Huyu raia Godwin Gondwe amepata wapi ujasiri wa kuvaa sare za JWTZ?

Huyu raia Godwin Gondwe amepata wapi ujasiri wa kuvaa sare za JWTZ?

Ni Tanzania tu kuvaa hivi ni kosa la jinai .
20190929_095254.jpeg
 
Kuna kipindi nilikuwa na mazungumzo na vijana fulani wa ughaibuni, na mnene mmoja aliyetoka serikalini na kwenda kufanya kazi mashirika ya kimataifa ughaibuni.

Nikawa nalalamika habari za Magufuli kujimwambafy.

Mnene yule akasema, sasa hivi tatizo linatoka kwa Magufuli tu, huku chini vinatengenezwa vi Magufuli vingine viingi.

Sasa nilivyoona hili nikakumbuka kauli ile.

Viongozi wa serikali wanatakiwa kujua maana ya "civilian leadership of the military".

Wanatakiwa kujua "perception creates its own reality".

Magufuli ameshindwa kuongoza katika hili.

Kikwete aliyekuwa mwanajeshi, ikambidi aondoke jeshini ili kubaki kwenye siasa, alilielewa hili vizuri sana. Ndiyo maana ni nadra sana kumuona Kikwete kama kiongozi wa serikali kavaa nguo za jeshi.

Mkapa hakuvaa hivyo. Mwinyi hakuvaa hivyo.

Nyerere, rais pekee wa vita Tanzania, nje ya kuhamasisha majeshi vita vya Kagera, hakuvaa magwanda ya jeshi.

Siku hizi mpaka ma DC wanavaa magwanda.

Scratch that, mpaka wanajeshi -si wanajwshi wastaafu, walio active- wanateukiwa kuwa ma DC.

Kwa hivyo haya ya kina Gindwe sishangai.

Kwa sababu wanamuiga mkubwa wao, Magufuli.

Ukiwauliza watakwambia wao ni viongozi wa kamati za ulinzi wilayani!

Na kama umekubali Magufuli kuvaa magwanda, huna sababu ya kuwakatalia hawa.

Wanachotofautiana na Magufuli ni scope tu. Wote ni viongozi wa kiserikali. Wengine wilayani, Magufuli kitaifa.
Eeee bhana eeeee !!
 
Vita ikitokea ikawa kali ata wewe hapo mtaani utachukuliwa uende frontier..Ova Ova alisikika Kijana enzi za Rais Adolf
 
DC ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya husika!

Kwa hiyo vikosi vyote vya ulinzi katk wilaya husika yy ndo mwenyekiti.

Na huwa DC anapigiwa saluti pia akiwa wilayani kwake sambamba na kupeperusha bendera ya taifa ktk gari yake.
 
DC ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya husika!

Kwa hiyo vikosi vyote vya ulinzi katk wilaya husika yy ndo mwenyekiti.

Na huwa DC anapigiwa saluti pia akiwa wilayani kwake sambamba na kupeperusha bendera ya taifa ktk gari yake.

Hapo sasa ...pata picha mshauri wa mgambo wa wilaya cheo cha luteni au kapteni na mkuu wa wilaya (hana cheo cha kijeshi ) wakutane wote wamevaa unifomu za jeshi , nani wa kumpigia mwenzie saluti?
 
Soma hicho kifungu.

Nishakisoma mkuu, na kinaeleweka Vizuri , lkn pia kuna uhitaji wa mwanasheria kukielezea zaidi maana hakijasema specific about who is been entitled legally to wear those any National defense uniforms , otherwise tunaweza sema hata wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya, Ministry of Defence, president and so whatever has the credentials to dress up with those kind of uniforms,reason behind is “ are party of the security and defense cabinets as part of their responsibilities “
 
Mhe Dc sio raia kama sisi uyo ni mwenyekiti wa kamati yanulimzi na usalama ya wilaya maana yake ndiye.mlinzi namba moja wa wilaya,atakua alipewa na wanajeshi wenyewe wanajenga daraja maana yeye ndie operation kamanda pale
 
Labda kwa kuwa yeye ndiyo mwenyekiti wa ulinzi na usalama basi huenda anaruhusiwa

Ila hivi kwanini huwa wanapenda kuvaa za JW tu!! za magereza au zimamoto hawazipendi??
Mimecheka sana,vyombo vya ulinzi vina heshima yake kulingana na majukumu yake,la kwanza kabisa ni JWTZ,Linafuata polisi,magereza,uamiaji na mgambo
 
Hakuna uniform inayovaliwa bila kuwa na cheo, isipokuwa kwa commander in chief pekee. Hao wengine ni mbwembwe tu na kufanya waonekane.
Wigo ni kitu kibaya sana, yeye amevaa kwa kuiga lakini katika uhalisia hana mandate ya kuvaa, kuongoza vyombo vya dola kimkoa/wilaya sio kuingilia kwenye mavazi/taratibu zao bali ni kuwapa maelezo ya ufanyaji kazi tu.

Giving commands to someone’s this means ur a commander in chief that’s why wanavaa kama ulivyosema kwenye pragraph yako ya kwanza apo juu, otherwise utakuwa hujui kiundani hichi unachokitetea.
 
Halafu anajifanyaga mlokole huyo
Sijawahi ona mlokole akiwa ndani ya kombat za jeshi
Dah,mkuu ulokole na mtu kuvaa sare zs jeshi kuna ubaya gani ? Jeshini hakuna walokole ? Mi nahisi humpendi tu jamaa
 
Nguo aliovaa Gondwe sio sare ya JWTZ kwasababu ni T~SHIRT na Kofia za kawaida ; nguo ambazo leo hii mtu anaweza akaenda kwenye duka la MACY's au JC PENNY huko marekani au Canada na akanunua hizo nguo bila taabu yoyote!!! Ni ushamba na lack of exposure ndio inawasumbua watu; Gondwe angevaa tepe mabegani hapo mgekuwa na jambo la kudadisi!! Hizo Nguo za mabaka mabaka ni za kawaida sana ulaya na marekani kwa wenzetu. Waulizeni mabalozi wenu.
MAREKAN MBALI ZIMEVALIWA SANA NA DUKA MOJA LA PALE MLIMANICITY NA UNAKUTA HADI WATOTO WANA FULL JEZI

JAMAA ANA BIFU NA DC KACHEMKA MASIKINI YULE DOGO N MSTAARABU MNYENYEKEVU ANA HOFU YA MUNGU IO KAMA NYIE MAPOYOYO MNAFIA NJAA KUTAKA MWENZENU ATOLEWE MTEULIWE MMECHEMKAA SANA..SOGO YUKO JUU MPAKA MAWINGUNI
 
MAREKAN MBALI ZIMEVALIWA SANA NA DUKA MOJA LA PALE MLIMANICITY NA UNAKUTA HADI WATOTO WANA FULL JEZI

JAMAA ANA BIFU NA DC KACHEMKA MASIKINI YULE DOGO N MSTAARABU MNYENYEKEVU ANA HOFU YA MUNGU IO KAMA NYIE MAPOYOYO MNAFIA NJAA KUTAKA MWENZENU ATOLEWE MTEULIWE MMECHEMKAA SANA..SOGO YUKO JUU MPAKA MAWINGUNI
Jibuni maswali rahisi yaliyoulizwa badala ya kutetea uozo .
 
Back
Top Bottom