Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Acha kutetea ujinga! Magufuli hata mimi sielewani nae kwa siasa zake! Kama tunapenda haki tuache chuki, tusiwe na upendeleo na tuwe na utu na tuheshimu watu hata kama tunatofautiana nao kimtazamo.kwa hiyo kosa kuifurahi picha ya hao wazazi?does it sense. we mzazi wako nikimcheka picha yake utanifunga?au ndo matumizi ya madaraka?hembu tuambie sasa kavunja sheria ipi hata kama ni sheria za kidkiteta
Alichokifanya Idrisa ni dhihaki! Laiti kama angeliiweka picha ya mzazi wake halafu anaicheka unafikiri jamii ingelimpokeaje? Ingelimwambia hana nidhamu. Hata kama angeliiweka picha ya mzee mwenye umri kama wa Magu halafu anaicheka kwa muonekano unafikiri jamii ingelimchukuliaje? Ingelimwambia hana adabu! Anadharau watu kwa vile masikini! Huko siyo kuchekesha! Wengine wangelimwambia angelikuwa baba yako anafanyiwa hivyo ungejisikiaje?!
Ila kwa vile anafanyiwa Magu mnaona poa! Tuache unafiki. Angechekwa Mbowe hapo mngesema CCM inamtumia, serikali inaruhusu udhalilishaji wa upinzani na mngesema ingelikuwa ya Magu angelichukuliwa hatua!
Tuache unafiki! Kapanda upepo, muache avune kimbunga.