DOKEZO IGP ingilia kati kuhusu huyu Tapeli wa Dodoma Egron Rweyemamu aka Jenerali Mwamwega

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mhh,wanajuananae nn!!!?
Niliweka hapa ushahidi wa namba anayodanganya ni ya Rais Mwinyi. Na jinsi tulivyoweza kunasa namba yake na jina lake halisi. Ila Kama unavyojua kwa bongo money talks.
 
Itakuwa maana kila mtu anamkimbia. Tumeshirikisha polisi hola na wapelezi hola. Kila mtu anakuja na stori zake za uongo na kweli ila jamaa kila siku anatumiwa miamala na bosi sio Chini ya milioni Tano kwa wiki .
Kuna vitu Hii nchi viongozi wanafanya Nyuma ya pazia unaweza ukalia ukionyeshwa
 
sasa kabla hao uliowataja wachukue hatua,kwanini hukurepoti polisi akamatwe?
 
General ni mmoja?
Majenerali Tanzania wako wengi sema mmoja ndiye huwa kiongozi wa wengine.
La pili ni kwamba huyo anayetapeliwa ni mpuuzi anastahili kufungwa.
Mkuu ni Generali wa mwisho Yani Generali kwa CDF. Maana mwaka Jana alikuwa anajiita Luteni Generali.

Nakubaliana na wewe huyo anayetapaliwa anastahili kuchapwa fimbo sema tu ni bosi. Yani anatapeliwa milioni mia mbili kijinga. Halafu Cha kushangaza hajawahi kuonana na huyo Generali Mwamwega.
 
sasa kabla hao uliowataja wachukue hatua,kwanini hukurepoti polisi akamatwe?
Mkuu tumeenda polisi mpaka huyo anayetapeliwa akaitwa. Shida ni kwamba anayetapeliwa anakataa kwamba hatapeliwi.
 
Huyo Generali Tapeli anajiita Charles Mwamwega. Anadai ni Katibu ofisi ya Rais Zanzibar. Na kushangaza namba anayotumia kwenye MPESA inakuja na Jina Mwinyi Hassan. Kwa hivyo anadanganya watu kwamba anatumia simu ya Rais wa Zanzibar. Hivyo yeye ndio atakuwa anapiga simu na asipigiwe simu maana Rais anaweza kuipokea. Sasa siku moja tukatumia true caller application tukalipata jina lake halisi .
 
Wanaibiwaje? Au ni katika harakati za kutafuta slope?
Jamaa anajenga urafiki na wewe kwa kuangalia status yako. Anakuingia kwa gia kwamba yeye ni Generali wa JWTZ kwa maana ya cheo karibia na CDF, ukikubali tu umeliwa. Atajifanya kukuanganisha na Viongozi wakubwa .

Sasa ana simu nyingi so, anaweza kukudanganya kwamba kesho Waziri Mkuu atakupigia. Halafu kesho kweli unapigiwa simu na mtu mwenye sauti ya Waziri Mkuu kumbe Wana mtambo wa kuigiza sauti kwenye simu zao, ukisikia hivyo Unaingia line.
 
Ukiona hivyo boss nayeye ana makando kando kweli.

Hujafanya kosa unakubalije kosa!!!milioni 200 unazitoaje kwenye kipato halali kumhonga mtu anayekutuhumu tu!!!!
 
Hili suala tumeshalipeleka polisi ila chenga nyingi Sana. Watu umewapa ushahidi wote lakini kila siku maneno huu mwezi wa pili.
Kwenye kesi za matapeli polisi hakuna wanachofanya zaidi ya kula rushwa pande zote mbili. Utaambiwa leta laki mbili ya kum 'track' alafu wakimpata hafiki kituoni, anawatuliza kwa hela. Baada ya hapo wanaanza kukuzungusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…