwalimu kuhusu namna ya kuijenga Tanganyika mpya; basi hata wewe utasema jamaa walikuwa ni wahaini tu sababu hujui content za maudhui yao.

Jiulize toka 1961 hadi 1985 je taifa limesogea juu ya wale maadui watatu ( Ujinga, Maradhi na Umaskini)? Je toka 1985 hadi 2018 taifa limesogea kuwamaliza maadui hawa? Kushangilia ununuzi wa ndege moja kama sikukuu ya kitaifa; is that you call it nation achievement.
 

Fuso,
Napenda niseme machache kuhusu Kassanga Tumbo.

Mwaka wa 1955 babu yangu Salum Abdalah alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Tanganyika Railway African Union (TRAU) na Kassanga Tumbo akiwa Katibu.

TRAU si kwa bahati mbaya kuwa ilifuatana na TANU katika kuuundwa kwani huyu
Mwenyekiti wake alikuwa na historia ndefu ya siasa kuanzia African Association.

TRAU na TANU ilipigana bega kwa bega dhidi ya ukoloni wa Muingereza na kwa
hali hii Salum Abdallah na Kassanga Tumbo walikuwa pamoja.

Mwaka wa 1960 Salum Abdallah na Kassanga Tumbo waliongoza mgomo wa
wafanyakazi wa reli uliodumu kwa siku 82.

Mgomo huu ulisimamisha kila shughuli za reli kuanzia gari moshi, mabasi na meli.
Mgomo ulifanikiwa sana na mwishowe serikali ya kikoloni ilikubali madai yote ya
TRAU.

Baada ya uhuru mwaka wa 1961 Mwalimu Nyerere alimteua Kassanga Tumbo kuwa
Balozi wa Tanganyika Uingereza.

Kassanga Tumbo hakukaa Uingereza akajiuzulu ubalozi akarejea Tanganyika na kuunda
chama cha siasa, Tanganyika Democratic Party, (TDP).

Mwaka wa 1958 kutokana na Uchaguzi wa Kura Tatu baadhi ya wanachama wa TANU
wakajitenga na kuanzisha chama cha Kiislam, All Muslim National Union of Tanganyika,
(AMNUT).

Waislam walikikataa chama hiki kwa iyo hakikupata nguvu.

Wakati Kassanga Tumbo anarudi Tanganyika kutoka Uingereza baada ya kujiuzulu
ubalozi, Kassanga Tumbo aliingia mazungumzo ya kuunganisha chama chake TDP
na AMNUT.

Hii ilikuwa mwaka wa 1963.

Mwaka 1964 askari wa Tanganyika Rifles waliasi na na baada ya Waingereza kumaliza
uasi ule ikapita kamata kamata na Salum Abdallah na Kassanga Tumbo walikamatwa
na kuwekwa kizuizini pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Huu ukawa ndiyo mwisho wa TRAU na vyama vingine vya wafanyakazi ikaundwa NUTA.
Yako mengi lakini kwa sasa naomba kusimama hapa.
 
Ni kama unataka kuunganisha maasi ya mwaka 1964 na Simba wetu Sikonge Kasanga Tumbo.

Wakati wa uhai wake hakuwahi kugusia kabisa kwamba alitaka kuangusha Serikali ya Mchonga?

Nilikiwa mdogo sana by the time; na tatizo kubwa historia haipo na ukweli haujulikani kabisa kwa nini Kasanga alikuwa grounded?

Nitalifanyia kazi ingawa ni kazi kubwa kwangu sababu hakuna historia imeandikwa.
Mchango wako naufanyia kazi. Asante sana.
 
Mi naona haya ndiyo matunda ya taifa letu tunayovuna sasa; kuna watu walipigania demokrasia ya taifa hili tangu enzi zile lakini hakuna hata mmoja ambaye kaandikwa kwenye historia ya nchi yetu na wote walionekana ni waasi watupu.

Kuna hisroria ya taifa hili lnakosekana; hakuna balancing kwenye real story of nation struggle towards our independence; kuna vitu vilifanyika ila havikuandikwa kwa sababu maalum hili ni tatizo kubwa; walificha nini? Kwa manufaa ya nani?
Inabidi tuutafute ukweli na uandikwe kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
 
Fuso,
Hapakuwa na uhusiano wowote kati ya maasi yale ya 1964 ya Tanganyika Rifles
na viongozi wa wafanyakazi kwani kesi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi
hawakushitakiwa.

Kesi yote ile iliwahusu akina Elisha Kavana na Ingo Ilogi.

Jambo hili la kusingiziwa lilimuudhi sana babu yangu kiasi alipotoka kizuizini
akajiweka mbali sana na TANU hadi alipofariki mwaka wa 1974.
Mohamed Said: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
Mohamed Said: SIKU BABU YANGU SALUM ABDALLAH ALIPOMKABILI FREDERICK MCHAURU KATIKA MGOMO WA WAFANYAKAZI WA TANGANYIKA RAILWAYS TABORA 1947
 
Mkuu kadoda11 nime mmention Mohamed Said aje huku ajionee mwenyewe asifungwe na siasa za Gerezani na kutulazimisha ni siasa za Tanganyika.

Ngongo,
Inawezekana hujaona mchango wangu humu.
Kwa nini mimi nikulazimishe wewe kuhusu historia ya wazee wangu?

Nikulazimshe kwa kisa gani na ndiyo iwe nini?
Historia ya Gerezani katika uhuru wa Tanganyika ni ya pekee sana.

Mimi simlazimishi mtu yeyote wao wenyewe wanaposikia niko uwanjani
wanafika kwa khiyari zao kwani wanajua kuna kitu cha maana watajifunza.

Kama hivi wewe ulivyonkaribisha mimi hapa kwenye jamvi.
Je, kuna mtu kakulazimisha kuniita?

Umeniita kwa kuwa ndani ya nafsi yako unajua kuwa mimi najua.

Na hakika Alhamdulilah naijua historia ya wazee wangu na wengi wamethibitisha
hili.

Uzi huu nimeuona na nimeeleza niyajuayo kuhusu Kassanga Tumbo.

Kassanga Tumbo ana nafasi ya pekee kwangu kwani yeye na babu yangu Salum
Abdallah
ndiyo walikuwa waasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU)
mwaka wa 1955.

Pekua utaona mchango wangu.
Hii ni ziada kwako kukuthibitishia kuwa hii historia iko ndani kwetu.

Mtaa wa Kanoni Tabora Isevya mwisho wa mtaa unaelekea Kachoma katika miaka
ya mwanzoni 1960 kulikuwa na nyumba mbili nzuri sana zinatazamana.

Nyumba hizi zilikuwa moja ya babu yangu na nyingine ya Kassanga Tumbo.

Kadoda,
Katika lugha ya Kiswahii kudoda ni kuharibika.
Mathalan unga ukiingia maji na hauwezi kusongwa ugali tunasema ''umedoda,''

Unasema natokwa na ''povu.''
Povu linitoke mdomoni kwa kisa gani?

Hapa katika mchango wangu kuhusu Kassanga Tumbo nimeeleza pamoja
na historia ya babu yangu Salum Abdallah.

Je, lipo povu?
Naetokwa ni mishipa ya shingo si mimi.

Mtafute na jiangalie wewe binafsi.
Mohamed Said: GEREZANI NA HARAKATI ZA UHURU WA TANGANYIKA SIASA KATIKA MJI WA DAR ES SALAAM MIAKA YA 1950
 
heee!!! kumbe alikua anatumika Kwa maslahi ya watu Fulani?! tuachane na hayo nyerere alikua kiongozi mwenye akili sana si jambo dogo kutupatia Uhuru kutoka kwa watu waliokuahawapo tayari kuachia dhahabu,almasi,shaba,ndovu,na mengine mengiiii haikua kazi rahisi aisee...
 
Yaani kwenye majadiliano tu ya vyama vingi vita ikatokea !!! Nyerere bado alikua sahihi kuvifuta muda ulikua bado na hatukua tayari tumejiandaa na vyama vingi...sipingi ila najaribu kuangalia alichokiona Mwl nyerere by then kwenye upande Wa pili Wa shillingi je tulijiandaa wakati huo?!
 
Ikowa,
Ngongo
na Kadoda walioitana katika huu mjadala siwaoni tena.
Nini kimewasibu?

Au wanaupita uzi huu wima wima bila kusimama?
Au walidhani Tabora ni mbali sana siwezi kufika?
Au wameingia hofu mtego umenasa chui?

Ikowa,
TANU ilikuwa na nguvu sana hakuna chama cha upinzani kilichokuwa
na uwezo wa kupambananacho.

Tanganyika ilkawa nchi ya chama kimoja, ''de facto.''

Ukitaka kujua vipi TANU ilikuwa na nguvu kiasi kile isome historia ya
kweli ya TANU na waangalie waasisi wake ambao kwa bahati mbaya
leo wamesahaulika na angalia kujitolea kwao katika kupinga ukoloni.

Hapa ndipo utalipata jibu.

Chukua mfano mmoja tu wa Rashid Ali Meli nini alifanya mwaka wa
1955 kuhakikisha kuwa safari ya Mwalimu Nyerere UNO inafanikiwa
kwa muda ambao TANU ilipanga.
Mohamed Said: KUTOKA JF: ALI MWINYI TAMBWE, RASHID ALI MELI NA IDD FAIZ MAFUNGO - SAFARI YA NYERERE UNO 1955
 
 
Kama vile amenikumbusha enzi za campaign ya kudai Uhuru WA Tanganyika miaka ya 1950 hadi 1960,Historia ya Kasanga Tumbo na akina Chief Fundikila WA pale Itetemya Kipalapala iko wazi,MWL.Nyerere hakutaka malumbano ya vyama Bali waungane kupambana ukoloni,mkutano WA Tabora WA Tanu,wimbo unaosema Ehe Sasi jabela mitwe haaa ! Oho Tanu yajenga nchi Tanu haa nakumbuka sana na slogan ya Uhuru na Kazi ya Tanu na Nyerere WA kanda ya ziwa,wapi James Mapalala ?
 
Mtu kama Mtei angeweza sana kueleza yaliyompata lakini, naona hana ubavu wa kujieleza. Ninachokumbuka alipofukuzwa serikalini na JKN kwa maelewano yake na IMF miaka ya 80, nchi iliandamana kulaani tabia yake. Mtei alilaaniwa nchi nzima. Ni ajabu hata ktk kitabu chenye autobiography yake cha "From Goatherd to Governor" Mtei hasemi undani wa kukosana na serikali au JKN. Alistahili aeleze undani ili pia tufahamu tabia za JKN zilizojificha kwa wananchi.
 
Oh!
 
Vyama via wafanyakazi vilitoa mchango mkubwa sana katika harakati za kugombea uhuru wa Tanganyika. Kuna viongozi wake ambao wamesahaulika kabasa katika historia ya nchi hii mmoja wao ni Michael Marshall Mowbry Kamaliza!!
 
Hakika ni wanasiasa wachache sana wanaoweza kuvaa viatu vya Hon Kasanga Tumbo. Wanasiasa wa siku hizi ni wachumia tumbo zaidi ya wawakilishi wa wananchi. Nchi hii imebahatika kuwa na viongozi wachache sana aina ya Kasanga Tumbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…