Huyu PCK ni nani? Ana Bil. 57 benki, TRA wamezuia akaunti yake

Huyu PCK ni nani? Ana Bil. 57 benki, TRA wamezuia akaunti yake

Pesa ndogo Sana hio am 32yrs na Nina 1B kasoro ..na sijulikani na mtu yoyote natembelea tu ka vanguard ..show room ya magari ziko mbili mikoa miwili tofauti
Kwa hiyo kumbe ili kupata pesa nyingi inatakiwa kuwa na showroom za magari? Naona mnazitaja sana..
 
Ila huu mkeka wa huyu jamaa umenifanya nijisikie hopeless sana.., mtafanya watu tuanze kuuza madawa ya kulevya jamani, hii mikeka yenu msiwe mnaiweka hadharani bhana, mi najionaga nina pesa, kumbe hamna kitu kabisa aisee ,daaah, mnatupa msongo wa mawazo
 
Watu hatusomagi yale maelezo nyuma ya account opening form. Nakumbuka kuna mzungu mmoja nilikuaga namfungulia account akaomba aondoke na forms kwanza. Kesho yake akaja ame underline baadhi ya vipengele anataka ufafanuzi. Nikamuelezea ila vingine vikawa vigumu nikaipangua nikampeleka kwa boss wangu maana mi pia nilikua sijawahi kusoma nilijibu kwa experience tu
Alifungua?
 
Aisee usiwaine tu watu Instagram ukawachukulia poa, jamaa huyu huwa anatoka sana na wadada wa Bongo movie, na picha yake akila romance na Wema ilivuja na kumpa umaarufu mkubwa.

Huyu jamaa PCK amekuwa na urafiki na Mastaa wengi na ni mfanyabiashara , ana miliki maduka ya simu, hotel, show room etc.

Kilichonishangaza Leo, ameandika Instagram kuomba msaada Kwa mama Samia, wamezuia bilioni 57 zake zolizondani ya kcb bank, nimejiuliza kiasi kikubwa namna hii Cha pesa kapata wapi.

Pia anadai makonda alimuua masogange Kwa ajili ya bilioni 12, pia anadai makonda alimzurumu range Rover lake . Sasa kama huyu mtu wa kawaida tu ana mihela yote haya, dah hii nchi, kazipataje bilioni 57?

Kumbe ndomana bongo movie wanampenda.
View attachment 2463384View attachment 2463385View attachment 2463386
duuh kama si yeye mwenye hzo b57 watu wana mawe
 
Watu wana BTC 10 na nimadogo wengine casino,youtube,wengine insta,wengine prize pools,watu wana mabillioni wanaishi kawaida huku nchi ambayo inawaza umasikini,wivu,njaa kibao milioni 30 tu eti umetoa wapi ,kwani yako inakuhusu nini,kwani wapi imeandikwa kiwango cha mwisho cha kumiliki hela?
Hujui unachoongea.. Soma about money laundering and effect zake.

Kama hizo fedha ndizo zinafadhili M23 na Magaidi wengine utajuaje?? Unafikiri hao jamaa wanakaa msituni wanakulaje, wanaishije, wanapata wapi silaha?? Huyo jamaa within 15 days amefanya transaction ya zaidi ya 50b unataka asihojiwe??
 
..huyu angekua kenya wangeshamkamata..hii bank statement inaonyesha typical money laundering....yani hela zinazoingia ni nyingi kuliko zinazotoka...na biashara zake wala haziendamni na hela inayoingia..nadhani tz kuna watu wengi mno wanafanya money laundeirng bila kufatiliwa....kiboko yao alikua jpm....sasa wakati wa mama naona wamefungulia mbwa wanapitisha hela haramu mno kwenye ma accounts huko....yaani TRA wanabiri waongeze nguvu kwenye hili....
 
Huamini ninaweza kuwa na 847m 🏦 bank

Hivi show room Kuna crown za 2012 na 2014 ngapi na alphard ngapi na canter ngap , horse mbili za scania 124 na magari mengine ..show room ingine Kuna LX cruiser na cruiser 76 series Ni Bei gani hizo Kama unafahamu mixer magari mengine madogo dogo Ni pesa ngapi hizo hadi bank ushindwe kwa na 800m plus

Haya Bado wenye ma bus hao kina abood nk bus moja Ni sh ngapi na analeta ngapi .. imagine 430m+ na zinakuja bus 16 ..equal to 6.8bil unahisi bank anabaki na sh ngapi hapo unahisi anaweza toa 7b abaki na 1B bank?

Nafikiri hamuelewani mwenzako anazungumzia 25ML USD Wwe unazungumzia 847Ml TSH.

HIZO NI PESA MBILI TOFAUTI KABISA!! 25ML USD Ni hela ndefu haswa!!

Kama unayo 847 ml USD ni sawa na mtu anazungumzia katibia 2 trilllion Tsh
 
Jamaa ana bil 57 bank ila Kuna wale washamba million 100 tu utasikia kwetu matajiri..mara walishe mbwa burger mara hivi ushamba mzigo .

Watu wa Pwani haswa zanzibar Wana madili ya hatar wanapiga pesa ila hata kujionyesha ni ngumu sana ...wengi ni dili haramu kama kawaida wanauza mpaka unga ila ngumu sana kuwajua kama wana pesa.
Nlishangaa ilitoka list humu matajiri wa Tz mzee hayupo. Dah manake ilibdi nichek walahi
 
Hao wanatakatishaa pesa za officials wa serikal hao wala wasikutishe... Et ana show room.. bla bla. Hiv bil57 mchezo.. huyo anatakatisha pesa za viongoz wa burundi huyo kama sio uganda
Labda mkuu
 
Back
Top Bottom