Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Ni kweli mkuu,Viti maalum vufutwe tu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Nani kakwambia wapo upinzani? Low thinking
 
Pia waondoe na wabunge wa kutoka jimbo la ikulu pia itapendeza

In God we Trust
Wabunge wa chato na kolomije watapewa wizara ya Ulinzi, Utawala bora, mambo ya ndani, fedha , madini na ujenzi wizara zingine watapewa kabla zingine
 
Kumbe serikali ina kamati kuu na halmashauri kuu (NEC)?
 
Hapo watakaopungua wengi watatoka upande ule.....
 
Hili mimi naliunga mkono kabisa

1. Kwanza futa viti maalum havina msaada wowote zaidi ya kuwapa individuals ulaji

2. Unganisha hayo majimbo, tena inafaa Jimbo liwe na ukubwa wa Wilaya nzima

Nchi hii masikini sana, Ulaji katika siasa inabidi upunguzwe na badala yake pesa zipelekwe kwenye maendeleo

Katika mambo machache ya maana ambayo JPM atakuwa amefanya katika utawala wake ni hili.

Hii nchi siyo kubwa kivile kiasi cha kuhitaji wabunge wote 300+, wote wa nini hao, wameongeza tija gani zaidi ya kumbebesha zigo mlipa kodi?
 
Shida ya kumpa uongozi asiejua uongozi ni nini ,tutashuhudia vitimbi vya kila aina visivyokuwa na kichwa wala miguu hivi huyu mzee hana hata work plan ,vipaumbele kwenye uongozi wake au anajiendea tu .Leo hili kesho hili shaghala baghala ,wapongezaji juhudi wajiandae kuandamana .
 
kwanini jiwe anateseka hivyo? ana wabunge wengi hivyo apeleke mswada wa kufuta vyama vingi ili tupumue
 
Jiwe akifanya hayo,hata akitawala milele poa tu,apunguze idadi ya mikoa,wilaya,wabunge ni wengi sana,hakuna uhusiano wa maendeleo na kuwa na mbunge,
Wabunge wawe 100 tu,wizara zipungue idadi,vyeo na idara zipungue katika utumishi wa umma,taasisi za umma zipungue,kuna haja gani kuwa na Tarura,wakati Tanroads ipo,?
Hayo mapesa,yapelekwe kukopesha vijana wasome elimu ya juu,wawezeshwe waende huko duniani wakatengeneze pesa,kama hakuna bidhaa za kuuza nje,basi tuuze wasomi wetu,wahandisi,madakitari,tuwe kama India,wamejaa kibao US,kwenye sekta za IT,na udakitali.
Wabunge 75 wanatosha,wilaya zipungue,Zamani dar ilikuwa,Kinondoni,Ilala,na Temeke,Leo tunaambiwa kuna Ubungo na Kibamba!!!kilichoongezeka hapa ni idadi ya watu,sio eneo LA kijiografia,sasa kwanini kuongeza gharama ya uendeshaji,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukubwa wa baraza la mawaziri ni eneo lingine muhimu sana kuliangalia. Inafaa kuwa na serikali ndogo yenye mawaziri wasiozidi 20 ili kubana matumizi na kuongeza tija
Usipende kuingilia mambo ya wakubwa, juzi tu imeanzishwa wizara mpyaaa kapewa yule mama wa mavito ya thamani. Hakuna kumuingilia alishasema.
 
Mimi naona ni bora hata tusipokuwa na Bunge kabisa, kusiwe na vyama vya siasa tuache iwe jeshi la mtu mmoja.
 
Nani alikuja na wazo la kujaza hao wabunge? je alikuwa ni sababu zipi? hizo kwa nini sababu hizo zikose tija kwa sasa?
 
Ukubwa wa baraza la mawaziri ni eneo lingine muhimu sana kuliangalia. Inafaa kuwa na serikali ndogo yenye mawaziri wasiozidi 20 ili kubana matumizi na kuongeza tija
Well,...eneo jingine ni kupunguza magari ya thamani kubwa kwa viongozi kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa, hayo magari kuyamaintain ni gharama kubwa mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…