Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Akwilina: Padri Mayanga ataka aliyeua awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania

Nimeumia sana kwa msiba wa mdogo wangu huyu, natumia nafasi hii kusali na kukushukuru Mungu Baba mwingi wa rehema, ulimleta Akwelina kama ua zuri kwetu, tunashukuru kwa waliopata kumfahamu na kuishi naye, nakuomba Baba umpokee, umsamehe dhambi zake zote, wafariji wazazi wake, wadogo zake wote, kaka hata ndugu zake. Uwasamehe na kuwahukumu wale wote walio sababisha haya kadri utakavyoona inakupendeza.
Tunashukuru kwa kutufariji kipindi hiki kigumu cha msiba wa rafiki, mdogo wetu, mtoto wetu.

Sina la kuongea zaidi, akwelina pumzika kwa amani, siku moja tutaonana tena ! Amen !!
 
Padri sio kiongozi wa serikali ni wa kidini alitakiwa ajikite hapo tu akijua kuwa huyo mpiga risasi aweza kuwa mkatoliki ambaye aweza kuja kwake kuungama dhambi ya kuua.Mihemko ya kisiasa imemtoa kwenye reli ya upadre akaongea yasiyohusiana na upadre
Falsafa aliyotumia huyo padri kufikisha ujumbe ni ngumu sana kwa wenye vichwa vya panzi kama wewe kumuelewa
 
Pumzika kwa a mani binti yetu Dunia tunapita na binadamu sote tutakufa kiburi cha uzima kitakoma inahuzunisha sana Mungu atupe moyo mkuu na ajilipizie kisasi kwa wahusika.
 
Leo hii kuna matukio makubwa mawili yanafanyika ambayo yametokana na athari za maandamano yaliyofanyika siku ya Ijumaa Februari 16, 2018.

Tukio la kwanza ni la kuagwa kwa mwili wa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilin linalofanyika chuoni hapo; Tukio la Pili ni la Wafuasi wa Chadema waliokamatwa siku ya maandamano wakipandishwa Mahakamani.

Katika matukio yote mawili hatukumuona Mwenyekiti Mbowe aliyekuwa akiongoza maandamano haramu yasiyo na kibali ambayo yalisababisha madhara yote haya. Hajui pasipo kuitisha maandamano yasiyo na kibali pasingetokea madhara tunayoyaona leo?

Bado najiuliza, Mwenyekiti hajahudhulia msiba wa Akwilina kwa sababu hajaguswa nao? Ama sio wa muhimu kwake? Ama shida zetu sio zake? Inauma sana!

Kama haitoshi wale Wafuasi waliokamatwa wamekwenda Mahabusu kwa kukosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5 tu. Kweli wanakwenda Mahabusu kwa sababu wamekosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5?

Jambo la kushangaza, hakukuwepo hata kiongozi mmoja toka Chadema ambaye alikwenda Mahakamani kuwa nao bega kwa bega. Wanakwenda mahabusu kizembe kwa kuwasikiliza Wanasiasa ambao leo hii wamewatelekeza!!

Wamejikuta kwenye matatizo lakini wale waliosababisha wao wapate matatizo hawapo nao pamoja. Inauma sana!

Ninapofikia hapa nakumbuka ule msemo wa Rais Mstaafu Mzee Kikwete aliosema "Akili za kuambiwa, changanya na za kwako".

Hili ni funzo kwetu sote, tunapoambiwa na Wanasiasa tukafanye jambo ambalo tunajua tutakuwa matatani kisheria tuwe makini kuchanganya na akili zetu maana shida zitakazotupata zitakuwa ni zetu na si zao, mateso yatakuwa kwetu na si kwao.

Narudia tena kuwasihi, akili za kuambiwa changanya na za kwako.

*Na Thadei, Mwanaharakati Mpambanaji*
Siku mtapiga watu risasi na hakutakuwa na kiongozi wa upinzani wa kumtupia lawama.

Jitoeni akili tu. Jifanyeni hamuoni. Jifungeni macho na masikio. Jitieni mnajua sana kusimamia baadhi ya vifungu vya sheria huku vingine mkivifumbia macho.

Mtu anayekuogopa akikupiga, anakupiga kwa nguvu sana kwasababu moyoni mwake ana hofu kuwa utampiga yeye. Uwoga wenu umesababisha mtumie nguvu kubwa sana siku hadi siku.

Karma will strike.
 
Padri aliyehubiri msibani kusema mhalifu aliyepiga risasi awekwe wazi hapo padri kakosea ina maana huyo muuaji akienda kuungama kwake kuwa ameua akwilini atamwanika wazi huyo muuaji.Hilo haliendani na upadri wake.Hakustahili kuongea hivyo alitakiwi aombe huyo mtu atubu sio kusema aanikwe wazi .Hapo padri kawa influenced na mihemko ya kisiasa badala ya imani yake ya upadri.Anafukuza waumini wasipende kwenda kuungama dhambi kwa mapadri sababu waweza anikwa wazi any time
Stupid logic. Eti akienda kutubu atamwanika wazi. Usichanganye mambo ya kiroho na kijamii.
 
Inakuwaje katika msiba wa yule Katibu wa CHADEMA hatukuona waziri au kiongozi yeyoye wa serikali akiwemo mkuu wa Mkoa. Leo wote wako hapo wakionyesha majonzi ya kutisha. Je damu ya Aqulina ni nzito kuliko ya Daudi?

R.I.P Aquilina na Daudi
Inawezekana wanaamini yule alistahili lakini huyu ni 'bahati mbaya'
 
Akiwekwa wazi . Na aseme ni nani alimpa amri ya kupjga risasi za moto.
 
Leo hii kuna matukio makubwa mawili yanafanyika ambayo yametokana na athari za maandamano yaliyofanyika siku ya Ijumaa Februari 16, 2018.

Tukio la kwanza ni la kuagwa kwa mwili wa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilin linalofanyika chuoni hapo; Tukio la Pili ni la Wafuasi wa Chadema waliokamatwa siku ya maandamano wakipandishwa Mahakamani.

Katika matukio yote mawili hatukumuona Mwenyekiti Mbowe aliyekuwa akiongoza maandamano haramu yasiyo na kibali ambayo yalisababisha madhara yote haya. Hajui pasipo kuitisha maandamano yasiyo na kibali pasingetokea madhara tunayoyaona leo?

Bado najiuliza, Mwenyekiti hajahudhulia msiba wa Akwilina kwa sababu hajaguswa nao? Ama sio wa muhimu kwake? Ama shida zetu sio zake? Inauma sana!

Kama haitoshi wale Wafuasi waliokamatwa wamekwenda Mahabusu kwa kukosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5 tu. Kweli wanakwenda Mahabusu kwa sababu wamekosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5?

Jambo la kushangaza, hakukuwepo hata kiongozi mmoja toka Chadema ambaye alikwenda Mahakamani kuwa nao bega kwa bega. Wanakwenda mahabusu kizembe kwa kuwasikiliza Wanasiasa ambao leo hii wamewatelekeza!!

Wamejikuta kwenye matatizo lakini wale waliosababisha wao wapate matatizo hawapo nao pamoja. Inauma sana!

Ninapofikia hapa nakumbuka ule msemo wa Rais Mstaafu Mzee Kikwete aliosema "Akili za kuambiwa, changanya na za kwako".

Hili ni funzo kwetu sote, tunapoambiwa na Wanasiasa tukafanye jambo ambalo tunajua tutakuwa matatani kisheria tuwe makini kuchanganya na akili zetu maana shida zitakazotupata zitakuwa ni zetu na si zao, mateso yatakuwa kwetu na si kwao.

Narudia tena kuwasihi, akili za kuambiwa changanya na za kwako.

*Na Thadei, Mwanaharakati Mpambanaji*
Umeandika upuuzi mwingiii
 
NENO
 
Back
Top Bottom