Polisi hawawezi kujitenga na raia halafu wakashinda vita km hii.
Kuna kitu kinaitwa "THEORY OF STAKEHOLDERS IDENTIFICATION AND SALIENCE"
Hapa vitu vitayu POWER,LEGITIMACY NA URGENCY.
Kuminywa kwa haki za raia ndio chanzo cha raia kuanza kutumia nguvu "POWER" kushinikiza wasikilizwe au mambo yao yatekezwe au haki zao wazipate. Hapa utawala utashurutishwa kutekeleza wanachokitaka na hapa ile dhana ya "KUTII BILA SHURUTI" haina maana tena kwani shuruti ndio imeshika hatamu.
Labda niwakumbushe juu ya Yusuf Mohamed aliyekuwa kiongozi wa Boko Haram alikuwa akishinikiza maendeleo katika jimbo la Maiduguri lililosahaulika kimaendeleo ya kila namna na kukomeshwa kwa ukandamizi uliofanywa na dola kwa watu wa jamii hiyo,huyu mtu alikamatwa na kuuawa mikononi mwa polisi akiwa na pingu mikononi. Aboukar Shakau akachukua hata na kuanza kushinikiza kwa nguvu "POWER" akiwa na "STAKEHOLDERS" wengine. Nadhani mnajua kinachoendelea.
Hapa kwetu tumelia sana juu ya ukandamizaji wa haki za raia na sasa nguvu inatumika (MUNGU ATUEPUSHE).
LEGITIMACY(POLISI) na URGENCY(VIONGOZI WA SERIKALI) nadhani watakuwa wahanga wa hili suala.
Serikali itumie busara kubwa kutatua hili suala na lazima irudi kwa wananchi maana bila hivyo watabaki kuwa wahanga na wananchi wanawaona polisi na viongozi wa serikali km maadui.
SERIKALI NDIO WACHOCHEZI WA HILI SUALA