Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

Juzi nilipita pale alipopumzika Simba wa Tabora...jamani ni huzuni kubwa....hebu JF hata sisi tumjengee na tumhigadhi hiyu Nguri na muasisi wa siasa za Upinzani miaka kablanya TANU. ..

Mtu aliyekuwa na vision kubwa kitaifa; Taifa halimkimbuki hata sisi JF? Nipo tayari kushirikiana nanyi kwa hili.
 
Fuso,
Naomba nami nikueleze machache kuhusu Christopher Kassanga Tumbo.

Mtaa wa Kanoni Isevya, Tabora mwanzo wa mtaa kwa mkono wa kushoto kama unaelekea Kachoma, kuna nyumba ya babu yangu Salum Abdallah maarufu kwa jina la Baba Popo.

Huyu Popo ni mwanae wa kwanza ambae kwangu mimi ni baba yangu mkubwa.

Jina lake hasa ni Humud lakini hili halikushika alijulikana kwa jina la Popo hadi mwisho wa maisha yake.

Jina lake kamili lilitakiwa liwe Mwekapopo jina la babu yake aliyeingia Tanganyika kutoka Belgian Congo kama askari katika jeshi la Wajerumani miaka ya mwisho 1880 lakini kwa ufupisho akawa wanamwita Popo.

Hapo mwanzo wa mtaa mkono wa kushoto ndipo ilipokuwa nyumba ya babu yangu Salum Abdallah Mwekapopo Samitungo Muyukwa.

Yote haya majina ya Kimanyema.

Nyumba ya babu yangu ilikuwa maarufu kwa kuwa katika miaka ile ya 1950 wakati harakati za kudai uhuru zimepamba moto yeye alikuwa mstari wa mbele dhidi ya Waingereza kwanza akiwa katika TAA, TANU na TRAU.

Mwisho wa mtaa wa Kanoni kabla hujafika Kachoma ilikuwapo nyumba nyingine ya babu yangu na mkabala wa nyumba hii ilikuwapo nyumba ya Christopher Kassanga Tumbo na zote mbili ni nyumba kwa wakati ule zilizokuwa nzuri mtaa mzima.

hii Kachoma ni sehemu maarufu kwa kuwa kulikuwa na kilabu cha pombe za kienyeji.

Mwaka wa 1955 mara tu baada ya kuundwa kwa TANU babu yangu na Kassanga Tumbo waliasisi chama cha wafanyakazi wa reli Tanganyika, kikijulikana kama Tanganyika Railway African Union (TRAU) babu yangu akiwa Rais na Kassanga Tumbo Katibu.

Wakati wa likizo mwaka wa 1964 nikiwa darasa la sita nililifika Tabora kumtembelea babu yangu lakini hakuwapo nyumbani na kwa akili za kitoto hili halikunishughulisha na baada ya likizo kwisha nikarudi Dar es Salaam bila ya kumuona.

Lakini kilichotokea kwa babu yangu kutokuwa nyumbani ni kuwa alikuwa amewekwa kizuizini jela ya Uyui kufuatia maasi ya wanajeshi tarehe 20 Januari,1964 na baada ya Jeshi la Kiingereza kumaliza maasi yale, serikali iliwakamata viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi na kuwaweka kizuizini.

Kassanga Tumbo alipata taarifa za msako wa viongozi wa vyama vya wafanyakazi mapema na akawahi kutoroka akaenda Mombasa lakini alikamatwa baadae na akarejeshwa Tanzania na kuwekwa kizuizini.

Babu yangu pia alitoweka akawa haonekani mjini na makachero wakawa wanamsaka bila mafaniko hadi alipojitokeza mwenyewe kituo cha polisi na hapo ndipo alipokamatwa.

TRAU wakati wa uhai wake TANU ilipokuwa inapigania uhuru wa Tanganyika chama hiki kilikuwa na nguvu kubwa kwani viongozi hawa wawili waliunganisha nguvu ya TRAU na TANU kupambana na Waingereza na hili lilitoa uwanja mpana sana kwa TRAU kufanya siasa za mapambano.

Mwaka wa 1960 TRAU ilifanya mgomo uliodumu siku 82 mgomo huu ulivunja rekodi ya mgomo wa Kenya chini ya kiongozi Makhan Singh wa siku 62 ambao kabla ya huu mgomo wa TRAU ndiyo uliochukua muda mrefu zaidi kumalizika.

Inasemekana ilikuwa mgomo huu ndiyo uliomtia Mwalimu Nyerere hofu kwani kwa miezi mitatu wafanyakazi wa reli waligoma na kufanya treni, meli na mabasi yasimame.

Ikamdhihirikia Nyerere kuwa hawa ndiyo viongozi wa wafanyakazi ambao atakuja kukabiliananao katika Tanganyika huru.

Hii ndiyo ikawa sababu ya yeye kuwakamata viongozi wa vyama huru vya wafanyakazi baada ya maasi na kuwaweka kizuizini na kuunda NUTA chama kipya cha wafanyakazi na kukiweka chini ya TANU.

Wakati Kassanga Tumbo anaondoka kwenda Uingereza kuchukua nafasi yake kama Balozi alikwenda kumuaga babu yangu na alimwambia kuwa Nyerere kaamua kumpeleka Uingereza kuwa balozi ili apunguze nguvu ya TRAU.

Yapo mengi sana ambayo Kassanga Tumbo na babu yangu walifanya pamoja na kushauriana.

Katika picha kulia ni Christopher Kassanga Tumbo na pembeni yake aliyevaa mgolole ni babu yangu Salum Abdallah.

Unaweza kumsoma zaidi Salum Abdallah hapo chini:
 

Attachments

  • SALUM ABDALLAH NA KASSANGA TUMBO.jpg
    76.8 KB · Views: 20
Asante sana chief; ndiyo tunasema harakati za kudai Uhuru wetu kuna baadhi ya mambo yamenyofolewa!! Ni lazima tuhakikishe tunayadai yarejeshwe kabla hatujatoka hapa duniani.
 
Nakumbuka nikiwa mdogo Mwalimu alituma wapambe wake kijijini na 109 Landrover kumpa tena KasangaTumbo shirika la Reli; Kasanga aligoma kabisa akasema Shirika umeliua wewe mimi leo unanipa maiti nikaizike...

Haya aliyasema mara kwa mara kwenye misiba ambapo ndipo ilikiwa room yake kuyasema; nikiwa mdogo sana tuliona kwamba kachanganyikiwa baadaye sana nikajua kumbe the guy was bright and intelligent .

Si kila kitu unachoambiwa na kiongizi wako kinakuwa sawa; hapana. Kiongozi bora ni lazima awe na focus & vision yake.

Viongozi wa sasa ni wa ndiyo Mzee...hapa ndipo tunapoiua Tanzania yetu kifo cha wima.
 
Tunashukurubkuona kuwa bado wapo watanzania wanapata nafasi ya kufahamu ukweli juu ya historia ya taifa letu. Napenda pia kuwahimiza waandishi na wanahistoria mbalimbali kuandika upya historia ya nchi yetu ingali mapema kwani bado vyanzo vya taarifa vinapatikana kabla hatujasahau tulipotoka kabisa.
 
Ahsante kwa histori kama hiz.
 
Ahsante kwa histori kama hiz.
London 1,
Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ina mengi ya kusisimua.

Mimi nilijukuta kama vile niliyeingia dunia nyingine ambayo sikuwa hapa kabla najua kuwa ipo.

Fikiria nilikuwa hali gani siku Ahmed Rashad Ali ananifahamisha kuwa 1950 mashindano ya Kombe la Gossage yalikuwa yanafanyika Nairobi.

Haya yalikuwa mashindano ya mpira ya nchi nne za Afrika ya Mashariki yakifanyika kila mwaka.

Ahmed Rashad alikuwa nahodha wa timu ya Zanzibar.

Ananambia Abdul Sykes kaja Nairobi na akamweleza kuwa kaja kukutana na Jomo Kenyatta na viongozi wenzake wa Kenya African Union (KAU).

Abdul alikuwa ndiye katibu wa TAA baada ya mapinduzi yaliyowatoa madarakani Thomas Plantan President na Clement Mtamila Katibu.

Ahmed Rashad kwa jicho lake ananambia nimemsindikiza Abdul na nimemuona Kenyatta katoka nje ya nyumba ambayo walikuwa wanakutania na kamwita Abdul kwa jina kumkaribisha ndani.

Ahmed Rashad ananieleza yeye alibaki nje kusubiri akiwa na walinzi.

Baada ya zaidi ya miaka 30 rafiki zangu Uingereza wananiletea Tanganyika Intelliegence Summary taarifa za siri za kikachero za Waingereza wakithibitisha mkutano huu wa Abdul Sykes na Jomo Kenyatta, Peter Mbiu Koinange, Bildad Kaggia na timu nzima iliyokuja kujulikana kama Kapenguria Six.

Abdul alikuwa kijana mdogo wa miaka 26.
 

Attachments

  • KAPENGURIA SIX.jpg
    38.4 KB · Views: 18
Huyu atakuwa yule jamaa wa MAKETE mwenye degree saba
 
Nyerere asingewafanyia hayo waliompa changamoto madaraka yake yangekumbwa na misukosuko sana
 
RIP Kasanga Tumbo rafiki yangu pia
 
Daaa kweli
 
Historia adimu sana kwenye Uzi huu. Nilisoma kwenye kitabu cha Sir Andy Chande, A Knight in Africa, anaeleza kuwa mgogoro wa Africanization uliwafanya Nyerere na Tumbo kugombana.

Afrikanization ilikuwa ni vuguvugu lilokuwa ndani ya TANU ambalo lilipigania kuona watanganyika 'weusi'-wakidaiwa ndio watanganyika halisi-pekee ndio wanashika nafasi zote za utawala nchini. Nyerere alipinga sera hii akiamini utanganyika sio rangi bali uzalendo. Nyerere aliacha uwaziri mkuu na kumkabidhi Kawawa, yeye akazunguka nchi nzima akihubiri dhidi ya afrikanaizesheni. Sasa vyama vya wafanyakazi mfano cha mkonge cha Kassanga Tumbo kilikuwa mstari wa mbele juu ya afrikanaizesheni. Hii ikamlazimu Nyerere kuja na sheria iliyoipa mamlaka serikali kuweka mtu kizuizini pasi na kupelekwa mahakamani (Preventive Detention Act). Tumbo alikumbwa na gharika hili. Na ndio sababu vyama na jumuiya za kijamii kuwa 'chini' ya serikali.
 
Huyu mzee alipotoka kizuizini, alikuwa anaishi maeneo ya Ubungo kwa mdogo wake. Alikuwa akisikia watu wanaongea siasa tu alikuwa anatoka nduki. Hivi walimfanya nini?
Anaona mnamletea nyoka amgonge kwa Mara ya pili tena tena kinga za mwili zimeshachoka hazihimili sumu ya nyoka huyo
 
Karanga Tumbo alianza siasa alisoma shule ya Tabora boys secondary school na alimaliza katika miaka ya katikati ya 50 akiwa na Edwin Mtei alianza siasa tangu akiwa shule Tabora school kwa kukataa kuitwa Christopher Samuel Tumbo na kujiita Kasanga Tumbo (jina lake la kiafrika) ilipelekea kuta kufukuzwa shule lakini alifanikiwa kumalizia shule na kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Makerere huko uganda lakini hakwenda na aliamua kuanza kazi katika shirika la Railways co.na hapa ndipo alipoanza Siasa baada ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi cha Railways na mwaka 58 (akiwa na umri wa miaka 24) alianzisha mgomo uliodumu kwa siku tisini (huu ndio ulikuwa mgomo wa mwisho wa kupinga ukandamizaji wa wazungu ambao uliwaogopesha wazungu na kupelekea kuachia nchi) baada ya uhuru akiwa na miaka 26 aliteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Uingereza baada ya muda aliacha ubalozi na kurudi Tanzania na alianzisha chama cha siasa PDP ambacho kilikubarika sana nadhani ndio kilicho mletea shida mpaka ukapelekwa kukimbia nchi na kupata hifadhi nchini Somalia na baadaye Kenya huko ndiko alipokamatwa na kurejeshwa Tanzania na alishtakiwa kwa kesi ya uhaini akaukumiwa kunyongwa kwa bahati nzuri inashindikana (haikuwa kunyongwa mpaka kufa) ivyo akafungwa miaka 27 (miaka3 jela) . Mwaka 92 wakaanzisha kamati ya kushinikiza katiba (NCCR) yeye akiwa masterplan baadae akataka kiwe chama wengine wakaogopa yeye na Chief s Fundikira wakaanzisha UMD ndicho chama cha kwanza cha upinzani lakini kikasambaratika bàada ya hapo akajiunga na vyama mbalimbali na atimaye Chadema likiwa bado akatembee nchi nzima na aliweka matawi nchi nzima lakini aliona baada ya kufanyiwa figisu figisu zilizo mfanya aende CUF napo pia alifungua matawi mengi sana na alipata umaarufu sana ( washabiki walimwita Mandela) napo figisu zimuondoa ndio akajiunga na CCM lakini hakudumu na alifariki dunia
 
Paundi 60,000 ili kuweza kumpindua Mwalimu Nyerere, nahisi hapa ndipo alipochemsha na kujikuta hawezi kukwepa mkono wa dola.
Je zilibainishwa sababu ni nini hasa za kulipwa ili ampindue Mwalimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…