Idadi ya watoto ndani ya ndoa: Nani huamua?

Mkuu hii point yako ni ya makini sana umenena vema mkuu, unaongeza mtoto mwingine kutokana na uwezo wa mfuko kama ni mmoja ndo una uwezo wa kumlea basi ni huyo huyo, ili kutowatesa watoto,
 
Uko serious? Hebu ongeza mwingine apate ndugu/rafiki wa kukua nae hata kesho mkiondoka ajue anaendugu yake wa damu itamtolea upweke.
Watoto wa ma uncle na aunties wapo lakini kuna raha ya kua na kaka/dada wa baba/mama mmoja.
hapana.... Tumezaliwa watatu ila huwa natamani saana ningekuwa mwenyewe kwasababu....tumeishi pamoja tu enzi za utoto tulipokua tunaonana Mara moja kwa mwaka.

shida yote ya nini?
 
watu mnazaa....duuh...

una watoto watatu ila bado hawakutoshi.... mtoto mmoja anatosha wa pili labda ukipitiwa.

binafsi nina mmoja na hapati kaka wala dada.
Muongezee wawili tyuuh.
 
Wavivu ndo huzaa watoto wachache,hebu fikiria umezaa watoto 2,mmoja akawa shoga mwingine nun vipi utapata wajukuu?”zaeni mkaongezeke na kuijaza dunia “ni kauli ya Muumba mwenyewe
Hata ukizaa 7 wanaweza wasiwe mashoga, na wajukuu wasilete pia, kwan nan kakuambia mashoga hawazalishi?
 
Nimekuelewa vilivyo mkuu, ILA siku utakayotambua kuwa kama Botswana wananunua 1Lt of diesel kwa 17P,na sisi tunanunua kwa zaidi ya 2500tsh na SIO 18TSH,then tutakua in the level to discuss this,kwa sasa naona itakua vigumu mno maana umeona ni Sawa kwa 17 na 2996,kwangu naona ni tofauti kubwa mno,2996P=2996ths, sio 17=2996
 
Mkuu nikuulize,
Mishahara ya Botswana ipo kwenye range gani kwenye Pula? Ukinijibu hili tutaenda sawa.
 
Mkuu nikuulize,
Mishahara ya Botswana ipo kwenye range gani kwenye Pula? Ukinijibu hili tutaenda sawa.
Sorry mkuu nimechua muda kujibu, mishahara kwa pula ndani ya Botswana 🇧🇼 ipo kwenye range ya 12,000BWP hadi 60,000BWP,thanks
 
Kwanza angalia afya ya mkeo, pili jali na kumsaidia kuangalia watoto, tatu mpe upendo mapenzi mahaba mjali thamini sana pia watoto wake mtoe out mpe zawadi akikuletea ndugu zao warithi wa jina lako.
Malezo magumu sana kwa wazazi hasa wanawake wanavumilia sana wakati wa ujauzito na kunyonyesha.
Wanaume wengi hawawapi thamani wake zao wanawaza watoto wengi wanachojua wao mke ale alale kama vile ulimkuta jalalani.
 
Mimi napenda watot wengi Saba hivi japo sijaanza kuwapata hila napenda wengi sababu ntakuwa nalima hvyo uwezo wa kuwahudumia nitakuwa nao
 
Mwanaume ndio unaamua
We ndio kichwa bwana usikubali kupangiwa
Ni sahihi lakini Mimi kama Mwanamke.... Uzazi za sasa ni changamoto sana, mambo ni mengi. Mimi nipo tayari kuzaa watoto wawili tu. Mume akitaka kuongeza akaongeze .... Hakuna namna. Kwa sasa unawazaje kuzaa watoro tisa??
 
Kama wewe ni mwanaume uliyepiga goti wakati unamvalisha pete ya uchumba mkeo basi Mwanamke ndio ataamua kila kitu ndani ya nyumba yenu
 
Ni sahihi lakini Mimi kama Mwanamke.... Uzazi za sasa ni changamoto sana, mambo ni mengi. Mimi nipo tayari kuzaa watoto wawili tu. Mume akitaka kuongeza akaongeze .... Hakuna namna. Kwa sasa unawazaje kuzaa watoro tisa??
Tisa wengi duuh.....
 
Uchumi wako, pamoja nam mengine ndio unaamua idadi ya watoto. Siku hizi hata maji ya kunywa yananunuliwa so uchumi ni factor ya kwanza kabla mengine hayajaja. Katne ya kuzaa sita-kumi imeisha tayari
 
Idadi ya watoto inategemea na uwezo wa familia japo mungu ndo anayepanga ila angalia kama unaweza kuwapa huduma wote bila kumtegemea mtu basi we fyatua tu ila kama tia maji tia maji ndo hivyo ujipange.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…