Kenya 2022 IEBC: William Ruto ameshinda Urais kwa 50.4% dhidi ya 48.8% za Raila Odinga

Kenya 2022 IEBC: William Ruto ameshinda Urais kwa 50.4% dhidi ya 48.8% za Raila Odinga

Kenya 2022 General Election
Tume ya Uchaguzi Huru na Mipaka (IEBC) imemtangaza aliyekuwa Naibu Rais, William Ruto (55) kuwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano kwa tiketi ya Chama cha UDA kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 9, 2022

Tume imesema Ruto amepata Kura 7,176,141 sawa na asilimia 50.49 huku akifuatiwa na Raila Odinga kutoka Chama cha Azimio la Umoja

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ametangaza matokeo hayo baada ya siku sita za kuyasubiri tangu siku iliyopigwa kura, Agosti 9, 2022.

Ruto amewashinda wagombea wenzake ambao ni Raila Odinga, mgombea wa Chama cha Agano, David Waihiga ambaye Agosti 14 alitangaza kushindwa, pamoja na Profesa George Wajackoyah wa Chama cha Roots.

William Ruto (UDA)
50.49%
7,176,121 Votes

Raila Odinga (AZIMIO)
48.85%
6,942,930 Votes

George Wajackoyah (RPK)
0.44%
61,969 Votes

David Waihiga (AGANO)
0.23%
31,987 Votes
Hongera sana Ruto na pole sana Raila. Kugombea x5 unaangukia pua, imetosha sasa!
 
Mzee Lee Kinyanjui alisema katika uwindaji pori ukiongozana na mbwa wako kuwa makini. Kwani porini utakuwa pekee yako pamoja na mbwa, mbweha na mbwa mwitu. Sasa hawa wanyama watatu binamu wakiamua kukugeuka wakati upo nao pekee yako utapona ?
Nawe umeanza vitendawili kama Mzee wa Kitendawili?
 
Kinyanganyiro kinahamia supreme court of Kenya. Karua twit-it is not over until it is over. Mahakama inayo siku 14 kusikiza malalamiko na kutoa maamuzi. Iwapo mahakama itaafiki uchaguzi ulikuwa na dosari,uchaguzia wa

marudio muda usiozidi siku 14
Kumpeleka Ruto supreme court ni sawa na kumsukumia chura majini! Mabepari wote wa Kenya wako nyuma ya Ruto!
 
Hongera sana tume ya uchaguzi Kenya kwa kusimama katika misingi, hongera sana wilson mahera chebukati na mwisho hongera saaaaana hustler Bob Ruto.
 
Wakuu nakuja kuwapa habari kamili.

Kama taarifa inavyoeleza pichani, mkongwe na mzoefu wa siasa za Kenya mh Raila Odinga ameangukia tena pua kwa mara nyingine. Huku bwana mdogo aliejifunza siasa juzi mh William Ruto akiibuka mshindi katika uchaguzi uliokuwa na mvutano mkali nchini humo.

Hii imefanya wengi tuamini kuwa siasa haina mwenyewe.
 

Attachments

  • Screenshot_20220815-195943.jpg
    Screenshot_20220815-195943.jpg
    45.2 KB · Views: 2
Sidhani ,siyo kweli. Mpasuko wa IEBC dhahiri ngoma bado mbichi.
Hoja pekee kubwa waliyo nayo (kama ni hoja kweli), ni kwamba eti hawakuwa-previewed matokeo kabla ya kutangazwa. Kwamba walipaswa kwanza kuyajua matokeo ndipo yatangazwe. Nonsense!
 
Wakuu nakuja kuwapa habari kamili.

Kama taarifa inavyoeleza pichani, mkongwe na mzoefu wa siasa za Kenya mh Raila Odinga ameangukia tena pua kwa mara nyingine...
Mbona Raila alisema yuko kwenye serikali, deep state, na kwa wazoefu na manguli wa siasa? Nini kimetokea tena huko? Au ameamua kumwachia mdogo wake?
 
ila uchaguzi ilikuwa wa wazi japo raila sidhani kama atakubali hii ngoma iishe hivihivi
Mwaka 2017 alisema kulikuwepo na VIFARANGA VYA KOMPYUTA kwenye matokeo ya uchaguzi. Ngoja tuone safari hii sijui vitakuwa vifaranga vya ndege yupi?
 
Back
Top Bottom