Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Akwilina: Padri Mayanga ataka aliyeua awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania

Hapo wa kulaumiwa ni wazazi na Ndugu wa Marehemu kwa kukubali kuingia kwenye huu mtego wa Serikali kujiingiza kwenye Mazishi ya huyu Binti. ili kujijengea Heshima na kuonyesha hisia zao kwa hiki kitendo cha binti yao kuuawa kwa makusudi na hawa polisi wangekataa Jambo hili na wao kumzika huyu Binti kwa gharama zao wenyewe. kwa hiki kinachotokea wamejidhalilisha aisee.
 
Mtoa amri
 
Bonge moja la point
 
Shithole country kabisa kabisa kabisa!
hili neno lina tafsiri zaidi ya mbili kwa kiswahili lakini yote yanahusiana na uchafu sasa Hatuwezi kuiita nchi yetu mku.ndu.
hatujafikia kudharau nchi yetu kiasi hicho kwa udhaifu wa viongozi wetu ambao wengi wetu tumewachagua kwa mkumbo bila kuhudhuria mikutano na kupima watatupeleka wapi na hata pale mmoja alipowaonya kuwa mtalimia meno bado mkakubali halafu leo wote tukubali tuiite nchi yetu mku.ndu pamoja wananchi wake wote hii hapana Babu!
 
Siyo rahisi kama unavyofikiria, ila hakimu wa haki ni Mungu mwenyewe......wako wapo leo Ngeleja na Nchimbi?!!
 
Sijaweza kuyasoma ila ni wakati Prof Ndalichako akitoa neno
 
R. I. P Binti Akwilina A.B.
Machozi, hasira, uchungu pamoja na maumivu kamwe haviwezi kurejesha uhai wako. Majonzi na huzuni uliyotuachia watanzania wenzako wenye moyo safi havina kifani.

Akwilina, Umekatishwa ndoto zako na maisha kama vile mshumaa uzimwavyo.

Lala salama.
Daima tutakukumbuka.. Kristo Yesu akuangazie mwangaza wake wa milele. Amina.
 
"Mimi ninasafiri (alikuwa akienda Bagamoyo), lakini sijajua nitarudi lini. Unajua ninapambana na maisha, nataka nitoke, lakini pia nataka niwasaidie wazazi wangu (wazazi wake ni wakulima na wafugaji), kwa hiyo niombee tu kwani na wewe pia utanufaika na mafanikio yangu.”

Maneno yake ya mwisho kwa ndugu yake na dada yake.

Painful. So much painful.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…