Huyu raia Godwin Gondwe amepata wapi ujasiri wa kuvaa sare za JWTZ?

Huyu raia Godwin Gondwe amepata wapi ujasiri wa kuvaa sare za JWTZ?

Labda kwa kuwa yeye ndiyo mwenyekiti wa ulinzi na usalama basi huenda anaruhusiwa

Ila hivi kwanini huwa wanapenda kuvaa za JW tu!! za magereza au zimamoto hawazipendi??
Hujawahi Muona mkuu wa Wilaya ya Hai akiwa na za polisi?
 
Mbaya zaidi hata wale ambao hawajawahi pitia hata mgambo unaweza kuwakuta wamevaa mavazi ya majeshi yetu.
 
Kuna yule dada kule Morogoro aliyepiga picha na nguo za jeshi za brigedia jenerali, tulisikia kwamba yule bigedia jenerali alichukuliwa hatua. Hakika huyu akiachwa itakuwa ni double standard. Mwenye ile picha ya yule dada hebu weka hapa kwa ajili ya kumbu kumbu.
 
Mleta mada kwani hujui kuwa huyo ni mwanajeshi? Aliyekuambia ni raia Nani?
 
So wewe una exposure kuliko JW wenyewe sio?haya soma hapo chini:

JWTZ ilisema kuwa wamewasiliana na Jeshi la Polisi ili kuchukua hatua za kisheria dhidi ya ‘Diamond Platnumz’ kutokana na kuvaa nguo za kijeshi akiwa jukwaani.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na jeshi hilo kutoka Makao Makuu yake Upanga, Dar es Salaam, ilieleza kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika.

“Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kwa wananchi wote kuwa ni kosa kisheria kumiliki au kuvaa sare za JWTZ kwa mtu yeyote asiyehusika. “Aidha, kumeonekana matukio kadhaa ya baadhi ya vikundi, ama mtu mmoja mmoja kumiliki au kuvaa sare za JWTZ. Inakumbushwa kuwa kwa yeyote atakayeonekana amevaa ama kumiliki sare hizo, sheria itachukua mkondo wake,” ilieleza taarifa hiyo ya JWTZ juzi.

Katika mazungumzo na simu na gazeti hili, Ofisa Habari wa Jeshi hilo, Meja Joseph Masanja, alifafanua kuwa kwa sasa tayari polisi wameombwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya tukio la Diamond na wenzake.

Meja Masanja alisema JWTZ imekuwa ikitoa elimu mara kwa mara ya kupinga uvaaji wa mavazi hayo kwa watu wasiokuwa wahusika, lakini wapo watu wanaoendelea kujivalia kama watakavyo.

Source:Tsn
Huo ni moja ya ujinga unaoendelea kwenye hiki kinchi. Ujinga mwingine ni ule wa kusema Usipige picha eneo hili.
 
Sahv vazi Hilo kiongozi yoyote wa kijani ruksa kulivaaa ila usiwe cdm tu

Ova
 
1. DC Gondwe amepataje credential za kuvaa sare za JWTZ?
2. Nani amempa DC Gondwe sare za JWTZ?
3. Sheria inasemaje kuhusu matumizi ya sare za JWTZ?



Kama kuna katazo hili la raia kutokuvaa sare za jeshi, kwanini hili limefanyika ?

Alikuwa kwenye operesheni inayofanana na ya kisheshi. Yeye ni mkt wa ulinzi na usalama wilaya hivyo vyombo vyote vya ulinzi na usalama wilaya zinamhusu.
 
Huyu ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama kiwilaya, sioni kama ni tatizo
Hapo umeelewa nini!?
sketch-1572414835566.jpeg
 
1. DC Gondwe amepataje credential za kuvaa sare za JWTZ?
2. Nani amempa DC Gondwe sare za JWTZ?
3. Sheria inasemaje kuhusu matumizi ya sare za JWTZ?



Kama kuna katazo hili la raia kutokuvaa sare za jeshi, kwanini hili limefanyika ?


Watu wanasiri nyingi sana. Yawezekana tunavyomfahamu sivyo alivyo.
Yawezekana ni mwanajeshi, kwani kuna wakuu wa mikoa ambao ni wanajeshi na wanavyaa sare za jeshi.
Pia JPM anavaaga na hakuna aliyeuliza.
 
Watu wanasiri nyingi sana. Yawezekana tunavyomfahamu sivyo alivyo.
Yawezekana ni mwanajeshi, kwani kuna wakuu wa mikoa ambao ni wanajeshi na wanavyaa sare za jeshi.
Pia JPM anavaaga na hakuna aliyeuliza.

JPM kuvaa ni sawa kwani yeye ni Amiri Jeshi mkuu...lakini kwa DC kuvaa sare za JWTZ hii ni mpya..Hata nafasi yake ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya haimruhusu kuvaa sare za jeshi....Awali ya yote napata taabu kuamini kama kweli Gondwe kama DC amevaa sare za jeshi...nataka niamini kuwa hii picha ni fake...Ila kama ni kweli basi lipo tatizo kubwa, na nataka niamini kuwa ataondolewa kwenye cheo hicho cha u-DC ..
 
Kwani akina Kibatala na Kambole wapo bize sana? Si muwaombe wakafungue shauri mahakamani?
 
Back
Top Bottom