Jugado
JF-Expert Member
- Oct 28, 2021
- 1,446
- 3,184
Habari.
Miaka ya wazazi wetu mwanamke akiolewa ni kuzaa mpaka kizazi kiishe. Huku watoto wakipishana miaka miwili.
Ndiyo maana si ajabu kuona familia zenye watoto nane, tisa mpaka kumi. Lakini Karne hii mambo ni tofauti. Wanawake hawataki kuzaa watoto wengi. Utasikia wawili wanatosha. Akienda sana watatu au wanne.
Swali langu kwa wana JF nani wakuamua idadi ya watoto? Ikiwa hakuna makubaliano? Mama hataki watoto wengi na baba anataka! Naelewa kile wanachokipitia wamama wakati wa kubeba mimba, kunyonyesha na hata malezi. Lakini ndivyo ilivyo. Naelewa hivyo kwani mimi na mke wangu tuna watoto watatu.
Kilichonifanya kuandika huu uzi ni mke wangu kupata mimba ambayo hatukuitarajia/hatukupanga. Hivyo kuleta gumzo japo hatimaye Mungu mkubwa kakubali kuzaa kwa sharti lazima afunge kizazi baada ya kujifungua! Kwa upande wangu naona nahitaji watoto zaidi. Sipo tayari wife afunge kizazi. Hii imekaaje? Je, ni kweli watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu?
Au ni maamuzi ya wanandoa wote au mmoja wao. Nawasilisha kwa michango ya jumla kuhusu mada na specifically kuhusu mimi na wife tutatoboaje?