Ibada ya Wakristo kuabudu Jumapili imeanza Karne ya nne. Ni kwanini Karne 3 za kwanza watu waliabudu Jumamosi?

Ibada ya Wakristo kuabudu Jumapili imeanza Karne ya nne. Ni kwanini Karne 3 za kwanza watu waliabudu Jumamosi?

Dini zina upuuzi, mwingi, karne ya 19,huko ulaya, watu walikuwa wanalipa ili waombewe, wanatoa sadaka zaidi ili Mambo Yao yaende vzr, waepuke umaskini, na magonjwa, makanisa, yakawa tajiri Sana, ilipokuja industrial revolution, watu wakagundua kuwa kumbe unaweza kubadilisha maisha yako kwa kufanya kazi na kutumia sayansi, watu Waka kacha kwenda nyumba za ibada!sasa yaliyofanyika karne 19! Ndio yapo Leo bongo, pale kawe kwa mwamposa, watu wanaenda "kutatuliwa matatizo" yao ya kiuchumi, ki afya, nk,
Wanazidi, kuwa, maskini, wenye makanisa yao, ndio, wanazidi kuneemeka.


Huo siyo ukristo huo ni upagani wa kanisa katoliki ambao waliuendesha kwa miaka mingi sana, Haijaandikwa popote kwenye biblia kwamba ulipie ili uombewe dhambi zako.

Tukizungumza mafundisho ya kipagani ya ukatoliki ni pamoja na hili
 
Ili kuonyesha kwamba hajabadili aliwaroga na kitu kimoja kwa kuwaambia kuwa Siku itabaki kama ilivyo ila tarehe ndo itabadilika..
Unafiki ni kweli siku zilibaki hivyo hivyo na kilichobadilika kilikuwa ni Tarehe peke yake..
Hebu naomba tustick kwenye kifungu hiki pekee,

Ingemake sense kama ungeniambia alibadili siku yaani leo ni jumanne, yeye akasema kesho itakuwa jumatatu(ambapo ingetakiwa kuwa jumatano), Lakini kama aliacha siku za week zikaendelea kucount kama zilivyokuwa awali then hakuna kilichobadilika, (Kwa nilivyoelewa). Ila tarehe tu,
 
SHIDA IKO WAPI, JAMBO LOLOTE JEMA LIKIAMULIWA NA KANISA HAPA DUNIANI, MBINGUNI LINAPIGWA MUHURI WA NDIO
Tumekatazwa kufuata mafundisho yoyote ya binadamu!

Mambo yote ambayo Mungu aliamua aliyapitisha kwa watu na ndio hayo unayaona kwenye Biblia. Sasa huwezu kutulazimisha tuwafuate viongozi wako wa dini tuiache Biblia. Huku ni kumkosea Mungu.
 
Kwa hiyo ukisoma vizuri hayo maandiko ya Waebrania utaona kwa mwamini kila siku ni sabato, unaingia siku yeyote na unaendelea kudumu ndani ya sabato siku zote. Hii ndo sababu wako wakristo wanakutana Ijumaa kusali kwenye nchi za kiislamu na sio tatizo kabisa maana kila siku tunapaswa kumwabudu Mungu.
Kila siku ni sabato?????

So kila siku tustarehe????

Luka 23:56 inasema "Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa."

Kama ilivyoamriwa na nani?

Hao ni akina Mariamu Magdalena ambao muda mwingi wamekuwa na Yesu na wanapumzika siku ya sabato masaa machache baada ya Yesu kufa. Je huo ulikuwa ni utaratibu mpya kwao?

Je kwenye Biblia sehemu zote ilipotajwa sabato walimaanisha ni siku yoyote?

Mbona Ijumaa imetajwa kama siku ya maandalio na Jumapili imetajwa kama siku ya kwanza ya juma?
 
8
Ni sawa lakini wao ni wayahudi na wewe ni mkristo wao hawamtambui ukristo ndo maana hata makanisa yamepigwa mabomu Hebu fafanua hiyo siku ya sabato Ina rangi gani. Vipi kama mtu atafanya KAZI siku zote harafu ataamua kupumzika Kila jumatano.
Jumatano ni siku ya saba ya Juma?
 
Sabato ilianzia agano la kale

Onyesha kwenye agano la kale ambako sabato ndiko ilikoanza ni wapi inatajwa jumamosi?
Kwa hiyo agani jipya siyo biblia tuchache tutupe?
 
Sabatho ya sasa tofauti na ya zamani lmekuja sabatho nyingine
Si ajabu kama hiyo unayotaka kusema wayahudi walimshitaki Kwa kuhalifu sabatho Yao
Soma Kwa utulivu wakolosai 2:8-23 utabarikiwa
Mzee hii wakolosai 2 mnaitumia sana kupotosha watu, kabla sijaendelea naomba tukubaliane Paulo aliabudu jumamosi, Soma matendo ya mitume 17:2
 
Kwani Yesu mwenyewe amesemaje? Na hao wakristo unaowasema karne ya 1,2,3 walikuwepo Mimi najua ukristo ni baada ya kristo na huo ukristo umeenezwa na akina Paulo mpaka na wewe umeupata, Yesu alimwambia yule Msamaria mwenye swali kama lako yeye msamaria alikomalia eneo la kumuabudu Mungu ila wewe umekomalia siku ya kumuabudu Mungu Yesu alimjibu saa imefika nayo ni sasa ambayo waabudu halisi watamwabudu Mungu katika roho na kweli, kinachotakiwa ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli na Mungu ndio anawataka hao, kuabudu jumamosi, jumapili, jumatatu au siku yoyote hakumpeleki Mungu mbinguni bali aliye na Moyo safi
 
Mungu aliagiza tuabudu siku ya kwanza ya juma ambayo ni jumamosi, hebu nenda kanisani muulize kiongozi wako wa dini, sabato ni juma ngapi?
Aliyesema jumamos ndio siku ya Kwanza ni Nani?
 
Mzee hii wakolosai 2 mnaitumia sana kupotosha watu, kabla sijaendelea naomba tukubaliane Paulo aliabudu jumamosi, Soma matendo ya mitume 17:2
Hebu inukuu yote bila kuacha neno kisha tufafanulie nini maana yake
 
Siku zote ni za Kumwabudu Mungu! Mungu anachotaka ni Kumwabudu katika Roho na Kweli,(Yohana4:23-24)
Tukishamjua Mungu au kujulikana naye,hatufungwi na Siku au Sikukuu au Sabato,wala sheria za Vyakula au Vinywaji! BWANA Yesu aliyatimiza Yote pale Msabani.
Wagalatia4:8-11
Wakolosai 2:16-18
Waebrania4:4-8
Nyakati zile kabla ya karne ya tatu walisali siku ya Sabato kama desturi lakini siyo kama Sheria! Wanafunzi walipotawanyika mataifa yote kwenda kuhubiri Injili,hakuna ko kote walipowataka Mataifa kusali Jumamosi.
 
Hebu naomba tustick kwenye kifungu hiki pekee,

Ingemake sense kama ungeniambia alibadili siku yaani leo ni jumanne, yeye akasema kesho itakuwa jumatatu(ambapo ingetakiwa kuwa jumatano), Lakini kama aliacha siku za week zikaendelea kucount kama zilivyokuwa awali then hakuna kilichobadilika, (Kwa nilivyoelewa). Ila tarehe tu,
Ok Sawa japo nimeshalielezea ngoja ntakuelezea kitu ili unielewe zaidi...

Ngoja nitumie mfano hai kukuelekeza...

Lets say leo kasema kuwa Atabadilisha siku na keo ni 07/11/2023...siku ya Jumanne
Na akasema kesho iwe tarehe 17/11/2023
Ikumbukwe kwamba tarehe 17 ingekuwa Ijumaa kama isingesogezwa kesho..
Kwa hiyo alipoisogeza akaifanya kuwa Jumatano..
Kwahyo hiyo skipping days ikachange siky ya Ijumaaa kuwa junatano..
Its seems kuonekana sawa but hiyo sio sawa..
Kwa mfano sikukuu ya christmass ilikuwa tarehe 25/12/2023 siku ya jumatatu unafikiri itakuwa siku ya jumangapi baada ya hiyo displacement?

Huko ndo kubadili majira kusikoumiza wala kujulisha..

Kuna huwa ni magumu Mpaka utumie ufahamu mkubwa na ndo maana biblia kuna wakati inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...

Na kuna wakati kwenye ile 666 biblia haisemi kila mtu atajua kuhusu hiyo kitu ila inasema...

"Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni 666."

Anasema hapo ndipo penye hekima kwa lugha nyingine penye ujuzi na yeye aliye mwenye ujuzi..
Maana si rahisi kutambua vitu baadhi kutoka kwa mwovu
 
Waafrica wengi tumegawa kwenye fikra ma mitazamo juu ya imani! Kama wewe unaamini unaabudu Mungu wa kwel yann umlazimishe mtu awe kama wewe, inuka ukafanye kazi acha kubishana maslwala ya siku au juma ama mwezi, uliletwa dunia sio kubishana na watu bali kuishi
 
Kila siku ni sabato?????

So kila siku tustarehe????

Luka 23:56 inasema "Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa."

Kama ilivyoamriwa na nani?

Hao ni akina Mariamu Magdalena ambao muda mwingi wamekuwa na Yesu na wanapumzika siku ya sabato masaa machache baada ya Yesu kufa. Je huo ulikuwa ni utaratibu mpya kwao?

Je kwenye Biblia sehemu zote ilipotajwa sabato walimaanisha ni siku yoyote?

Mbona Ijumaa imetajwa kama siku ya maandalio na Jumapili imetajwa kama siku ya kwanza ya juma?
Ndio kila siku ni sabato ya kiroho. Waamini wa sasa hivi ni wa kiroho na wanafuata sabato ya Mungu mwenyewe.

Sabato ni pumziko, wanaomwamini Yesu wamepata pumziko la kiroho sio la kimwili kama walilopewa Israeli.

Kumbuka Yesu aliishi agano la kale japo yeye ndo alileta agano jipya kwa hiyo ni sahihi kukuta wakina Magdalena waki observe sabato ya kimwili kama waisraeli wengine walivyokuwa wameagizwa
 
Kwa sababu umewaza Kibinadamu yes ila kwa Mungu mambo hayako hivyo.
Kwani wewe ni Mungu?
Haya, mimi nimewaza kibinadamu, haya wewe uliyewaza kimungu njoo na hayo mawazo yenye kujibu hizo changamoto.

Yaani mshika Sabato wa zama hizi, atakwambia Jumamosi hafanyi kazi kwa kuwa ni siku ya sabato lakini hapo hapo anataka kupewa huduma zote siku ya jumamosi kutoka kwa watu wanaofanya kazi siku hiyo. Kwa mfano;
1. Atapanda usafiri wa umma (Anasahau kuwa dereva yupo kazini)
2. Atatumia umeme (anasahau kuna utiriri wa wafanyakazi wa TANESCO wapo kazini kuhakikisha umeme upo)
3. Atatumia simu (Anasahau kuna utiriri wa wafanyakazi wa mitandao ya simu wapo kazini)
4. Atatumia maji...
5. Atataka usalama...
 
Mzee hii wakolosai 2 mnaitumia sana kupotosha watu, kabla sijaendelea naomba tukubaliane Paulo aliabudu jumamosi, Soma matendo ya mitume 17:2
Hivi unajua Paulo alichokuwa anakuhubiri, unajua paulo alitumwa awahubiri akina nani?

Unajua kuwa paulo alitamani ndugu zake(wayahudi) waokolewe pamoja na kwamba walishika sabato ila walikuwa wamepotea. (Rum 10 : 1-3)

Paulo alihesabu juhudi zote za yeye kuwa farisayo(mtu aliyebobea katika kusoma na kutenda torati) kuwa ni hasara (flp 3 : 2 -10)

Soma tena paulo alisemaje gal 3 : 10-14, je unaijua baraka ya Ibrahim iliyopaswa kuwafikia mataifa?

Muangalie Yesu alichukua hatua gani kwa mambo yanayohusu sabato, biblia inasema Yesu alivunja sabato unayo ipigia kelele hapa. Je huoni haya kwenda kinyume na "Mwana" wa Mungu(Kristo) bali unataka umsikilize "mtumishi"(Musa)?( Yoh 5 :17-18)

Yesu asema hivi:
Yohana 5:45
Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.

Paulo nae asema hivi:

nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa.
2 Kor 3:13‭-‬16 SUV

Sasa fikria, Kama kusoma torati ya Musa(Amri za Mungu) utaji unaziba moyo wako yaani unapotea, Je kumgeukia Bwana ndio kupi?

Karibu nyumbani mwa Bwana huku tupo huru wala hatuna mshtaki.
 
Kwa sababu umewaza Kibinadamu yes ila kwa Mungu mambo hayako hivyo.
Na ukitaka kutekeleza, unatekeleza kama binadamu na si kama Mungu

Mk 3:4 SUV​

Akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? Kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza.
 
Toa uthibitisho kuwa Musa siku alipowr amri 10.hiyo sabato aliambiwa ni Jumamosi
Yesu alikufa siku ya Ijumaa, akashinda kaburini siku ya Sabato, na akafufuka siku ya kwanza ya juma ambayo ni Jumapili
Hii inaonyesha kuwa siku ya saba ya juma ni Jumamosi
 
Back
Top Bottom