DOKEZO IGP ingilia kati kuhusu huyu Tapeli wa Dodoma Egron Rweyemamu aka Jenerali Mwamwega

DOKEZO IGP ingilia kati kuhusu huyu Tapeli wa Dodoma Egron Rweyemamu aka Jenerali Mwamwega

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mhh,wanajuananae nn!!!?
Niliweka hapa ushahidi wa namba anayodanganya ni ya Rais Mwinyi. Na jinsi tulivyoweza kunasa namba yake na jina lake halisi. Ila Kama unavyojua kwa bongo money talks.
 
Habari, naomba nitoe taarifa kwa JWTZ ya kwamba Kuna mtu anajiita Generali Charles Mwamwega na kudanganya watu yeye ni makubwa jeshini na anafanya kazi kwenye ofisi ya Rais wa Zanzibar Ikulu. Ukienda pale ikulu Zanzibar hayupo mtu Kama huyo na ukienda kwenye data base ya JWTZ Hilo jina halipo kabisa, ukiachana na cheo Cha uongo Cha Generali ambacho ni kimoja tu kwa CDF.

Mpaka Sasa ameshatapeli watu wengi lakini hachukuliwi hatua yeyote. Maana Mimi najua Generali wa JWTZ ni mmoja inakuaje wawepo majenerali wawili?. Pia huyu Generali anatumia jina la Waziri Mkuu kuibia watu Magari pale bandarini. JWTZ ingilieni kati raia wanalizwa, wasaidieni.
sasa kabla hao uliowataja wachukue hatua,kwanini hukurepoti polisi akamatwe?
 
General ni mmoja?
Majenerali Tanzania wako wengi sema mmoja ndiye huwa kiongozi wa wengine.
La pili ni kwamba huyo anayetapeliwa ni mpuuzi anastahili kufungwa.
Mkuu ni Generali wa mwisho Yani Generali kwa CDF. Maana mwaka Jana alikuwa anajiita Luteni Generali.

Nakubaliana na wewe huyo anayetapaliwa anastahili kuchapwa fimbo sema tu ni bosi. Yani anatapeliwa milioni mia mbili kijinga. Halafu Cha kushangaza hajawahi kuonana na huyo Generali Mwamwega.
 
sasa kabla hao uliowataja wachukue hatua,kwanini hukurepoti polisi akamatwe?
Mkuu tumeenda polisi mpaka huyo anayetapeliwa akaitwa. Shida ni kwamba anayetapeliwa anakataa kwamba hatapeliwi.
 
Huyo Generali Tapeli anajiita Charles Mwamwega. Anadai ni Katibu ofisi ya Rais Zanzibar. Na kushangaza namba anayotumia kwenye MPESA inakuja na Jina Mwinyi Hassan. Kwa hivyo anadanganya watu kwamba anatumia simu ya Rais wa Zanzibar. Hivyo yeye ndio atakuwa anapiga simu na asipigiwe simu maana Rais anaweza kuipokea. Sasa siku moja tukatumia true caller application tukalipata jina lake halisi .
 
Wanaibiwaje? Au ni katika harakati za kutafuta slope?
Jamaa anajenga urafiki na wewe kwa kuangalia status yako. Anakuingia kwa gia kwamba yeye ni Generali wa JWTZ kwa maana ya cheo karibia na CDF, ukikubali tu umeliwa. Atajifanya kukuanganisha na Viongozi wakubwa .

Sasa ana simu nyingi so, anaweza kukudanganya kwamba kesho Waziri Mkuu atakupigia. Halafu kesho kweli unapigiwa simu na mtu mwenye sauti ya Waziri Mkuu kumbe Wana mtambo wa kuigiza sauti kwenye simu zao, ukisikia hivyo Unaingia line.
 
Inaonekana huyo Generali Mwamwega alitumia jina la Waziri Mkuu kumtapeli huyo bosi. Shida ya huyo bosi naye kichwani hazitoshi. Kila analoambiwa Wala hashtuki. Mtu anapigiwa simu anaambiwa una kesi ya utakatishaji naye anajaa na kuanza kulipa faini bila hata kuhoji. Huyo Generali Mwamwega kamshika kweli huyo bosi kamfanya mradi wake. Siku JF wakinikubalia nitatoa stori nzima hapa.
Ukiona hivyo boss nayeye ana makando kando kweli.

Hujafanya kosa unakubalije kosa!!!milioni 200 unazitoaje kwenye kipato halali kumhonga mtu anayekutuhumu tu!!!!
 
Kazi ya polisi hiyo, wanawalea sana matapeli na kula nao. Acha tuanze kuwatia viberiti wenyewe.
Tayari
tapatalk_1712992899113.jpg
 
Hili suala tumeshalipeleka polisi ila chenga nyingi Sana. Watu umewapa ushahidi wote lakini kila siku maneno huu mwezi wa pili.
Kwenye kesi za matapeli polisi hakuna wanachofanya zaidi ya kula rushwa pande zote mbili. Utaambiwa leta laki mbili ya kum 'track' alafu wakimpata hafiki kituoni, anawatuliza kwa hela. Baada ya hapo wanaanza kukuzungusha.
 
Back
Top Bottom