Idara ya Uhamiaji sasa kuwa Jeshi kamili na litawajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Idara ya Uhamiaji sasa kuwa Jeshi kamili na litawajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Bunge limefanya mabadiliko madogo ya sheria ya idara ya Uhamiaji ambapo sasa litakuwa ni jeshi kamili litakalowajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Waziri wa Mambo ya Ndani mh Simbachawene amesema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza nidhamu kwa Idara ya Uhamiaji ambapo sasa litajiendesha kwa Amri.

Chanzo: ITV habari
Swali la msingi ni kwanini iwe hivyo ??
 
Bunge limefanya mabadiliko madogo ya sheria ya idara ya Uhamiaji ambapo sasa litakuwa ni jeshi kamili litakalowajibika moja kwa moja kwa Amiri Jeshi Mkuu

Waziri wa Mambo ya Ndani mh Simbachawene amesema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza nidhamu kwa Idara ya Uhamiaji ambapo sasa litajiendesha kwa Amri.

Chanzo: ITV habari
Hayo ni maandalizi ya kujidhihirisha mpinga kristo, mifumo inasukwa upya ku centralize information kupitia njia za kielectronik.......mifumo ya malipo, kusajili watu nk. na kuongeza command zaidi kuweza kuthibiti watu, time will tell......
 
Idara ya Uhamiaji au Jeshi la Uhamiaji ndo jicho la Taifa hasa kwa wageni na Raia wa nchi hii, kwa unyeti wake inapaswa iwe section ndani ya usalama wa Taifa au ipelekwe wizara ya ulinzi.
 
kila siku TISS unajua hata bajeti ya hao ama unajua imeajiri vijana wangapi? acha udwazi.
 
1642020885071.png
PAMOJA!
 
Idara ya Uhamiaji au Jeshi la Uhamiaji ndo jicho la Taifa hasa kwa wageni na Raia wa nchi hii, kwa unyeti wake inapaswa iwe section ndani ya usalama wa Taifa au ipelekwe wizara ya ulinzi.
... duniani kote hiyo ndio setup; Uhamiaji wako Mambo ya Ndani (Internal Affairs). Dhima kuu ya Mambo ya Ndani ni usalama wa raia na ili hilo litekelezeke ni lazima kuwatambua raia wote (including wageni waliopo nchini) ndio maana ukiacha Uhamiaji, NIDA pia wapo Mambo ya Ndani. Uhamiaji (na Mambo ya Ndani kwa ujumla wake) wanashughulika na wageni wanaoingia kiraia; wale wanaojaribu kuingia "wamevaa kombati" hiyo ni kazi ya JWTZ.
 
Alafu hao NIDA Wana njaa balaa ,Nipo mpakani Mwa Tanzania na Kanchi fulani huwez Amini wanagawa vitamburisho vya uraia kwa raia wa nchi jiran Tena kwa elfu hamsini tu.
Hii nchi ya hovyo Sana ,watu wanapata wapi ujasiri wa kugawa nida kwa raia wa kigeni Tena hao raia wanaishi bila hata vibali yaan hii nchi hovyo sana
 
Idara ya Uhamiaji au Jeshi la Uhamiaji ndo jicho la Taifa hasa kwa wageni na Raia wa nchi hii, kwa unyeti wake inapaswa iwe section ndani ya usalama wa Taifa au ipelekwe wizara ya ulinzi.
Kwani hao usalama wa Taifa wapo wizara gani na ufanyaji wao kazi una endana na taratibu za utendaji za uhamiaji? Wanaposema ulinzi wana maana mipaka so automatically ni JWTZ na kamandi zake swali uhamiaji ni jeshi au idara?.....nyongeza ufanisi wa chombo hautegemei wizara
 
Back
Top Bottom