Ignore list on JamiiForums: Maboresho ya mwaka 2020

Ignore list on JamiiForums: Maboresho ya mwaka 2020

Mfano mrahisi tu... Unaweza ukapigwa wimbo clouds wa WCB nikasikiliza nikamaliza ukapigwa wa Alikiba nikabadilisha station....


Je, nimemnyima Alikiba haki yake ya kusikililwa? Simtaki tu na sitaki nyimbo zake...

Kaveli
 
Hii sio kesi mzee baba na hakuna anayehukumiwa hapa.... hii ipo fair kabisa wala haihitaji mijadala mipana ya kisheria.

Ishu ni sitaki kuona jambo fulani kwasababu zangu binafsi...na kutokuona kwangu hilo jambo hakumwathiri mtu mwingine kabisa.

Na ipo hata kwenye maisha ya kawaida tu...kijiweni akija fulani mie najikataa...wala hakuna aliyenyimwa haki yake. Hapa mtaani tu sio sehemu rasmi kama bungeni au mahakamani.

JF sio sehemu 'rasmi' kwa vigezo gani?

-Kaveli-
 
Ingore iondolewe. La sivyo ile slogan ya
Great Thinker
Na
Dare to speak openly na yenyewe iondolewe kabisa
 
Hapana asee , hii sikubaliani nayo,, huko mbele itasababisha watu kuwa waoga kutoa opinion au kuanzisha mada kwa kuogopa kukosolewa . kama hujapenda kitu ukipita kimya kimya inatosha,


Sent
Yaani mtu akionyesha hajakubaliana na wewe unaingiwa woga?

Kwani unapoanzisha mada unafikiri wote wataikubali?

Sasa kama kabutton tu ka dislike mnakaogopa vipi komenti za kudiss mbona zinaendelea?

Basi uwanja wa comment ungeondolewa mtu anapost tunasoma tu

Hii ndio inafanya vijana wengi wa upinzani wanakimbia kupingana wao wanataka waongee watu wa lugha moja tu, nawaona wanavyoshangilia humu kama mahayawani
 
Nakubaliana na mabadiliko,huna haja ya kuona mada ambazo zinakuharibia mood,hata kama hujasoma yaliyomo,
Kichwa cha habari tu kinatosha kukuchafulia Siku,ni bora Kum- ignore mtu kama huyo
 
Back
Top Bottom