Huyu ndiye Giriki, Dereva aliyetoka na basi Dar saa 12 asubuhi, akaingia Mbeya saa saba mchana

Kuna chuma kiliitwa turbo express songea-mbeya ndio lilikuwa basi la kwanza(sina uhakika)ila lilikuwa na carrier juu haya ma tawaqal aliendesha baadaye.
Ila jamaa hazeeki, maana Turbo Express, Movement Star, Amina Express (Aluta Continua), Kwacha, Kamata, Nyota ni basi za miaka mingi sana, Giriki alikuwepo
 
Nazungumzia miaka hiyo mkuu sio siku hizi.
 

wamva nisaidie nani alikua anaendesha mabasi ya Ilangamoto kabla hayajafungiwa miaka ya 97-98?
 
Nakumbuka 2015 nikiwa natoka likizo MUST tulikodi Happy nation ikatufata chuo.. Aisee tuliingia Moro saa 8... Tukapigwa mkono na kuruhusiwa saa 10... Ajabu bado ikawa ndo gari ya 1 kuingia ubungo kutokea MBEYA... Sijawahi panda gari ikiwa speed zaidi ya ile...
 

Mwaka gani maana hii story ni kama ya kijiweni? Kama 12 jioni ni sawa ila sio ya sa sita
 

Saa moja sawa , mdau alivyoweka 12:45 imekaa kama alifika saa 6 kujiuliza singida alipita saa ngapi. Ally’s sport saa 2 kuingia dar ilikua kawaida
 
Ila sasa hivi tunaonewa sana. Dodoma - iringa masaa matano kwa basi? Sio poa kabisa. Dodoma mbeya masaa 10 na zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…