Idadi ya watoto ndani ya ndoa: Nani huamua?

Idadi ya watoto ndani ya ndoa: Nani huamua?

Wengi hili huwa hatulijadili..........idadi ya watoto ni muhimu sana kujulikana mapema,ili mipango ya Elimu na mambo mengine......Kwa maisha ya sasa watoto watatu wanatosha........tusitake wanetu nawao wapite maisha tuliyopita sisi
 
Ni sahihi lakini Mimi kama Mwanamke.... Uzazi za sasa ni changamoto sana, mambo ni mengi. Mimi nipo tayari kuzaa watoto wawili tu. Mume akitaka kuongeza akaongeze .... Hakuna namna. Kwa sasa unawazaje kuzaa watoro tisa??
Haina shida as long as umeruhusu nikatafute huko nje

Tisa ni too much .. watoto wawili ? are you serious sema wewe ndio huwezi wenzako wanaweza
 
Kwanza angalia afya ya mkeo, pili jali na kumsaidia kuangalia watoto, tatu mpe upendo mapenzi mahaba mjali thamini sana pia watoto wake mtoe out mpe zawadi akikuletea ndugu zao warithi wa jina lako.
Malezo magumu sana kwa wazazi hasa wanawake wanavumilia sana wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
Wanaume wengi hawawapi thamani wake zao wanawaza watoto wengi wanachojua wao mke ale alale kama vile ulimkuta jalalani.
Wow!
 
Kama una hali nzuri, unazaa tu ila sikiliza na mke anasemaje, wakati mwingine ni Jambo la kupanga mapema kabisa.
 
Watoto kuwa nao uwe na mipango mizuri tu kiuchumi. Vinginevyo ni hawa bodaboda na wauza nguchiro tunawaona humu njiani.
Binafsi nnao wa5.
Kati yao kiukweli ni wa2 tu nilizalisha kwa kudhamiria pamoja na mama zao.
Wa3 waliobaki ni mimba zisizotarajiwa,kutegesheana,na kubambikiana.
Watoto wapo ni wakwangu haikwepeki.mama zao vimekua vizee haswa watoto ndo hao wanashamiri na kuonyesha baba yao nani.
Kizazi chetu tumezaliwa wa4 full stop.
Watajua wazazi walichofanya, ila bibi ukoo upande wa mama alizaa 10,
Bibi ukoo upande wa baba aligonga 6.
Hao wote walikua mama wa nyumbani.
Na walikua ngangari mpk wanakufa.
Kwasasa wanawake tunaoa wanataka wachakarike watengeneze vyao utamzalisha vipi watoto 10?
Hiyo sio mashine,watoto 10+ halafu ukute lijitu anazaa nalo km ww mleta mada unamuona mwanamke ni kumtumia tu.
Unataka watoto kagonge nje huko km we mwamba.
Hao wa3 wanatosha sana wape huduma na mahitaji ya muhimu bila kupungua na mpe afya ya kutosha mzazi mwenzio arudishe nuru yake.
Nna wa5 na kila mmoja na mama yake.
So i talk from experience

Eti kubambikiana, ni kwamba amekubambikia mtoto au ni vipi?
 
hapana.... Tumezaliwa watatu ila huwa natamani saana ningekuwa mwenyewe kwasababu....tumeishi pamoja tu enzi za utoto tulipokua tunaonana Mara moja kwa mwaka.

shida yote ya nini?
Husikii raha mnavyokutana hiyo mara moja kwa mwaka na nduguzo.
 
Nadhani ni makubaliano ya wote wawili wakati wa uchumba. Japo wakati mwingine mnaweza badilisha hayo makubaliano.
 
Habari.

Miaka ya wazazi wetu mwanamke akiolewa ni kuzaa mpaka kizazi kiishe. Huku watoto wakipishana miaka miwili.

Ndiyo maana si ajabu kuona familia zenye watoto nane, tisa mpaka kumi. Lakini Karne hii mambo ni tofauti. Wanawake hawataki kuzaa watoto wengi. Utasikia wawili wanatosha. Akienda sana watatu au wanne.

Swali langu kwa wana JF nani wakuamua idadi ya watoto? Ikiwa hakuna makubaliano? Mama hataki watoto wengi na baba anataka! Naelewa kile wanachokipitia wamama wakati wa kubeba mimba, kunyonyesha na hata malezi. Lakini ndivyo ilivyo. Naelewa hivyo kwani mimi na mke wangu tuna watoto watatu.

Kilichonifanya kuandika huu uzi ni mke wangu kupata mimba ambayo hatukuitarajia/hatukupanga. Hivyo kuleta gumzo japo hatimaye Mungu mkubwa kakubali kuzaa kwa sharti lazima afunge kizazi baada ya kujifungua! Kwa upande wangu naona nahitaji watoto zaidi. Sipo tayari wife afunge kizazi. Hii imekaaje? Je, ni kweli watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu?

Au ni maamuzi ya wanandoa wote au mmoja wao. Nawasilisha kwa michango ya jumla kuhusu mada na specifically kuhusu mimi na wife tutatoboaje?
Ukipenda mwanamke mwingine zaa nae upendavyo
Ila hakikisha we sio baba suruali

U need to provide na sio kifedha tu...muda.,malezi nk
 
Kilichonifanya kuandika huu uzi ni mke wangu kupata mimba ambayo hatukuitarajia/hatukupanga. Hivyo kuleta gumzo japo hatimaye Mungu mkubwa kakubali kuzaa kwa sharti lazima afunge kizazi baada ya kujifungua! Kwa upande wangu naona nahitaji watoto zaidi. Sipo tayari wife afunge kizazi. Hii imekaaje? Je, ni kweli watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu?
  • Je ni hatua zipi mlichukua kabla?
  • Je mlifika kituo cha afya kupata ushauri njia salama za uzazi wa mpango?
 
Ni sahihi lakini Mimi kama Mwanamke.... Uzazi za sasa ni changamoto sana, mambo ni mengi. Mimi nipo tayari kuzaa watoto wawili tu. Mume akitaka kuongeza akaongeze .... Hakuna namna. Kwa sasa unawazaje kuzaa watoro tisa??
Wanaume wabinafsi sana
Hawajui kubeba mimba
Wala labour
Wala operation
Wala kunyonyesha
Wala kuhudumia mtoto
Mix wasiohudumia ipasavyo

Inshort they dont do the hard work
mlezi ni mama
Ndo mana wababa wanachukulia poa tu hili suala
 
Au ni maamuzi ya wanandoa wote au mmoja wao.
Daima ni maamuzi ya wanandoa wote, Na iwapo mkeo hayuko tayari basi 👇
- Iwapo dini inaruhusu ongeza mke wa pili, watatu, hata wa nne utabarikiwa na kupata watoto idadi ile unayohitaji.
---
Kuna Mzee hapa Tanzania ana wake 16 na watoto idadi kubwa, Tazama video
 
watu mnazaa....duuh...

una watoto watatu ila bado hawakutoshi.... mtoto mmoja anatosha wa pili labda ukipitiwa.

binafsi nina mmoja na hapati kaka wala dada.
Mmoja hapana. Yani unakuwa kimachale machale sana. Ni kama ume bet under 1.5 halafu tayari timu ina goli dakika ya 10. Hizo dakika 80 unazoishi ni sawa sawa na maisha unayoishi na huyo mtoto mmoja uliye naye
 
Wanaume wabinafsi sana
Hawajui kubeba mimba
Wala labour
Wala operation
Wala kunyonyesha
Wala kuhudumia mtoto
Mix wasiohudumia ipasavyo

Inshort they dont do the hard work
mlezi ni mama
Ndo mana wababa wanachukulia poa tu hili suala
"Utazaa kwa uchungu" ulidhani Muumba alikuwa anaongea kimasihara? Imagine Muumba alikutandika kofi la aina hiyo! Aisee pambana tu siku ukirudi kwake nenda kamuhoji alidhamiria nini?
 
"Utazaa kwa uchungu" ulidhani Muumba alikuwa anaongea kimasihara? Imagine Muumba alikutandika kofi la aina hiyo! Aisee pambana tu siku ukirudi kwake nenda kamuhoji alidhamiria nini?
Sio poa ujue

Mana mwanamke sikuhz unaweza diriki ukae tu home all ur life usile kwa jasho?
 
Maisha ya sasa ni magumu ivyo basi kila mtu azae kuendana na kipato chake, wapo watu watakuja kusema mara oh mungu kasema tukaongezeke but kesho na kesho kutwa ukija omba msaada wa ela japo ya ada ya mtoto utasikia anakwambia nani alikwambia uzae watoto wengi. Binafsi ntazaa ambao nitakuwa na uwezo wa kuwalea kwa sasa ninao wawili.
 
Wanaume wabinafsi sana
Hawajui kubeba mimba
Wala labour
Wala operation
Wala kunyonyesha
Wala kuhudumia mtoto
Mix wasiohudumia ipasavyo

Inshort they dont do the hard work
mlezi ni mama
Ndo mana wababa wanachukulia poa tu hili suala
Watoto wengi wana raha uzeeni. Imagine una mtoto mmoja afu umezeeka. Kuhusu wasiohudumia ni kitu kibaya sana. Mwanaume sharti ahudumie mke na watoto.
 
Back
Top Bottom