Hivi bila mikataba ya kubadilishana taarifa (Intelligence Sharing Agreements) na mataifa ya kizungu (Anglo-Saxons States/5 Intelligence Eyes ) Israel inaweza kuwa na nguvu hii-hii kijeshi na kijasusi ??? Hebu tuwe wakweli kidogo.
Pia, kila mwaka Israel anapewa msaada wa kijeshi kutoka Marekani, dola za Kimarekani bilioni 3.3, ambazo ni sawa na trilioni 7 za Kitanzania. Mahela yote haya ya kununulia vifaa, kufanya tafiti na kufanyia oparesheni za kijeshi na kijasusi, unadhani watakuwa wa kawaida kweli ???
Leo hii hata sisi Tanzania tupewe trilioni 7 kama bajeti ya jeshi kila mwaka, unadhani TPDF itakuwa ya mchezo mchezo ??? (Japo nina wasiwasi sisi Tanzania tukipewa msaada kama huu, lazima tutaiba tu)