Idara ya Uhamiaji sasa kuwa Jeshi kamili na litawajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Idara ya Uhamiaji sasa kuwa Jeshi kamili na litawajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Sasa itakuwa ngumu kwa wanasiasa wa upinzani kutoka au kuingia nchini hata kama wametimiza vigezo na masharti vya visa!!!NAMUONA TUNDU LISU NA LEMA WAKIZUIWA KUINGIA NCHINI KWA AMRI KUTOKA JUU NA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI WA 2025!!!
 
Pia ina maanisha kuna tishio kubwa la kiusalama nchini na Hamza kawafumbua macho huenda kuna kina Hamza wengi watakuja kulipa kisasi kwa kuondokewa na Hamza wao!!!!
 
Bunge limefanya mabadiliko madogo ya sheria ya idara ya Uhamiaji ambapo sasa litakuwa ni jeshi kamili litakalowajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene amesema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza nidhamu kwa idara ya Uhamiaji ambapo sasa litajiendesha kwa Amri.

Source: ITV habari
itapendeza saaaaana
 
Kwahiyo likiwa jeshi alafu? Uliwahi kusikia Magereza wanaendesha kesi zao wenyewe zaidi? Yaani wakamate, wapeleleze kesi n.k?

Issue ya kukamata kila mtu ana uwezo wa kukamata, hata raia wa kawaida amepewa power ya kukamata mhalifu
Hata Polisi kuendesha kesi ni kwasababu DPP hajawa na watu wa kutosha tu
 
Sasa wahamishiwe mipakani wakalinde mipaka ya nchi, ofisi zao ziwe kwenye border posts zote zilizopo, kazi ya kutoa pasi za kusafiria wawaachie TAMISEMI na NIDA.
 
Ni baada ya ile kauli za makamanda, zerro kuwa raisi asiwe na "double standard" na yule mpare kuwa aliyesema Baba atabaki kuwa Baba na baba hasemwi hadharani kwani kuna namna yake ya kumsema... kwa hayo tu Raisi ashajua kuwa kuna watu wanamdharau na pia wanademka na wamepandisha mabega so polisi wote ni kama waasi.. hivyo Raisi hana budi kutengeneza Jeshi lingine aliveshe silaha ili kuleta heshima maana zile silaha zinawaletea jeuri waliotangulia. Even vyama vya Siasa navyo vingekuwa na majeshi yao upumbavu wa polis tusingekuwa tunausikia na nchi ingeongoza kwa amani na sifa dunia nzima
 
Kwa miaka yote hii ambapo wamekuwa wakiliita Jeshi la Uhamiaji, na mabadiliko ya vyeo waliyofanya ilikuwa ni gelesha?

Kwani wakati wa Mkurugenzi Kihomano si ilikuwa idara na alipokuja Kamishina Makakala likawa ni jeshi...
 
Tunalipongeza jeshi la uhamiaji. Ila ni wakati muafaka sasa wa kutoonea watu kwa vigezo sio raia, au kuwasumbua kupata mahitaji ya lazima kutoka kwao, kwa sababu zisizo na mashiko. Ili lipate heshima kama JWTZ, lazima liende kwa weledi na nidhamu iliyotukuka.
Kazi wanayofanya sio ya kitoto wala ya lelemama. Inataka wawe zaidi ya kundi la watu wasiojua wanafanya nini. Tuko pamoja nanyi.
 
Kama jeshi la polisi ambalo linawajibika kwa Rais halina nidhamu unadhani hiyo idara ya uhamiaji kwa kufanywa jeshi kamili na kuwajibika kwa Rais ndiyo itaongeza nidhamu!?
Naanza kuwa na wasiwasi kuna siku haya majeshi yatatwangana risasi. Tumekwisha ona JWTZ na polisi kurushiana risasi maslahi yao yanapogongana sembuse hawa Uhamiaji na polisi!
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Naanza kuwa na wasiwasi kuna siku haya majeshi yatatwangana risasi. Timekwisha ona JWTZ na polisi kurushiana risasi maslahi yao yanapogongana sembuse hawa Uhamiaji na polisi!
hizo conflict zipo ila ni ndogo sana sana. na kuna taratibu za kijeshi za kumaliza hizo kesi. ndio maana huzisikii sana. wenyewe kwa wenyewe wana taratib za kumaliza hizo ishu
 
Kwahiyo likiwa jeshi alafu? Uliwahi kusikia Magereza wanaendesha kesi zao wenyewe zaidi? Yaani wakamate, wapeleleze kesi n.k?

Issue ya kukamata kila mtu ana uwezo wa kukamata, hata raia wa kawaida amepewa power ya kukamata mhalifu
TAKUKURU wanapeleleza na kushitaki wenyewe
 
hizo conflict zipo ila ni ndogo sana sana. na kuna taratibu za kijeshi za kumaliza hizo kesi. ndio maana huzisikii sana. wenyewe kwa wenyewe wana taratib za kumaliza hizo ishu
Sasa ndiyo zinaongezwa!
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene amesema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza nidhamu kwa idara ya Uhamiaji ambapo sasa litajiendesha kwa Amri.

Source: ITV habari

Litajiendesha kwa amri kwani hapo mwanzo lilikuwa halina amri? Au lizidi kupewa amri ili kuhujumu wapinzani juu ya uraia wao?

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957][/QUOTE]Huyu naye ni waziri hewa
 
Back
Top Bottom