Idadi ya watoto ndani ya ndoa: Nani huamua?

Idadi ya watoto ndani ya ndoa: Nani huamua?

  • Je ni hatua zipi mlichukua kabla?
  • Je mlifika kituo cha afya kupata ushauri njia salama za uzazi wa mpango?
Kuhesabu siku! Ila ndo hivyo kufumba na kufumbua kitu tayari. Ila imepita miaka mitatu kwa mtindo huo huo.
 
Ukipenda mwanamke mwingine zaa nae upendavyo
Ila hakikisha we sio baba suruali

U need to provide na sio kifedha tu...muda.,malezi nk
Sipendi purukushani za kulea huku na kule. Niliazaa mtoto mmoja tu wakati ule sijaoa. Sasa hivi mke wangu kashaanza kumuonea wivu japo hatuishi na huyo mtoto. Nikiongeza wengine naona itakua vita tu.
 
Kama una hali nzuri, unazaa tu ila sikiliza na mke anasemaje, wakati mwingine ni Jambo la kupanga mapema kabisa.
Hali ni ya wastani naweza kuhudumia vizuri watoto sita. Ila sio wale baga! Ni mwendo wa wali maharage, dagaa na sukuma wiki! Nyama jumapili!
 
Mambo yote mnapanga wakati wa uchumba. Ya mwanaume na ya mwanamke unajumlisha kisha gawa kwa mbili. Jibu ni wastani, basi enendeni mkaishi kulingana na huo wastani wa makubaliano. Hapo hakuna malalamiko na mtaishi kwa raha. Nawabariki kwa jina la aliye juu, Amen!
 
Sipendi purukushani za kulea huku na kule. Niliazaa mtoto mmoja tu wakati ule sijaoa. Sasa hivi mke wangu kashaanza kumuonea wivu japo hatuishi na huyo mtoto. Nikiongeza wengine naona itakua vita tu.
Ss utaingia kwny vita isiyo ya lazima na mkeo

Unapenda watoto wengi mama 2/3 sio mbaya
 
watu mnazaa....duuh...

una watoto watatu ila bado hawakutoshi.... mtoto mmoja anatosha wa pili labda ukipitiwa.

binafsi nina mmoja na hapati kaka wala dada.
Mke wako atakuongezea Mtoto wa nyongeza wala usijali!!!
 
Watoto wengi wana raha uzeeni. Imagine una mtoto mmoja afu umezeeka. Kuhusu wasiohudumia ni kitu kibaya sana. Mwanaume sharti ahudumie mke na watoto.
Kuna watu wana watoto wengi af walio na maisha byee ni mmoja au wawili tu, na kuna wengine hakuna mwenye maisha wote apeche alolo na kuna wenye mtoto mmoja na yuko vizuri kweli..anafanya majukumu vizuri kama mtoto wa hiyo familia.. mkuu usikariri haloo. Naongea na mifano kibwena ninayo.
 
Hata ukizaa 7 wanaweza wasiwe mashoga, na wajukuu wasilete pia, kwan nan kakuambia mashoga hawazalishi?
wanaweza kuuana kwa tamaa ya mali na wakawauwa wazazi pia. Mungu atunusuru.

Kuna baba mmoja alibarikiwa mali sana na akabarikiwa watoto 4, wakiumw wakawa wahuni tu hawataki shule , hawataki kazi kwasababu mzee ana pesa.

Baba yao aliwafukuza watoto wa kiume akabaki na wakike, miaka ilivyoenda mzee akafariki, wale wa kiume wakarudi wakataka kuuza mali zote, dada yao mkubwa alikuwa ameolewa Arusha, mdogo ndio alikuwa anaishi na baba yao.

Walivyoona dogo kawa mbishi wakapanga njama wakamuua mdogo wako, long story short, walikamatwa wapo jeal , kabaki dada yao pekee.

Mungu ndio mgawa riziki ikiwemo riziki ya watoto.
 
Kama ni maskini bora usizae mana unakuja kuwatesa tu hao watoto
 
Back
Top Bottom