ICC yakiri kupokea rasmi malalamiko kutoka Tanzania juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi uliopita

ICC hawapokei na kushighulikia barua za individuals

Zitto kaandika peke yake akiwa kajifungia ndani na Maria Sarungi naye kajiandikia peke yake !!!

Pursuant to Article 15 of the Rome Statute, any individual, group, or organization can send information on alleged or potential ICC crimes to the Office of the Prosecutor (OTP) of the ICC.

Au hujui kiingereza. Mahakama hii hupokea taarifa toka kwa watu binafsi, kikundinau taasisi.

Wewe unaandika upumbavu kuwahadaa watu kuwa mtu binafsi haruhusiwi.

Unaweza kuwa mjinga, ukaufurahia ujinga wako, ukaishi nao. Lakini ni kosa kubwa la kimaadili kutaka watu wengine nao wawe wajinga kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya tunasubiri mkuu!!
 
Mkuu tupe kidogo insight ya hii Rome Statute. Ni makosa gani au ya aina gani ICC wanashughulika nayo. Itasaidia sana kufunga huu mjadala
The core mandate of the ICC is to act as a court of last resort with the capacity to prosecute individuals for genocide, crimes against humanity and war crimes when national jurisdictions for any reason are unable or unwilling to do so.

Watu wengi hawaelewi. Wanachojua ni kuwa ICC inashughulika tu na genocide. Mauaji na uonevu na ukiukaji wa haki za msingi hapa nchini, siyo genocide lakini ni uhalifu unaoangukia kwenye crimes against humanity. Na kwenye hili wala haihitajiki mpaka watu wafe au wateseke kwa maelfu.

Kinachoweza kuifanya mahakama hii iyakubali mashtaka haya ni ukweli kuwa mahakama za Tanzania zipo mfukoni mwa Rais na Serikali, badala ya kuwa muhimili unaojitegemea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes kwa Sababu wamewekwa and they must comply with their Lord's wishes!
 
Ila haya maisha ya sasa yanatisha aisee.
Yaani kuna watu hatuna amani, ni hofu na huzuni.
 
Mahakama za Tanzania zipo mfukoni mwa Magufuli! Umehudhuria Mahakamani Mara ngapi!? Huu ni ujinga mwingine kwa kuopima Mahakama kwa Sababu ya kesi za Wanasiasa. Incompetence ya Mahakama haiwezi kupimwa kwa kesi ya Mbowe au Msigwa tu. Unajua Mahakama kwa mwaka Inaamua kesi ngapi ba unajua ni watu wangapi wanatendewa haki na Mahakama. Mbona mnakuwa wajinga kiasi hiki. Kuwa mwanasiasa hakukufanyi wewe uwe juu ya Sheria. Wakishakuwa kuwa Wanasiasa, wakishtakiwa hata Kama ni halali watasingizia Siasa. So kwa Afrika Siasa ni kichaka Cha kutafuta Kinga!
 
Tunataka Mungu aamue hii kesi kama alivyofanya kwa Anania na Safira.
Mtudanje tu maana hata huko Mahakamani tunapoteza muda,
 
Let's be party of change for Tanzania democracy
 
Hii ni nzuri, japo inaweza kuchukua muda kidogo.

Watahitaji kujiridhisha kwanza, kama uhalifu tajwa upo ndani ya mamlaka ya kisheria ya mahakama. There will be an inquiry.

Ninaamini mauaji ya watu yaliyofanyika Zanzibar yanapaswa kuchukuliwa hatua.

Hizi siasa za kilevi za kuua watu kiholela, kuwatesa na kuwatisha kwa kutumia jeshi, HAZIKUBALIKI.

Jeshi sio chombo cha kufanyia uharamia na ubedui.

Waliohusika kutuma jeshi likatandike watu risasi wanapaswa kushughulikiwa on individual capacity.

Ninaamini ICC ni chombo makini. Kitachukua hatua zinazowezekana.

Good luck!
 
Mpinzani yupi aliuliwa, ukiambiwa utaje jina unaweza kumtaja. Mbona hamsemi viongozi na wanachama wa CCM waliokufa, Juzi Kuna sijui diwani hapo kibaha kachomewa Nyumba akiwa ndani na wajukuu zake. Na hapa ndipo mnashindwa kuelewa na kuonekana mazwazwa. Kwani kabla ya Uchaguzi watu walikuwa hawauani, watu walikuwa hawafi, kwahiyo ICC ije ishugulikie waliomuua Mwenyekiti wa UV CCM Iringa au huyo diwani aliyechomwa Moto. Ndio akili zenu zimefika hapo.
Hayo matukio Kama yapo ni uhalifu Kama uhalifu mwingine na unadhughulikiwa kwa mjibu wa Taratibu zilizopo.
USA kila siku watu wanabutuliwa Risasi tena wakati mwingine na Askari! Umeskia Kuna mtu amepelekwa ICC. Kwahiyo watu wakiuana, watu wakijeruhina basi twende ICC. Umesema huko Singida wapo Mahakani. Mimi nadhani uache Mahakama ifanye kazi yake ili haki itendeke!
 
Unaweza kukuta ninyi ndio washauri wa Magufuli.

Mnampa amani sana kwa maandiko kama haya.

Ila mdharau mwiba mguu huota TENDE.

#Propagandanists
 
Bahati mbaya unajibu hoja kwa kukurupuka. Hujaelewa context!

Hapa hatuzunhumzii uwezo wa mahakama katika kuamua baadhi ya kesi hali tunazungumzia uhuru wa mahakama katika ujumla wake.

Mahakama inayoambiwa hukumuni haraka wenye kesi za madai ya kodi, mahakama inayopewa hukumu iliyoandaliwa na RC kama ilivyotokea kwa Sugu kule Mbeya au inayoamriwa imfunge Mbowe, mahakama ambayo Jaji mkuu anashiriki vikao vya siri vya CCM, mahakama ambayo kiongozi wake mkuu yaani Jaji mkuu anayepokea maelekezo toka jwa Rais na Katibu wa CCM, mahakama ambayo imepewa uhuru wa kuhukumu kesi za wizi wa kuku, mashauri ya viwanja lakini ikanyimwa uhuru wa kuamua kesi za wanasiasa na wanaodaiwa ni wahujumu uchumi, hakuna namna yoyote ya mahakama hiyo kuitwa ni mahakama huru.

Na Rais Magufuli anajivunia kuweza kuiweka mahakama na Bunge mfukoni mwake. Naye kwa kauki yake aluwahi kusema, muhimili wake wa Serikali una mizizi iliyojichimbia, akimaanisha kuwa mahakama na Bunge ni matawi, yeye ana uwezo wa kuyafanya atakavyo. Na amedhihirisha hilo kwa kauli na vitendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo kesi za msigwa na mbowe ndizo zinazotumika kupima weledi na uhuru wa mahakama katika mwelekeo wa Kisiasa.

Mahakama sio chombo cha kuamua kesi za nyanya na vitunguu pekee. Ni chombo ambacho wakati mwingine kinapaswa kuamua mambo muhimu yanayogusa nyoyo za hao akina magufuli.

Constitutional petitions, declaratory orders etc.

Ukiona kila kesi magufuli anashinda, tena anashinda katika mazingira tatanishi, unaona hapa mahakama imegeuka kuwa KANGAROO COURT ama mahakama ya kimagufuli magufuli.

We do not need magufulified courts.

Tunahitaji mahakama makini zenye MAMLAKA YASIYOCHEZEWA na wanasiasa wasiojua hata kuzungumza Kiswahili kama hao akina magufuli.

The court is not a political arena for propaganda and abdacadabras.

Mahakama sio mahala pa kufanya ujanja ujanja na MAIGIZO ya kimagufuli.

Kwa msingi huo, ICC ni chombo kinachoaminika zaidi machoni mwa wengi katika mazingira haya ya kimagufuli.
 
Wewe nadhani huelewi hata kinachojadiliwa. Tuliza akili.

Hapa tunaongelea mauaji ya watu yenye uhusiano na mchakato wa uchaguzi au shughuli za siasa.

Unafahamu chochote kuhusu mauaji yaliyofanywa na serikali kwa wananchi wake kule Zanzibar? Hatuongelei mtu mmoja au wawili au hata watano waliouawa na majambazi bali wananchi waliouawa na Serikali kwa sababu ya misimamo yao ya kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hajui chochote.
 
Kweli King'eng'e kina wenyewe yaani mimi ni namba moja ambaye nilielewa tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…