Ninachokitarajia ni kuona matunda ya bidii zangu ktk kaz ctoweza kupambana milele kuna muda itafikia mwili na akili yangu vitashindwa kufany kaz tena ndipo ndo nianze kumlilia mungu aninyooshee mamb yangu muda huo nitakuwa nimeshajichokea mwili hauwez tena sabab co mashine.
Kwani wakat unaanza ulimshirikisha Mungu, au ulikuwa unasubiri mkamo ndio utoe lawama kwa Mungu?
Ayubu 22:21
[21]Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.
Tembea katika njia ya Mungu pamoja na bidii yako
Zaburi 1:1-3
[1]Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
[2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
[3]Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.
Hizo nguvu tu za kupambana miaka mitano zimetoka kwa Mungu
Kumbukumbu la Torati 8:17-18
[17]Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
[18]Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Soma neno la Mungu na lisitoke kinywani mwako ndio ustawi wako.
Yoshua 1:8
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.