Kuna kipindi nilikuwa na mazungumzo na vijana fulani wa ughaibuni, na mnene mmoja aliyetoka serikalini na kwenda kufanya kazi mashirika ya kimataifa ughaibuni.
Nikawa nalalamika habari za Magufuli kujimwambafy.
Mnene yule akasema, sasa hivi tatizo linatoka kwa Magufuli tu, huku chini vinatengenezwa vi Magufuli vingine viingi.
Sasa nilivyoona hili nikakumbuka kauli ile.
Viongozi wa serikali wanatakiwa kujua maana ya "civilian leadership of the military".
Wanatakiwa kujua "perception creates its own reality".
Magufuli ameshindwa kuongoza katika hili.
Kikwete aliyekuwa mwanajeshi, ikambidi aondoke jeshini ili kubaki kwenye siasa, alilielewa hili vizuri sana. Ndiyo maana ni nadra sana kumuona Kikwete kama kiongozi wa serikali kavaa nguo za jeshi.
Mkapa hakuvaa hivyo. Mwinyi hakuvaa hivyo.
Nyerere, rais pekee wa vita Tanzania, nje ya kuhamasisha majeshi vita vya Kagera, hakuvaa magwanda ya jeshi.
Siku hizi mpaka ma DC wanavaa magwanda.
Scratch that, mpaka wanajeshi -si wanajeshi wastaafu, walio active- wanateuliwa kuwa ma DC.
Kwa hivyo haya ya kina Gondwe sishangai.
Kwa sababu wanamuiga mkubwa wao, Magufuli.
Ukiwauliza watakwambia wao ni viongozi wa kamati za ulinzi wilayani!
Na kama umekubali Magufuli kuvaa magwanda, huna sababu ya kuwakatalia hawa.
Wanachotofautiana na Magufuli ni scope tu. Wote ni viongozi wa kiserikali. Wengine wilayani, Magufuli kitaifa.