Ifikapo 2030 hizi nyimbo za kipuuzi za bongo flava zitaiharibu jamii nzima

Unayo haki ya kuzuia kupigwa nyimbo hizo, ulitakiwa umwambie mhudumu wa ndani ya basi badala ya sisi.
 
Unayo haki ya kuzuia kupigwa nyimbo hizo, ulitakiwa umwambie mhudumu wa ndani ya basi badala ya sisi.
Mkuu ningeweza kumuambia lakini niliogopa reaction ya abiria. Kuna baadhi ya aboria wamepinda sana wangenitukana kwa kuwanyima 'burudani'.
 
Moja ya sababu kwa nini sipendi safari za basi ni huo upumbavu, hua wanaona kama vile abiria wote ni wahuni wenzao, ni bora watu wasafiri kibubu kama kwenye treni kuliko kuweka huo upumbavu
 
Hakuna jipya chini ya Jua haya yote unayoyaona yalikuwepo enzi na enzi

Wapi Sodoma na Gomola
Wapi yule kahaba aliyemfuta Yesu vumbi la miguu kwa kutumia machozi.
 
Mkuu ningeweza kumuambia lakini niliogopa reaction ya abiria. Kuna baadhi ya aboria wamepinda sana wangenitukana kwa kuwanyima 'burudani'.
Muite mhudumu kwenye kiti chako kisha mueleze kwa sauti ya kawaida bila kupayuka.
 
Hali ni tete sana, enzi za kina msondo na bendi nyingine za zamani miziki ilikuwa ya kuelimisha na ilipigwa kiutu uzima, siku hizi ni matusi tupu hadi watoto wa chekechea wanaitikia vibwagizo.
 

Kuna siku waliweka wimbo wa Mr Mwanya, aisee ilibidi wautoe. Ulikuwa Kama pono vile. Nikajiuliza BASATA wameruhusuje kitu Kama hiki.
 

Kuna siku tupo kwenye basi wakawa wameweka movie, Sasa movie imekolea yule konda akaitoa na kuweka bongofleva za kijinga. Aliniboa Sana. Kwa masaa Saba tuanaangalia vichupi.
 
Bottom line watasema wanaimba kwaajili ya maokoto. Cha kushangaza wanachoingiza ni kidogo sana hakiendani na athari ya maadili wanayoyaaribu.

Watu wachache wasituaribie vizazi.

Na hiyo ndio sababu. Wanasingizia kuwa watu wanataka nyimbo za hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…