Hakuna kosa hapo.DC ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya Wilaya na kwa msingi huo yeye ni Amiri jeshi mkuu kwa ngazi ya Wilaya huku Rc akiwa Amiri jeshi kwa ngazi ya mkoa. Tukumbuke kuwa hawa wote wanasimama kwa niaba ya Rais ambaye ni Amiri jeshi mkuu. Majukumuambayo angeweza kuyatimiza Rais wao ndio huyafanya kwa ngazi zao. Hivyo si dhambi na si kosa kisheria kwa RC au DC kuvaa nguo za kijeshi. Na wakati mwingine inapotokea oparesheni yoyote ya kiusalama DC anapaswa kuwa mstari wa mbele, na haendi kama DC anaenda kama Askari wa kwa ngazi ya Wilaya.