Kenya 2022 IEBC: William Ruto ameshinda Urais kwa 50.4% dhidi ya 48.8% za Raila Odinga

Kenya 2022 IEBC: William Ruto ameshinda Urais kwa 50.4% dhidi ya 48.8% za Raila Odinga

Kenya 2022 General Election
Wazee wa Katiba Mpya wanasemaje maana nako huko kwa 'wenzetu' Nako kuna madai ya wizi wa kura
Matokeo ambayo hayawezi kusimama yenyewe na kuthibitishwa kimahesabu si matokeo halali ya uchaguzi.
Naona kesho asubuhi milango na vyumba vya mahakama vitavyokuwa busy!

NB: Kuna wajumbe wanne wa IEBC wamejilipua kuwa kilichofanywa na IEBC dakika za mwisho hakiwahusu!
 
Wazee wa Katiba Mpya wanasemaje maana nako huko kwa 'wenzetu' Nako kuna madai ya wizi wa kura
Rais na mteule wake wote wametoswa.

Imewezekana Kenya, Itawezekana Tanzania.

Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi Hoyeeeeeeeee😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀.
 
Kupambana na Ruto sio kwenye majukwaa tuu lakini hata kwa wizi hawamuwezi ingawa najua wizi safari hii hajafanya ila Ruto wakati wa Moi alipachika watu Kenya nzima idara nyeti ili walinde maslahi yake akijua siku moja atagombea urais na anavyoijua Kenya angeweza hujumiwa. Ruto ni Hustler sio mchezo.
Mwizi mwizi sana
 
Takwimu zinaonesha kuwa wakenya wanategemea sana soko la Tanzania kuliko sisi tunavyotegemea soko lao.

Wakiamua hivyo basi wao wataathirika zaidi kuliko sisi.
Aliyeingia kuwa Rais ndiye mpinzani Mkubwa wa biashara ya Nafaka Kati yetu na wao, kipindi kile cha Jpm ndiye aliyekuwa sababu ya kuzuia mahindi yasiingizwe nchini kwao Kwa kuwa alikuwa na mashamba makubwa ya mahindi Congo!

Sasa ndo kashika usukani, piga picha itakuwaje!
 
Kitendo cha kuweka matokeo wazi kila mtu kuyaona ndicho kilichofanya washindwe hata kuyachezea, kwa uhakika Ruto alistahili ushindi
Wengine tulisema Ruto atashinda tukatukanwa lakini sasa imedhihiri , wakenya wanachagua mtu sio chama ndio maana kuna county kama Nairobi seneta ametoka kwa Odinfa na gavana kwa Ruto. Matokeo yako kwenye portal hata mtu akijidanganya kwenda mahakamani hatoboi .

Funzo kubwa: transparent preempts those who always think they can fool mass with false allegations of results rigging.

God bless Dr Ruto to lead Kenya in accordance to your will.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Kenya, Wafula Chebukati amemtangaza William Ruto kuwa mshindi wa kiti cha urais Kenya kwa kupata 50.4% ya kura zote za Urais dhidi ya 48% za Raila Odinga.

Awali katika ukumbi wa Bomas kulitanguliwa na vurugu baada ya sintofahamu ya kuchelewa kwa matokeo huku maafisa wanne wa IEBC ikiripotiwa kutokubaliana na matokeo.

Matokeo ya Urais yalitarajiwa kutangazwa saa 9 alasiri hata hivyo yalichelewa na hatimaye kutangazwa saa 12 jioni.

Matokeo hayo yametangazwa bila uwepo wa mgombea wa Azimio RAILA ODINGA.

WILLIAM RUTO kwa matokeo hayo ndiye Rais mteule wa 5 wa Jamhuri ya Kenya
View attachment 2324663
View attachment 2324665
Raila alichoharibu ni kuwa na urafiki na dictator Jiwe ,
 
Back
Top Bottom