Huyu ni Mungu wa aina gani anaacha niteseke kiasi hiki?

hakuna ajuaye ila muhimu ni kuamini kuwa yupo ili tukifa tuwe na chakueleza huko tutapoenda.
 
Ubarikiwe mkuu
 
Mungu huwa hapendi kulaumiwa, ila anapenda kulalamikiwa. Mlalamikie kumuonyesha kuwa njia yako ni YEYE na bila yeye huwezi kutoka hapo ulipo. Usiendelee kumlaumu kwa sababu kwa kufanya hivyo, ATAKUPIGA muda siyo mrefu. Ni uhakika na siyo utani
huo ni upotovu wa kifikra mkuu hakuna atakayepona kati yetu
 
Mungu mvaa pajama. Endelea kupambana achana na mungu mzungu.
 
Haoo umesema umefanya KAZI miaka mitano bila kutetereka, wakat kuna wenzako walifanya miezi miwili walitetereka, Bado unamkufuru Mungu TU??
 
Haoo umesema umefanya KAZI miaka mitano bila kutetereka, wakat kuna wenzako walifanya miezi miwili walitetereka, Bado unamkufuru Mungu TU??
Ninachokitarajia ni kuona matunda ya bidii zangu ktk kaz ctoweza kupambana milele kuna muda itafikia mwili na akili yangu vitashindwa kufany kaz tena ndipo ndo nianze kumlilia mungu aninyooshee mamb yangu muda huo nitakuwa nimeshajichokea mwili hauwez tena sabab co mashine.
 
Sasa matatizo yako unataka ayasolve huyo Mungu ambaye hata wew humjui?[emoji28][emoji28].

Ndio matatizo mlipokubali Miungu migeni mnayoiabudu na kuiomba huku hamjui mnachokiomba wala hamjui kutarget shida zenu kwa huyo mnaemuomba.

Utasota sana kupeleka shida kwa kiumbe usichokijua.

Hakuna muujiza kwenye kuomba Mungu usiyemjua.

Maombi yangekuwa yanafanya kazi, basi mahospital yasingekuwepo maana wagonjwa wote wangepona kwa miujiza.

Umasikini usingekuwepo maana walokole wanaomba kila siku.

Njaa&taabu zisingekuwepo sabbu ya maombi.

Sometimes unaweza kuzani Shetan ana nguvu kulko hayo Mamiungu yenu mnayoyaabudu makanisan na misikitin, maana shetan huwapa wamfuatao mahitaji yao by100% bila kinyongo na kupoteza muda, lkn hao Miungu wasiojulikana wao kutwa kutaka misifa ya kipumbavu na kuwabembeleza as if unachumbia ukweni, That is Nonsense.

Washirikina ndio watu Pekee wanaojua kutarget maombi yao na kupata wakitakacho, maana wanamjua wanaemuabudu, na wanakijua nini wanakitaka na nini huyo wamuabuduye anakitaka, .

Sas wew na wana dini wenzako, changanyikeni mujiulize je Huyo Mungu wenu Mnamjua? Je anataka nini? kwa muda gani? Sio tu mnafuata mkumbo wa kujiombesha kama wale wapumbavu wanaopiga makelele asubuhi& usiku kwa kuomba maombi yasiyojibika.


Ukimjua unayemuomba, kamwe hutolalamika wala hutopata shida.

Endelea kujuta maana mpaka hapo inaonesha bado hujajua Nini unakitafta
View attachment 2121574
View attachment 2121577
 
Yakobo 4:3
Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
 
Kwani wakat unaanza ulimshirikisha Mungu, au ulikuwa unasubiri mkamo ndio utoe lawama kwa Mungu?

Ayubu 22:21
[21]Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.

Tembea katika njia ya Mungu pamoja na bidii yako
Zaburi 1:1-3
[1]Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

[2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

[3]Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.

Hizo nguvu tu za kupambana miaka mitano zimetoka kwa Mungu
Kumbukumbu la Torati 8:17-18
[17]Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.

[18]Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Soma neno la Mungu na lisitoke kinywani mwako ndio ustawi wako.
Yoshua 1:8
[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…