Huyu Polisi wa zamani Marehemu Mkama Sharp alikuwa na Kipaji gani ambacho Polisi wengi wa sasa hawana?


Huyu ndio alikuwa askari wa "Serve and Protect" sio hawa wa sasa wa "Maim and Kill", askari ambao hata kuwakamata walevi wa gongo wanahitaji msaada wa mabomu ya machozi!
 
Huyu mangi ni proffesional killer

Ndio kazi yake..alikua kituo cha sitakshari nadhan mnajua shughul za hicho kituo

Sijui kwa sasa yupo chimbo gani!!

Kaskazin nadhan aliweka rekod kwa kutoa roho za wahalifu
 
Aiseee nilikuwa nadhani ni mimi tu ndo namkumbuka yule Pot kwa members wote wa Jf, kumbe tupo wengi tunaomkumbuka!

Kiukweli, kwa mtu ambaye hakuwahi kumuona au kuingia kwenye 18 za huyu njagu anaweza akadhani jamaa tunampamba bure au tunazungumzia story ya abunuasi.

Nilikuwa namuona sana pale Uwanja wa Taifa wa zamani (shamba la bibi). Na mimi kama mrukaji ukuta maarufu enzi hizo nilishanusurika mara kadhaa kuingia mikononi mwake. Nakumbuka sometimes jamaa alikuwa na mbwa, na mbwa huyu alikuwa anafata maelekezo ya afande Sharp kwa namna ya kushangaza sana.
 

Kuna Siku moja nikiwa pale pale Shamba la Bibi ( Taifa ) huku nikiwa bado ni Mdogo kabisa Kipindi kile Katibu Mkuu wa Simba SC alikuwa Mzee Mmoja Mbabe sana ( sasa Marehemu ) Priva Mtema niliwahi Kuona Mbwa wa Mkama Sharp akiondoka na Kipande cha Nyama cha Tako la Kushoto la Mhalifu na sina uhakika kama alipona ile Siku au alikufa baadae.
 
Huyu 7 6 ana mtoto wake wa kike anajiita tunda [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sharp na mbwa wake (mbwa wa polisi).

Si mara 1 au mara 2 niliwahi kumwona Sharp akiwa na mbwa. Kuna wakati angemwacha mbwa karibu na geti la kuingia kwenye Uwanja wa Taifa wa zamani (shamba la bibi) bila kumfunga popote.Angemwamrisha "tulia hapa hadi nikukute, usiondoke!" na mbwa angatulia hapo. Hata akikuona unajipenyeza getini kiwizi wizi au unajaribu kuruka ukuta mbwa huyo asingekuwa na time na wewe.

Ila ole wako aamrishwe kukukamata ndo utaisoma namba.Afande Sharp angemwelekeza mbwa wake " unamwona yule jamaa aliyevaa kofia ya blue, t-shirt nyeupe na jeans ya blue?nenda kamkamate!" Ni hivi mbwa angekusonga wewe tu aliyeelekezwa akukamate (hata kama uko kwenye kundi la watu wengi, na angekukamata).

Iliwahi kutokea afande Sharp alimsakizia mbwa msela mmoja aliyekuwa anajaribu kupita chini ya geti, jamaa alivyoona atadakwa ikabidi akimbilie kwenye kambi ya jeshi ya Abdallah Twalipo (almaarufu 'Ngome') iliyo jirani kabisa na Uwanja wa Taifa na kituo cha mafuta. Jamaa alivyoingia kambini, wazee wa JWTZ waliokuwa zamu walimlinda na kumwambia asiwe na hofu, walichofanya ni kumsubiri mbwa aingie kambini kisha wamfanyie mambo ya Samson na Simba wa Wafilisti. Ila yule mbwa alikuwa na akili bhana, alifunga breki getini na kurudi kwa boss. Wajeda wakamwambia Sharp "huyo mbwa wako na wewe mwenyewe leo tulitaka tuwafundishe adabu.Rudia tena uone". Sharp hakujibu neno.

Ila huyu Pot alikuwa tishio kwa wahuni kwakweli.Kuna mtoto yupi wa mjini ambaye hakumfahamu?
 
wamekupa rangi zake zote mkuu.nyeupe na nyeusi yake.

hivi unajisikiaje ukiambiwa huyu mtu hapendi tabia fulani,lakini ni muelewa sana kama umefanya kwa kutokukusudia!!!!!

halafu unasikia wanaume na mbavu zao wanaufyata akikatiza,kwanini yeye tu na si manjagu wengine???maana yake hakuwa wa kawaida anapoamua kukutolea betri.
 
 
mbwa alijua atapigwa risasi.

mbwa yule wa polisi ni sawa na farasi,ana uwezo wa kujua dhamira iliyoko usoni kwa mtu.
 
Huyu afande Nkama Sharp alikuwa anamiliki kikundi cha Mchiriku kilichoitwa Night star musical club ambacho makao yake yalikuwa mtaa wa Kibambawe Kariakoo.
 
hIVI MAYENU WA UBUNGO BADOO YUKOO OFISINII MJI ULIKUWA NA FURAHAAA ACHA SIOO WA SASA WANAKOMAA NA BAULA MPAKA WANA.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…