DOKEZO IGP ingilia kati kuhusu huyu Tapeli wa Dodoma Egron Rweyemamu aka Jenerali Mwamwega

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Umefanya jambo jema kutoa taarifa ili watu wakae kwa tahadhari.
Lakini kama mnamfahamu kwa nini msimkamate ili aende akajieleze kituo cha polisi?
 
Poleni. Sema hawa matapeli huwa wanaangalia IQ za watu wanaowaibia, kwa akili ya kawaida tu Generali anafanya nini bandarini mpaka kufikia hatua ya kutapeli magari?!!!
Watu bado wanatapeliwa sana kwa sababu ya uono mdogo,jeshi na bandarini wapi na wapi
 
General wako wengi sio mmoja ila CDF ndio yuko mmoja tu
Meja General,Luten General wako wengi ila General yuko mmoja labda ukihesabia na waliostaafu ndio watakuwa wengi
Mimi ni whistleblower tu, ninalifanyia upelelezi maana wamekomba bosi mmoja milioni mia mbili. Wameanza kumpanga kuanzia mwaka 2021. Ila kumpigia rasmi wameanza 2023.
Duh hao itakuwa mtandao wao ni mpana milioni 200 sio mchezo,ndugu mtoa mada uwe makini sana wasipate details zako wakikunasa utakuwa matatizoni.
Matapeli wa aina hiyo huwa wamejipanga kwenye kila nyanja ikiwemo na kwenye uchawi.
Hao ndio wale matapeli huwa wanavizia wazee wastaafu wanakuja na Business plan wanakuchanganya unaingia kingi.
Na ubaya wao yaani ukipata mkwanja mrefu wanapata taarifa kisha wanakujia ghafla.
 
Nimeshangaa sana umesema jenerali ni mmoja tu,umemuacha wapi jenerali ulimwengu?
 
Hapa kuna kitu kinanishangaza mkuu.
Unasema anawatengenezea kesi ya utakatishaji fedha,hilo faili la kesi linaandikwa wapi?kwenye kituo gani cha polisi?Na mahakama ipi inahukumu hiyo kesi?
 
Mkuu, kama umeamua kufichua hili jambo basi nivyema ukaweka kilakitu wazi hapa pamoja na ushahidi ulionao.
Angalizo: Usipende sana mambo ya PM hasa unapo fichua mambo mazito kwa maslahi ya uma.
Classmate
 
Huyu jamaa anataka kumuhamisha nchi huyu kiongozi wa dini mmoja.
 
Si mmumalize,yaani unamiliki million 200 alafu huna mguu wa kuku?
 
Ikulu ya Zanzibar hamtendi Haki kabisa. Ofisi yenu inatumika kutapeli kiongozi wa FPCT. Kuna mtu anadai yeye ni Generali wa jeshi na anafanya kazi Kama ni katibu kwenye Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar. Na amekuwa anatapeli kiongozi wa FPCT kwa kiwango Cha shilingi Milioni mia mbili na hamsini 250,000,000 alitumia jina la Mwinyi Hassan , akidai hiyo ni namba ya Rais wa Zanzibar. Imebainika ya kwamba huyo mtu ni tapeli lakini anatumia jina la ikulu ya Zanzibar na jina la Rais kuiba na kutapeli.

Huyo Generali wa jeshi alidai ana shida ya matibabu hivyo akaomba msaada kwa jina la Rais wa Zanzibar Kama mdhamini. Kapewa pesa kaingia mitini na kudanganya Rais wa Zanzibar atalipa Deni kumbe uongo.

Hapo Chini ni kielelezo Cha namba ya Simu anayotumia kutapeli kwa jina la ikulu Zanzibar na jina la Rais wa Zanzibar. Ila muhusika jina lake ni MC Egron Rweyemamu.

 
1. Tanzania jenerali ni mmoja tu CDF wewe inakuaje mtu akwambie ni jenerali.
2. Unaamini kabisa Rais Mwinyi Hana uwezo wa kumsaidia mtu matibabu mpaka aombe msaada !!!
 
Ile pesa tuma kwenye namba hii
 
Kuna tukio kubwa la utapeli kuanzia viwanja mpaka pesa za watu. Kiasi Cha milioni mia tatu. Pamoja na RCO Temeke kufungua Jalada February 2024, hakuna kilichoendelea na tapeli anaendelea kutapeli kwa jina la mama Samia.

Utapeli huu umehusisha taasisi za serikali zifuatazo:

1. JWTZ: Mhusika wa utapeli ametumia jina la Jenerali wa Jeshi, wakati sio kweli. Yani Katumia cheo Cha mkubwa wa jeshi kutapeli. JWTZ Ina taarifa lakini ipo kimya. Je huyu tapeli ana nguvu kuliko jeshi?. Nimeshangaa nguvu za huyu jamaa kiasi kwamba anaweza kutumia cheo Cha jeshi bila kukamatwa.

2. Ikulu: Huyu tapeli Katumia jina la ikulu Zanzibar na ikulu JMT kutapeli. Ikulu Zanzibar Wana taarifa ila wapo kimya, na huyo tapeli anaendelea kutapeli akitumia cheo Cha ikulu Zanzibar. Hakuna anayemkamata.

3. Jina la Waziri Mkuu: Huyu tapeli Katumia ofisi ya Waziri Mkuu kutapeli na hakuna anayemsumbua.

4. Kwa Sasa anatumia jina la Mama Samia kutapeli. Na hakuna hatua anazochukuliwa.

Cha kusikitisha vyombo vya Dola vina taarifa lakini havichukui hatua madhubuti tangu mwezi wa kumi na mbili 2023. Shida ipo wapi?
 
Hebu funguka tujue mjinga nani kabla hujalaum serikal maana kuna watu hadi leo wanatapeliwa na jamaa wa UNICEF au mikopo ya MO na Tulia huko fesibuku, watu kama hao huwez laumu serikal maan kama unaakili timamu huwez kuambiwa utume elf 10 upewe laki si bora akate huko huko akutumie elf 90! Kwahy funguka wengi wanatapeliwa kwa tamaa zao.
 
Laiti ungekuwa na upeo kidogo tu kwamba:

1. Mambo ya sheria sio hisia.
2. Mambo ya siasa sio ya kuamini.
3. Usisikilize upande mmoja wa hadithi
4. Sheria zilivyo outdated

Ungeelewa kwamba hakuna police / RCO au mahakama aliyekula rushwa.
 
Hapo kila mtu anakula sehemu yake akili yako ndio inakupa kula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…