Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NimesomaView attachment 699855
Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwamo ya kumtaka waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kujiuzulu.
Ibada hiyo inafanyika leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali.
Waombolezaji hao walinyanyua mabango hayo baada ya waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliponyanyuka kutoa salamu kwa wafiwa kama walivyofanya viongozi wengine, akiwamo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Baadhi ya ujumbe katika mabango hayo ni; “muuaji hawezi kujichunguza na Mwigulu, Sirro kwa mauaji haya bado mko ofisini.”
Juhudi za kuwataka waombolezaji hao kushusha mabango ziligonga mwamba kutokana na baadhi ya watu waliokuwa karibu yao kuja juu, wakitaka waachwe kwa maelezo kuwa wana haki ya kufanya hivyo.
Katika salamu zake za rambirambi, Profesa Ndalichako alisema: “Rais Magufuli ameshaagiza uchunguzi ufanyike na mimi kama waziri nasisitiza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi haraka.
“Matukio ya aina hii hayapaswi kuendelea, nimehuzunika kwa msiba huu na naomba Watanzania waungane kuiombea familia.”
Soma: Padri ataka aliyempiga risasi Akwilina awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania -VIDEO
Nami pia nilitaka kumjibu UWONGO mbona hamna mambo ya kujiuzulu?Mbona sioni mabango yenye kile ulichoandika?
J2 wanakaa viti vya mbele Kabisaa eti wameenda kuabudu...hawa watu hawa..... Kuna sikuDaah dunia hii hakuna haki kabisa, Dada wa watu walimpiga risasi na kumuua ili tu wasalie madarakani! Hatari sana hii, halafu kuna wapumbavu fulani nao wanaunga mkono harakati hizi!
Umeona ehhMsiba na mambo ya 'vyanzo vya maji kujengewa fensi' wapi na wapi? Huu sasa upu.mbavu wa mleta mada
R.I.P Aqwilina AcqulineBila bila
Mkuu,
Poise, huwa sishabikii vyama.vya siasa.
Jiulize, NEC na DED wa Kinondoni umewaona kwenye msiba wakisindikiza Akwilina!?
Au umewaona katika mahakama ya kisutu wakisomewa mashitaka ya kuwa chanzo kikuu cha kifo cha Akwilina B!?
Acha kufanya propaganda za kiuchwara mbuzi kwenye mambo yasiyohitaji siasa.
Tanzania, tatizo lake ni
CCM. CCM must go...
Kagame. Kagame must be stopped visiting Tanzania.
(Maana, amefanywa kuwa waziri na mshauri wa serikali ya ccm ndiyo matokeo yake hayo)
Management ya NEC na DED wa Kinondoni watumbuliwe wafungwe. Ndiyo wauaji polisi ilikuwa ni chaneli tu ya kuua ila.NEC, DED na CCM ndiyo wauaji.
Mwisho,
We need an immediate justice for our daughter Akwilina B.
R.I.P Binti, Akwilina A. B.
Ndoto zako zote zimezimwa ghafula kama vile mshumaa uzimwavyo.
Daima tutakukumbuka Binti, Kristo Yesu akuangazie mwangaza wake wa milele. Amina.
Weka picha yenye uhalisia Piliz.View attachment 699855
Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwamo ya kumtaka waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kujiuzulu.
Ibada hiyo inafanyika leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali.
Waombolezaji hao walinyanyua mabango hayo baada ya waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliponyanyuka kutoa salamu kwa wafiwa kama walivyofanya viongozi wengine, akiwamo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Baadhi ya ujumbe katika mabango hayo ni; “muuaji hawezi kujichunguza na Mwigulu, Sirro kwa mauaji haya bado mko ofisini.”
Juhudi za kuwataka waombolezaji hao kushusha mabango ziligonga mwamba kutokana na baadhi ya watu waliokuwa karibu yao kuja juu, wakitaka waachwe kwa maelezo kuwa wana haki ya kufanya hivyo.
Katika salamu zake za rambirambi, Profesa Ndalichako alisema: “Rais Magufuli ameshaagiza uchunguzi ufanyike na mimi kama waziri nasisitiza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi haraka.
“Matukio ya aina hii hayapaswi kuendelea, nimehuzunika kwa msiba huu na naomba Watanzania waungane kuiombea familia.”
Soma: Padri ataka aliyempiga risasi Akwilina awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania -VIDEO
Nahili jambo watanzania walio wengi hawalielewi. Elimu elimu elimu.Anayedhani yuko salama asikilize vizuri clip ya mama Aquilina akimwambia prof Ndalichako kwamba alikuwa akisikia kwenye vyombo vya habari watu wanauawa na polisi lakini hakutegemea hata siku moja kwamba hilo litatokea kwa mmoja Wa wanafamilia wake. AJIDHANIAYE AMESIMAMA AANGALIE ASIANGUKE.