Yeye ni muislam, Azam channel ya muislam imemuweka awe anachambua masuala yote yanayoigusa Israel na Hamas, pamoja na wahurthi.
Mfalme, kwako wewe unaumia unapoona Muislam anachambua masuala ya Mashariki ya kati? Mbona unaonesha hisia hasi kwa Watanzania wenzio kisa dini? Unataka kumaanisha kwamba vyombo vyote vya habari vinavyomilikiwa na wakristo ni marufuku mkristo kuchambua masuala na vile vinavyomilikiwa na waislam iwe marufuku muislam kuchambua? Hapa unachochea ubaguzi ambao hauna afya yoyote kwa taifa.
1. Anasapoti wahurthi Yemen, na anasema wanafanya cha maana kuzuia meli zisiende Israel na dunia iache unafiki, ishughulikie kwanza vita ya Gaza ili wahuthi waacha kushambilia meli (ambazo hata sio za Israel).
2. Anasema Bandari ya Eliat ambayo ipo Israel, ipo kwenye ardhi ya Palestina. Amesahau kwamba Umoja wa mataifa unaitambua Israel kama nchi na hauitambui palestina kama nchi.
Kwanini UN hawaitambui Palestine kama nchi? Na umoja wa mataifa ni nani? Kwa maoni yako na utashi wako unaona Palestine haistahili kuwa nchi bali inastahili kutawaliwa?
Kama UN wameitambua Israel kama nchi, mfanyakazi mmoja wa serikali ya Tanzania anakujaje leo kusema Israel sio nchi? Na kwamba ile bandari haipo ISrael ipo palestina?
Bila shaka wewe ni mfuatikiaji mzuri wa siasa za kimataifa, Katibu Mkuu wa UN alisema nini juu ya mzozo wa Isreal na Palestine? Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa ndio mfanyakazi namba moja wa serikali alikuwa na msimamo upi juu ya Palestine?
3. Yeye ni mfanyakazi wa Mwalimu Nyerere Memorial Academy, chuo cha serikali, serikali haina dini, na hata kwenye migogoro yote hii serikali haijatamka lolote kwasababu wanajua nchini kuna wafuasi wengi wanaoipenda Israel na wengi wanaoipenda Palestina, huwezi kusimamia upande mmoja labda kama haupo serikalini.
Serikali kutotamka lolote kwa wakati huu sio hoja, Mwalimu Nyerere alikuwa ni Rais wa nchi na ni Mkristo lakini haikumzuia kuweka msimamo wake dhidi ya Isreal ambapo aliona kinachofanywa na Waisrael huko Palestine sio haki. Na yeye Mwalimu alipambana na kuwatetea waliodhulumiwa ikiwemo Afrika ya Kusini dhidi ya Makaburu.
Anapokataa uwepo wa Israel wakati bado anafanya kazi serikalini, anafanya hivyo kwa kuwakilisha chuo cha mwalimu nyerere au anafikiri nini? Chuo kimwangalie kwasababu suala la dini, Israel na palestina sio laini, linaweza kuharibu mshikamano wetu.
Anakataa uwepo wa Isreal mahala gani? Vipi kuhusu mipaka ya mwaka 1967 inayotambuliwa na Umoja wa mataifa ambayo Isreal kila kukicha inaendeleza makazi ya Wayahudi na kunyang'anya ardhi ya Wapalestine, unalionaje hili Mfalme?
Afrika Kusini wala sio nchi ya kiislam na haiongozwi na muislam lakini kutokana na kinachofanywa na Isreal huko Gaza nchi imeamua kusimama dhidi ya Isreal, hapo ndugu Mfalme una maoni gani pia?
Unadhani Ramaphosa anasimama dhidi ya Isreal anatetea uislam? Ana udini? Jibu ni hapana bali anatetea UTU, UBINADAMU na kupinga dhulma, unyanyasaji, ukatili ambao kimsingi huwezi kutofautisha na UGAIDI ambacho ndicho kinachofanywa na Isreal huko Gaza.
Au Mfalme, ukiondoa dini yako na ukaamua kubaki na utu wako, kwa dhati yako kabisa unaona wale watoto, wanawake, wazee maelfu kwa maelfu wanaouwa kila siku na Isreal ni sawa?
Na unadhani nini kifanyike ili utulivu na amani ya kudumu ipatikane huko Isreal na Palestine?
Au Mfalme utaungana na wale mawaziri wawili wa Isreal waliotangaza waziwazi kwamba Wapastina wote waangamizwe na mwenzie akasema Wapalestina wote wafukuzwe na pajengwe nyumba za waisreal?
4. Ni mtanzania wa aina gani tena mfanyakazi wa serikali anaweza kuongea mbele ya chombo cha tv kwamba wahurthi Yemen wasilaumiwe badi Israel ndio ilaumiwe?
Huyu hatakuwa mfanyakazi wa kwanza kueleza sababu au kiini cha machafuko huko Isreal na Palestine. Katibu Mkuu wa UN mbele ya vyombo vya habari vya kimataifa alibainisha wazi kuwa vitendo vinavyofanywa na Isreal kwa Wapalestine ndio vinachochea matokeo hasi. Lau Isreal ingekuwa inawatreat kiutu Wapalestina, kutambua uhuru wao, utaifa wao na kila mmoja akaheshimu mipaka ya mwenzie yamkini hata jina la Hamas usingelisikia Mfalme.
Kwahiyo eneo lile la bahari ya wote ambalo magaidi ya Yemen yanazuia nchi zingine zisipite sio ugaidi? Na yeye tuseme sio gaidi? hivi gaidi akija nyumbani kwa IBRAHIM RAHBI hawezi kumhifadhi na akasababisha matatizo nchini kwetu kama ana mlengo huo? yeye sio gaidi? hasapoti magaidi?
Ndugu Mfalme unapaswa kuwa fair kwa mambo ya huko. Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani wanatoa fedha na mabomu kuyapeleka Isreal ili yatupwe Gaza kuteketeza na kuchanachana mpaka miili ya watoto na wanawake kwa kisingizio cha kujilinda, huu wewe huoni kuwa ni ugaidi wa kutisha zaidi kuliko hata ugaidi wa Wahuthi?
Marekani inapotoa silaha kwa Isreal iangamize hata wasio na hatia huko Gaza na kweli imeangamiza vya kutosha huoni kama hili pia linapaswa kukemewa kama ambavyo wahuthi wanapozuia meli za Isreal na wafadhili wake kushinikiza waache kuendelea kuangamiza maisha ya wasio na hatia huko Gaza.
Mwisho; kama huyo Mchambuzi anasapoti kusimamisha mauaji ya Isreal huko Palestine na kwa sapoti hii wewe unamnasibisha na gaidi basi kufanya hivyo unaleta tafsiri kuwa hata Mwalimu Nyerere, Nelson Mandela na sasa Ramaphosa wanatetea ugaidi duniani.
Usisahau hata Mandela wakati anapigania uhuru dhidi ya ubanguzi na ukatili wa Makaburu naye aliitwa Gaidi na akafungwa jela kwa ugaidi wake. Unaamini Mandela kweli alikuwa Gaidi?
Mfalme, tumia Ufalme wako kusimamia haki, uadilifu, usawa, utu na uhuru. Ufalme huohuo utumie kupinga dhulma, ubaguzi, unyanyasaji, unyonyaji kwa wananchi wako bila kujali dini zao, makabila yao, jinsia zao.