IGP Simon Sirro: Magaidi wapatao 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara

Hivi hiyo idadi ya magaidi 300 ni kama platoon ngapi? Basi kwa idadi hiyo ya magaidi tena ikiwa ni kama walikuja kutesti zali tu tujihesabu kwamba hatuko salama kabisa. Kuna makubwa zaidi yanaweza kuwa yanakuja.
Mkuu wananchi tuna imani na jeshi letu.
Wengi hawajahadithiwa kile magaidi hao walichokipata kule MKIRU.(Mkuranga, Kibiti, Rufiji)
Vijana waliwapiga makonzi ya kutosha hao magaidi.
Sasa wamechokoza tutasikia mengi.
 
Acha uongo.
Hizo chopa ni za kukodi, na registration yake si unsona hapo?
Au kaujinga fulani kamekutawala.
Hizo chopa ni aina ya Bell na jeshini sidhani kama zipo hizi maana ni ndogo sana.
 
Mkuu wananchi tuna imani na jeshi letu.
Wengi hawajahadithiwa kile magaidi hao walichokipata kule MKIRU.(Mkuranga, Kibiti, Rufiji)
Vijana waliwapiga makonzi ya kutosha hao magaidi.
Sasa wamechokoza tutasikia mengi.
Kama sikosei ni wazenji waliokuwa wanajipoza maumuvu kwa kusema "....hata kama wametufunga magoli lakini chenga tumewala yahe". Tumeshaingiliwa, tusimame na kuchukua hatua.
 
Nina uhakika kuwa wako huko in hot pusuit.
Nduli hatukumuachia mpakani.
Yule ilikuwa ni vita baina ya nchi na nchi, ili huku msumbiji hatupigani na nchi kwaio ruhusa kutoka kwao lazima vyenginevyo watakuwa na haki ya kutushambulia kwa madai kuwa tumevamia ardhi yao
 
Hao wote hawakuwa wtz
 
Poleni majirani, hata kama BAADHI yenu(wale wale ambao huwa nasikia wakiitwa masisiemu) mlitucheka sana na kukenua kila mara mliposikia kwamba magaidi yamesababisha maafa nchini Kenya. Ila mna kibarua kigumu na sio kwasababu ya ugaidi tu. Naona serikali yenu ina uwezo wa kuwahesabu magaidi, 1,2,3 hadi 300. Tena wakati wa shambulizi, lakini waliouwawa hawatajwi na hawazumzi pia kuhusu idadi ya waliojeruhiwa na waliotekwa. Media za Tz nazo zipo zipo tu, uzalendo wa kuwapa taarifa na kufahamisha wananchi wenzao kuhusu suala nyeti kama hili umewapiga chenga kweli kweli. Hadi media za Mozambique na za kimataifa ndio zinawajibika zaidi yao, bure kabisa. Uwazi wa serikali na vitengo vya usalama kwenye kutoa taarifa kamili kwa wakati ufaao ni kipengele muhimu sana kwenye vita dhidi ya ugaidi. Alafu mbaya zaidi ni kwamba muda sio mrefu huu uzi utafutwa na kutupiliwa mbali kama kawa. Jf ya hapo awali ambayo iliitwa 'Swahili Wikileaks' sio hii ya sasa, very sad state of affairs.
 

Sisi style yetu ni ya kumkimbiza mwizi kimya kimya.
😛😛😛
Ukubwa wa tatizo unajulikana na wanaosababisha wanajulikana.
 
USA pamoja na ukubwa wao na tekinologia ila 11/9 walipigwa nq magaidi mpaka Pentagon ilipigwa ije iwe Tanzania
 
Magaidi walijaribu kuvamia Lugalo base ; usalama umeruhusu hawa watu wamepenya sana ; tuko nao mitaani sasa ...
 
Westgate tu magaidi hawakuzidi hata 10 lakini mziki wake tuliuona [emoji16][emoji16] hawa wanasema magaidi 300 aisee [emoji119]
Shida ya kua na policeccm wao ni kuongea wakiwa dar,si akaongelee akiwa kwenye uwanja wa mapambano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…